Ads 468x60px

Oct 28, 2014

Sayyiduna Umar Ibn Khattaab - PT 2 (Kiswahili)



Natumai hamjambo.  Kwanza kabisa nachukua fursa kuwatakia Heri za mwaka mpya wa 1436 hijria.
Jana ulikuwa mwezi mosi Mfungo Nne (Muharram) ambamo Khalifa wa 2 wa Kiislam, Sayyidina Umar ibn Khattaab Radwiy-Allahu Anhu, aliiaga dunia. Ifuatayo ni sehemu ya mwisho ya risala.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, aya hapo juu ya 29 Sura Fatah (48) inazungumzia fadhila za Makhalifa.
TAFSIRI: Muhammad ni Mtume wa Allah, na wale walio pamoja nae ni wakali kwa makafiri ila ni wenye kuhurumiana wao kwa wao, na utawakuta wana rukuu na kusujudu.
Fadhila za Sy Umar ni nyingi mno kiasi cha kwamba si rahisi kuzichambua. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alipotaka kujua fadhila za Sy Umar, basi Jibrail alimwambia kuwa lau kama mmoja aanze kusimulia kwa muda wa umri wa Mtume Nuh Alaihissalaam, basi hatakamilisha fadhila zake. Quran inatueleza kuwa Mtume Nuh Alaihissalaam alihubiri kwa muda wa miaka 950, je umri wake?
Hivyo nimejaribu kuzichambua baadhi tu ya fadhila zake, nazo ni hizi hapa:-
1)    Ukali wake dhidi ya maadui ulikuwa maarufu sana. Baada ya vita vya Badri, alimshauri Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam kuwa makafir waliotekwa wauliwe na miongoni mwao waliokuwa jamaa zake, aliomba yeye mwenyewe awaue. Ila Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alikubali ushauri wa Sy AbuBakr ya kuchukua fidia kutoka kwa watekwa hao.
2)    Ushauri wake uliendana na Aya za Quran; mfano: munafik alipokufa, Sy Umar alimshauri Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam asisalishe jeneza lake. Mara tu aya alishuka ikiunga wazo la Sy Umar. Sy Umar pia alimshauri Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam atoe hukumu ya kusali karibu na vikanyago vya Mtume Ibrahim Alaihissalaam baada ya kutufu na mara aya ikashuka ikiunga mkono. Vile vile siku moja alipokaa kwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, Wake wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam nao walilkaa, Sy alimshauri Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam kuwaambia Wake zake kujisitiri na hijab na mara tu aya ikashuka.
3)    Sy AbuBakr alipoiaga dunia, ufalme wa Kiislam ulikuwa na ukubwa wa maili mraba 800,000. Lakini Sy Umar alipoiaga dunia ilizidi kwa maili mraba 1,400,000 na kwa maili mraba 2,200,000; ina maana kila siku alikuwa akishinda maili mraba 350.
4)    Uadilifu wake ulikuwa wa hali ya juu sana. Alikuwa akienda mahakamani peke yake na siku moja hakimu aliposimama kumheshimu, basi alifukuzwa kazi kwa sababu ya kitendo chake cha kumtukuza kiongozi wa Kiislamu, Sy Umar, kisijekueleweka vibaya kiasi cha kudhaniwa anapendelewa!! Ikiwa hakimu kadhulumu basi shitaka lake hufikishwa mwezi wa kuhiji na uadilifu hupatikana. Viongozi wa leo wasipoheshimiwa basi hukasirika.
5)    Wakati Misri ilipokombolewa chini ya uongozi wa Amr bin Aas RadwiyAllahu Anhu ambae baadaye aliteuliwa kuwa gavana wa Misri. Kuliwa na desturi ya kijahili huko Misri ambapo kila mwaka maji ya Mto Nile hupungua na hadi msichana mwenye kufikia makamu ya kuolewa huzamishwa mtoni baada ya kupambwa kama bibi harusi, ndipo mto hujaa tena. Amr bin Aas alipopelekwa taarifa za kumuandaa msichana, alisema kuwa Uislamu ni kwa ajili ya kuondoa desturi zote za kijahili na hivyo taarifa zitatumwa mjini Madina kwa Amirul Mu’uminin, Sy Umar, ili atoe amri. Sy Umar alimwandikia gavana wake wa Misri, Amr bin Aas, akimpongeza kwa kutoendeleza desturi ya kijahili na kumwambia aitumbukize barua kwenye mto! Sub-hanallah!! Makafiri kama kawaida yao wakaanza mzaha kuwa eti kiongozi wa Waislamu ameiandikia barua mto!! Kwenye barua maandishi yalikuwa hivi: Ewe maji ya mto nile, ikiwa unatiririka bila ya hukumu ya Allah, basi hatuna shida nawe, ila kama unatiririka kwa hukumu ya Allah, basi mimi Umar namuomba Allah akufanye utiririke kama mwanzo. Sub-hanallah!! Historia inasema kuwa pindi barua iliyoandikwa na Sy Umar ilipotumbukizwa tu mtoni, basi maji yalipanda hadi juu na hadi leo hii mto haujakauka!
6)    Safari moja palitokea tetemeko la ardhi mjini Madina na mara Sy Umar akasimama na kuiamrisha ardhi: ewe ardhi kwa nini unatetemeka, je Umar hajakufanyia uadilifu? Na ardhi ilisimama!! Sub-hanallah.
7)    Usiku mmoja Mama Aisha alimuuliza Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam; je kuna mtu katika ummah wako mwenye kuwa na thawabu sawa na idadi ya nyota? Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alimjibu: ndiyo, nae ni Umar bin Khattaab. Kisha aliulizwa je thawabu za AbuBakr? Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alijibu kuwa thawabu moja tu ya AbuBakr ni sawa na thawabu zote za Umar.

Maoni / maswali yanakaribishwa
JazakAllah
Kind Regards,
Muhammad KHATRI

1 comments:

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views