Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo. Mwezi wa Rajab tumeshauanza na ifuatayo ni sehemu ya kwanza ya risala …
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad ﷺ, aya hapo juu ya 36 ya Sura Tawbah, inazungumzia utukufu wa miezi minne. Mwezi Rajab, ambao ni mmojawapo kati ya miezi hiyo minne, mwezi ambao una fadhila tele. Ni mwezi ambamo dua hukubalika.
TAFSIRI: Bila shaka idadi ya miezi kwa Allah ni miezi kumi na mbili katika kitabu cha Allah tangu Alipoumba mbingu na ardhi, miongoni mwao minne ni yenye huruma (tukufu). Hii ni dini iliyonyooka na hivyo msidhulumu nafsi zenu katika miezi hizo. Na piganeni na washirikina wote kama wao wanavyopigana nanyi nyote, na jueni kuwa Allah yu pamoja na wachamungu.
Mwezi wa saba katika kalenda ya Kiislam inaitwa RAJAB, ambayo inatokana na neno "TARJIB", yenye maana ya heshima na hata zama za ujahili Waarabu waliuheshimu sana mwezi huu kwa kuacha mapigano na mauaji, wakisema ni mwezi wa Mwenyezi Mungu.
Mtume ﷺ amesema kuwa Rajab ni mwezi wa Allah, Shaaban ni wa kwangu na Ramadhani ni ya ummah wangu.
Mtume ﷺ amesema kuwa Rajab ni mwezi wenye fadhila nyingi, thawabu ya amali njema huwa maradufu ya thawabu ya kawaida. Mwenye kufunga swaum 1 ndani ya Rajab, basi ni sawa na kufunga mwaka mzima.
Siku 1 Mtume Isa Alaihissalaam alipokuwa akipita karibu na mlima mmoja, aliona nuru sehemu Fulani ya mlima. Alimuomba idhini Allah ili aweze kuzungumza na mlima. Mlima ilimuuliza nini atakacho? Mlima ikasema kuwa ndani yake kuna Mcha Mungu mmoja nan i kwa sababu ya huyo mlima una nuru. Mtume Isa Alaihissalaam alimuomba Allah aonyeshwe huyo mtu na mara mlima ikapasuka na akaonekana Mcha Mungu aliye mzuri sana. Alisema kuwa yeye ni katika watu wa Mtume Musa Alaihissalaam na alimuomba Allah Amjaalie maisha marefu ili aweze kushuhudia zama za Mtume wa mwisho Muhammad ﷺ na hivyo ahesabiwe miongoni mwa ummah wa Mtume wa mwisho. Mcha Mungu huyo alikuwa mlamani humo kwa miaka 600. Kisha Mtume Isa alimuuliza Allah kama kuna Mcha Mungu ardhini zaidi ya huyo bwana? Allah alimjibu: "Ewe Isa, lau kama mja wangu katika ummah wa Mtume wa mwisho akifunga siku moja tu ya mwezi Rajab, basi huyo mja kwangu atakuwa Mcha Mungu zaidi kuliko huyo bwana!! (SUB-HANALLAH).
Baadhi ya tarehe muhimu:
Tarehe 1 – Mtume Nuh Alaihissalaam alianza safari na wafuasi wake katika mashua (meli) waliyoitengeneza.
Tarehe 4 – Vita vya Safin
Tarehe 4 – Imam Shafi-I Rahmatullahi Alaihi kuiaga dunia
Tarehe 6 – Sayyidina Moinuddin Chishti (kiongozi wa Walii kwa twariqa ya Chishtiya) kuiaga dunia
Tarehe 27 – Msafara wa isra na Mi-iraj ya Mtume ﷺ.
Tarehe 1 Mtume Nuh na wafuasi wake walianza safari katika meli kabla ya tufani kali iliyowaangamiza waliompinga.
Tarehe 4: Imam Shafi aliaga dunia. Jina lake ni Muhammad bin Idris na kizazi chake cha 4 kinakutana na kile cha Mtume Muhammad ﷺ kwa Abdi Manaf. Amezaliwa mwaka 150 hijria na kufariki mwaka 204h mjini Cairo, Misri. Alikuwa akikhitimisha msahafu mmoja kila siku katika mwezi Ramadhani. Kila alipopatwa tatizo, basi huenda kuizuru kaburi la Imam Abu Hanifa na kisha huomba dua akimtawassul.
Tarehe 6: Walii mkubwa wa Allah Moinuddin Chishti aliaga dunia nchini India. Walii huyo alikuwa mwaka sambamba na Sheikh Abdul Qadir Jilani Qaddasallahu Sirrah. Mtume Muhammad ﷺ alimjaalia uwalii wa bara hindi. Mabaniani milioni 9 walisilimu kwa jitihada zake.
Tarehe 27: Msafara wa Isra na miraj ya Mtume Muhammad ﷺ ambayo insha Allah tutaanza kuizungumzia hapo baadae.
Maswali / maoni yanakaribishwa
JazakAllah.