UWAHABI NI NINI NA NANI NI WAHABI?
الوهابية هي فرقة تتبع رجلا يسمى محمد بن عبد الوهاب الذي خرج من نجد الحجاز من حيث قال رسول الله صلى الله عليه و سلم و بها يطلع قرن الشيطان .رواه البخاري
Uwahabi\Mawahai ni kikundi cha watu wanaomfuata mtu mmoja anaitwa Muhammad bin Abdul Wahaab aliyetoka Najd (Mashariki ya Mdina al-Munawwara, na karibu na Riyadh) katika nchi ya Hijaaz (Saudi Arabia ya Leo), ambako Mtume صلى الله عليه وسلم alisema: “Na huko ndiko kutakochomoza Pembe ya Shetani (ameipokea Bukhari)
محمد بن عبد الوهاب لا يرى مسلما على وجه الارض غير جماعته و كل من خالفة يرسل له من يغتاله في فراشه لانه يقول بتكفير المسلمين و يستحل دمائهم انظر كتاب السحب الوابلة على ضـرائح الحنابلة طـُـبعَ في الريـاض مكتبة الامام احمـد - ثم الوهابية اعادوا طبع الكتاب وحذفوا الذم الذي ذكره صاحب كتاب السُّحـُـب الوابلة من الطبعة الثانية عند ترجمة والد محمد بن عبدالوهاب - ص 276 وحاشية رد المحتار على الدر المختار لإبن عابدين الحنفيّ ج4/262 و غيرهما
Muhammad bin Abdul Wahaab (mzaliwa wa Dir’iyya, Najd) anaamini kwama hakuna Mwislamu duniani, isipokuwa wafuasi wake tu; na hivyo mtu yeyote yule asiyekubaliana naye na kundi lake, humtumia watu wakamuue kitandani mwake; kwa sababu yeye anasema kuwa Waislamu wote ni makafiri (isipokuwa wafuasi wake) na hivyo ni halali kumwagwa damu zao (kuuliwa):
Angalia kitabu kiitwacho: al-Suhubul Waabilah, ala dhara’ihil Hanabila, (Mawingu yenye kutiririka mvua kubwa juu ya makaburi wa wanachuoni wa Kihanaabila) kilichopigwa chapa Riyadh, na Maktabat al-Imam Ahmad. Mawahabi baadae walikichapisha tena kitabu hiki na kundoa matusi na kashfa alizotaja Mtunzi wa kitabu hicho cha al-Suhubil Wabila, katika chapa ya pili, pale alipokuja kuandika historia ya Baba mzazi wa Muhammad bin Abdulwahaab, Ukurasa 276, na vile vile anagalia Hashiyat Raddul-Muhtaar ala al-Durar al-Mukhtar, (Fafanuzi za Pembeni mwa Kitabu cha Hashiyat Raddul-Mukhtaar) cha Ibn Aabidiin al-Hanaafi, Juzuu ya 4, Uk. 262, na katika vitabu vengine.
علماء عصره حذروا منه حتى ابوه الشيخ عبد الوهاب واخوه الشيخ سليمان , والف اخوه رسالتين في الرد عليه الاولى : فصل الخطاب في الرد على محمد بن عبد الوهاب و الثانيه : الصواعق الالهـيّـة في الردّ على الوهابية . و كذلك حذر منه مشايخه كالشيخ محمد بن سليمان الكردي في كتابه الفتاوى
Wanazuoni wa Zama zake Muhammad bin Abdul Wahaab, wametahadharisha upotofu wake; miongoni mwao ni Baba yake, mzazi, mwenyewe, Shaykh Abdul Wahaab na ndugu yake halisa Shaykh Sulauman bin Abdulwahaab, ambaye alitunga Vijitabu viwlli kumrudi na kumkosoa ndugu yake Muhammad bin Abdul Wahaab.
Kitabu kimoja alikiiita: Faslul-Khitab fi al-Raddi ala Muhammad bin Abdul Wahaab (Uchambuzi yakinifu wa kumkosoa Muhammd bin Abdul Wahaa [mpotofu].
Na kitabu cha pili amekiita: al-Swaa’iqul Ilaahiyya fi al-Radi ala al-Wahaabiyya (Minguruyo ya Radi za Mwenyezi Mungu dhidi ya Uwahabi na Mawahabi).
Vivyo hivyo, wametahadharisha dhidi yake hata walimu wake, ambao ni Mashekhe wake waliomsomesha, kama Shaykh Muhammd bin Sulayman al-Kurdi, katika kitabu chake cha Fatawa.
الوهابيه يقولون ان الله جالس على العرش ويُجلس معه محمدا يوم القيامة , والعياذ بالله من الكفر كما في كتاب مجموع الفتاوى لإبن تيميّـة الحـرَّانـي - حبيب الوهابية - ج4/374 و بدائع الفوائد ج4/40
Mawahabi wanasema: Allah ameketi juu ya Arshi na atamkalisha, pamoja Naye, Muhammd Siku ya kiyama!!! –Mwenyezi Mungu Atulinde na maneno haya ya Kufuru-; kama yanavyo semwa maneno hayo na Ibnu Taymiyya al-Harrani, Kipenzi cha Mawahabi, katika Kitabu chake, kiitwacho: Majmuu’ al-Fataawa = Majumuisho ya Fatwa zake, Juzuu ya 4, Ukrusara 374, na vile vile katika Kitabu cha Bada’I al-Fawa’id, Juzuu ya 4, ukurasa 40.
الوهابيه يدافعون عن الذي يقول , نوع العالم شريك لله في الازلية و العياذ بالله من الكفر كما في كتاب موافقة صريح المعقول ج1/75 و منهاج السنه ج1/24 و نقد مراتب الاجماع 168-شرح حديث عمران بن الحصين ص 193-شرح حديث النزول 161 وغيرها من كتب ابن تيمية الحـرَّانـي
Mawahabi wanamtetea mwenye kusema: “Baadhi ya Vilimwengu (vitu ulimwenguni) vinashirikiana na Allah katika Utangu!” -Mwenyezi Mungu atulinde na kufuru hii -.
Maneno hayo yamo kwenye kitabu kinachoitwa: Swariihul-Ma’quul, Juzuu ya 1, ukurasa 75 (Ubainifu wa kiingiacho Akilini), na Kitabu kiitwacho: Minhaaj al-Sunna, Juzuu ya 1, ukurasa, 14, na Naqd Maratib al-Ijmaa’ (Kupinga daraja za Ijmaa), ukurasa 168, Sherehe ya Hadith ya I’mraan bin al-Huswayn, Uk. 193, na Sherehe ya Hadithi al-Nuzuul (Kuteremka), ukurasa 161, na kwengineko katika Vitabu vya Ibnu Taymiyya al-Harrani.
الوهابيه يقولون : الله تعالى له فم والعياذ بالله تعالى من الكفر كما في كتابهم المسمى : السُّـنـَّـة ص77
Mawahabi wanasema: “Mwenyezi Mungu Ana Mguu”!!! – Mwenyezi Mungu atulinde na Kufuru hii- kama yalivyo semwa kwenye Kitabu kiitwacho al-Sunna, ukurasa 77.
الوهابية يقولون : امة محمد مشركة و شركها اشد من شرك عباد الاوثان كما في كتابهم مجموعة التوحيد ص 266 و 281
Mawahabi wanasema: “Umma wa Muhammad ni Washirikina, na UShirikina wao ni mbaya zaidi hata kuliko ushirikina na Wenye kuabudu masanamu!
Yanasemwa hayo kwenye kitabu cha Majmu’at al-Tawhid, Ukurasa 266 na 281.
الوهابيه يكفرون اهل الشام والمغرب واليمن والعراق ومصر كما في كتابهم فتح المجيد ص 217
Mawahabi wanasema watu wote wa Shaam (Syria, Jordan, Lebanon na Falastina), na Maghrib (Libya, Tunis, Algeria, Morocco na Mauritania), Yemen (na Hadhramout) Iraq na Misri ni Makafiri.
Yanasemwaa hayo katika kitabu chao kiitwacho Fath al-Majiid, ukurasana217.
الوهابية يدافعون عن الذي يقول ان النار تفنى لا يبقى فيها احد ويعتبرون ان له ثوابا كما في كتابهم حـادي الارواح الى بلاد الأفراح لإبن قـيـِّـم الجــوزية الزرعيّ
ص 260 و التعليق على رفع الستار ص 32
Mawahabi wanamtetea na mwenye kusema: Moto utawamaliza wataoingizwa ndani yake, na hakun atayesalia (milele) Motoni; na wanamzigatia kuwa anapata thawabu.
Yamesemwa hayo katika moja ya Vitabu vyao, kiitwacho: Haadil al-Arwaah ila bilaadil Afraah, cha Ibnu Qayyim al-Jawziyya al-Zar’iyya, ukurasa 260, na vile vile katika Kitabu kiitwacho Fafanuzi cha Kitabu kiitwcho:Raf’ al-Sitaar, (Kufunua Pazia) ukurasa 32.
الوهابيه يقولون عن حواء رضي الله عنها انها مشركه كما في كتابهم المسمى الدين الخالص ج1/ص 160
Mawahabi wanasema kuwa Mama Hawa رضي الله عنها ni Mshirikina!!
Wanasema hayo kwnye kitabu chao kiitwacho: al-Diinul-Khaaalis, (Dini Swafi=Takatifu) Juzuu ya Kwanza, Ukurasa 160.
الوهابيه يتهمون الصحابي الجليل بلال بن الحارث المزني رضي الله عنه بالكفر و الاشراك كما في تعليقهم على كتاب فتح الباري , طبع دار الريان للتراث ج2/575
Mawahabi wanamshutumu Swahaba Mkubwa, Bilal bin al-Harish al-Muzani رضى الله عنه kuwa Mshirikina na Kafiri
Wnayasema hayo katika maelezo yao ya kufafanfua kitabu cha Fath al-Baari, kilichochapiwa na Dar al-Rayyyan Li al-Turaath, Juzuuu ya 2, ukurasa 575.
الوهابيه يقولون ابو جهل و ابو لهب اكثر توحيدا و اخلص ايمانا من هؤلاء المسلمين الذين يقولون لا اله الا الله محمد رسول الله كما في كتابهم المسمى كيف نفهم التوحيد ص 16
Mawahabi wanasema: Abu Jahl na Abu Lahb ni watu wenye msimamo mwingi zaidi wa Tawhidi (kutomshirikisha Allah) na Imani safi zaidi kuliko Waislamu wanaosema La Ilaha Illal-Laah, Muhammad Rasulul-Laah.
Wanayasema hayo kwenye kitabu chao kiitwacho: Kayfa Nafham al-Tawhid (Vipi Tunaelewa maana ya Tawhid) ukurasa 16.
الوهابيه يكفرون من التزم و قلد مذهبا معينا من المذاهب الاربعة كما في كتابهم هل المسلم ملزم باتباع مذهب معين من المذاهب الاربعة و يقولون ان التقليد عين الشرك كما في شريط مسجل بصوت احد زعمائهم
Mawahabi wanasema mtu yeyote anayefuata moja kwa moja (pasi na kusaili ) madhehebu maalum, miongoni mwa madhehebu mane (ya Ahlul-Sunna wal Jamaa) ni Kafiri.
Wanasema hayo katika Kitabu chao kiitwacho: Hal al-Muslim multazam bi itbaa’ madhhabin mu’ayyan min al-madhahib al-Arba’a (Je, ni kweli kwamba Mwislamu hana budi kufuata mojawapo wa madhehebu mane?) na wanasema kufuata nyuma tu (katika Dini) ndiyo ushirikina wenyewe haswa, maneno hayo yamo kwenye kanda zilzisajiliwa za mawaidha ya mmojawapo wa viongozi wao.
الله تعالى قال : ان الله لا يغفر ان يشرك به , الايه و الوهابيه تقول ان الله يغفر بعض الشرك كما في كتاب فتاوي الالباني ص 351
Mwenyezi Mungu Amesema: Hakika Allah Hasamehe kushirikishwa na kitu chochote”
Mawahabi wanasema Mwenyezi Mungu Anasamehe baadhi ya ushirikina.
Yanapatikana maelezo hayo kaika kitabu cha Fatwa za al-Albani, ukurasa 351.
الامام البخاري أوّل في صحيحة قول الله تعالى ( كل شىء هالك الاو جهه ) سورة القصص 88 فقال الا ملكه و الوهابيه تقول من يؤول هذا التؤيل لا يكون مسلما كما في كتاب فتاوى الالباني ص523
Imam Bukhari رحمه الله amepambanua neno WAJHUHU, katika Qauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: “Kila kitu kitaangamia isipokuwa Wajhuhu” kwamba neno Wajhuhu maana yake “Ufalme Wake”.
Mawahabi wanasema yeyote anayefaisri Wajhuhu kuwa ni Ufalme wake hawezi kuwa Mwislamu. Maneno hayo yapo kwenye Kitabu Fatawa al-Algni, ukurasa 523.
الوهابيه يقولون من أراد أن يصلي أو يصوم فقال بلسانه نويت أن اصلي او نويت ان اصوم يعذب في النار و العياذ بالله كما في الجريده المسماه
Australia Islamic review 26 march 9 April 1996 page 10
Mawahabi wanasema: Mtu yeyote anayetaka kuswali au kufunga akatia nia kwa kutamka kwa ulimi wake: Nawaytu an Uswalli au Nawayti an Aswuma (Nanuwia Kuswali,……., au Nanuwia kuunga….. ) basi ataadhibiwa kwa Moto [ataingia Motoni!].
Wanasema hayo katika Jarida liiitwalo Ausralia Islamic Revie, toleo la March 26, na April 9, mwaka 1996, ukurasa 10.
الوهابيه يستحلون دم كل من صلى على النبي صلى الله عليه وسلم جهرا بعد الآذان ويعتبرونه اشد من الزنا انظر اواخر كتاب :تاريخ السلطنه العثمانيه وانظر كتاب الدليل الكافي
Mawahabi wanasema inajuzu kumua mtu anayemsalia Mtume صلى الله عليه وسلم kwa sauti, baada ya Adhana; na wanazingatia kufanya hivyo kuwa ni kubaya zaidi kuliko kuzini.
Angalia mwisho wa Kitabu kiitwacho: Tarikh al-Sultwanat al-UKthmaaniyya (Historia ya Ufalme wa Ottomans) na angalia vile vile Kitabu kiitwacho al-Dalil al-Kaafi.
الوهابية يحرمون الاحتفال بمولد النبي صلى الله عليه و سلم كما في كتابهم فتاوى مهمة ص 45 و كادوا أن يكفروا من احتفل بالمولد كما في كتابهم صيانة الإنسان ص 233 و أجازوا لانفسهم أن يجتمعوا لدراسة سيرة محمد بن عبد الوهاب بمناسبة مرور كذا عام على و لادتة أو وفاته في ظل ندوات أو مؤتمرات ينفق عليها المال الوفير انظر كتاب هذا و الدي ص 123
Mawahabi wanaharamisha kusherehekea Maulidi ya Kuzaliwa kwa Mtume صلى الله عليه وسلم na wapo karibu sana na kumkufurisha mwenye kusherehekea kwa kusoma Maulidi, kama walivyo eleza hayo kwenye kitabu chao kiitwacho: Swiyaanat al-Insaan (Kumlinda Mwanadamu) ukurasa 233.
Hata hivyo, wanaruhusu na kujuzisha kukusanhyika na kusoma Historia ya Muhammad bin Abdul Wahaab, na kusherhekea kutimiza miaka kadha wa kadha, tokea kuzaliwa kwake hadi kufa kwake. Wanafanya hayo katika Makongamano na Mikutano mbali mbali, ambapo hutumiwa fedha nyingi sana.
Angalia kitabu kiitwacho: Hadha Waalidi (Huyu Ndiye Baba yuangu) ukurasa 123.
[Nyongeza: Na wanafanya kila mwaka sherehe kubwa za kumbukumbu zinazofanyika Janaadiriyya; kuadhimisha mambo hayo hayo, tamaduni zao za kibedui, ikiwa pamoja na tarehe za kuadhimisha utawala wa wafalme wa ukoo wa Wasaudi, wafalme wao]
الوهابية يجعلون قراءة القران على الأموات المسلمين من الضلال كما في كتاب فتاوى مهمة ص 32
Mawahabi wanasema Kumsomea khitma maiti wa Kiislamu ni upotofu.
Wanasema hayo kwenye kitabu chao kiitwacho: Fatawa Muhimma (Fatwa zilizo muhimu sana).Ukursa 32.
الوهابية يحرمون على المسلمين أن يقولوا في تشيع الجنازة وحدوا الله كما في كتابهم الموت عظاته و أحكامه ص 26 هامش 1
Mawahabi wanasema ni HARAMU kwa Waislamu kusindikiza Jeneza huku wakisema: Wahhiduuh! (Semeni La Ilaha Illal-Laah!).
Wanasema hayo katika kitabu chao kiitwacho: Almawt: ‘Idhwatuhu wa Ahkaamuhu (Mauti: Mafunzo yake na Hukumu zake), ukurasa 26.
الوهابية يحرمون زيارة الأحياء للأحياء في العيدين كما في كتابهم فتاوى الألباني ص 63
Mawahabi wanasema ni Haramu Watu kutembeleana wenyewe kwa wenyewe katika Siku Kuu mbili za Kiiislamu: Iidi al-Fitr na Iid al-Adh-ha. Yamo hayo kwenye kitabu chao cha Fataawa al-Albani, ukurasa 63.
علي رضي الله عنه يقول : الخروج في العيدين إلى الجبانة من السنة رواة البيهقي و الوهابية يقولون حرام زيارة المقابر في العيدين كما في كتابهم فتاوى الألباني
Imam Aliyy كرم الله وجهه anasema: “Kuwenda kutembelea viunga vya maiti (walikozikwa Waislamu), katika Sikukuu mbili za Idi ni miongoni mwa Sunna” ameipokea al-Bayhaqi.
Mawahabi wanasema ni HARAMU kuzuru makaburi siku za Idi mbili. Yap ohayo kwenye kitabu chao Fatawa al-Albani.
الوهابية يريدون أن يهدموا قبة رسول الله صلى الله عليه و سلم الخضراء و يشجعون على ذلك كما في كتابهم تحذير الساجد ص 68
Mawahabi wanataka kuvunja Kuba la Kijani, juu ya Kaburi la Mtume صلى الله عليه وسلم na wanawahimiza wahusika (Watawala wa Saudi Arabia) wafanye hivyo [ila Watawala hao wanahofia hasira za Waislamu Duniani].
Yamo hayo katika kitabu chao kiitwcho: Tahdhiir al-Saajid (Onyo kwa mwenye kusujuudu\kuswali) ukurasa 68.
4 الرسول صلى الله عليه و سلم يقول من زار قبري و جبت له شفاعتي . صححه الحافظ السبكي و غيره و الوهابية يحرمون السفر لزيارة النبي عليه الصلاة و السلام كما في كتابهم الفتاوى الكبرى ص 142
Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: Ataye zuru kaburi langu, ni budi kupata Shafaa (Maombezi) yangu” imepokewa na kusahihishwa na al-Hafidh al-Subki na wengine.
Mawahabi wanasema ni HARAMU kufung safari kwenda kumzuru Mtume صلى الله عليه وسلم . Yamo hayo katika kitabu chao kiitwacho al-Fatawa al-Kubraa, ukurasa 142.
الرسول صلى الله عليه و سلم يقول إذا كانت ليلة النصف من شعبان فقوموا ليلها و صوموا نهارها . رواه ابن ماجه و الوهابية يحرمون قيام ليلها و صيام نهارها في كتابهم فتاوى مهمة ص 57
Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: Ukiingia usiku na nusu ya pili ya mwezi wa Shaabani, simameni usiku kwa Ibadan na fungeni mchana wake” Ameipokea Ibn Majah.
Mawahabi wanasema ni Haramu Kusimama kwa ibada usiku wa nusu ya Shaabani na kufunga mchana wake.
Yanasemwa hayo kwenye vitabu vyao, kama Fatawa Muhimma, ukurasa 57.
الله تعالى مدح الذين عزروا النبي صلى الله عليه و سلم أي عظموه بقوله ( فالذين ءامنوا به و عزروه و نصروه و اتبعوا النور الذي انزل معه أولئك هم المفلحون ) الآية 157 سورة الأعراف و الوهابية يستبيحون دم من يعظم رسول الله صلى الله عليه و سلم كما في كتابهم مجموعة التوحيد ص 139
Mwenyezi Mungu amewasifu waliomfuata na kumuamini Mtume صلى الله عليه وسلسم kwa kusema: “Basi waliomuamini yeye, na wakamtukuza na kumsaidia (kumnusuru) na wakaifuta nuru – hao ndio wenye kufanikiwa” al-A’raaf: 157.
Mawahabi wanasema mwenye kumtukuza Mtume سلى الله عليه وسلم anaweza kuuliwa!
Wanasema hayo katika Kitabu chao: Majmu’at al-Tawhid, ukurasa 139.
الرسول صلى الله عليه و سلم يقول و الذي نفسي بيده لقتل مؤمن اعظم عند الله من زوال الدنيا رواه النسائي . الوهابية يستبيحون دم المسلمين فقد دخلوا إلى شرقي الأردن فذبحوا النساء و الأطفال حتى بلغ عدد القتلى 2750من المسلمين انظر جريدة الصفا 21 اب 1924
Mtume صلى الله عليه وسلم anasema: “Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, kumuua Mwenye kuamini ni kubaya zaidi kuliko kutoweka (kuiangamiza) Dunia” ameipokea Nasai.
Mawahabi wamehalalisha kumwaga damu za Waislamu; waliinngia mashariki ya Jordan na kuchinga wanawake wa Kiislamu na watoto wengi hadi kufikia waliouliwa kuwa 2750. Analia Jarida la Al-Swafa, tole la Augosti, 1924.
و حتى أمواتنا المسلمين لم يسلموا منهم فقد دخلوا إلى اليمن و نبشوا القبور بالجرافات و كانوا مزودين بالقاذفات الصاروخية و الرشاشات انظر جريدة نداء الوطن 3/9/1994 تحت عنوان يهاجمون أضرحة أولياء عدن
Hata Waislamu waliokwisha kufa hawakusallimika nao! Kwani waliingia Yemen na kufukua makaburi kwa kutumia matingatinga, na walikuwa wakitumia makombora na bunduki.
Soma jarida la Nidaa’ al-Watwan, toleo 3/9/1994, chini ya Kichwa cha Habari: Wahujumu makaburi ya Mawalii, Aden.
الوهابية استباحوا دم جماعة التبليغ و كفروا زعمائهم الشيخ خالد النقشبندي و الشيخ محمد الياس و الشيخ محمد زكريا و الشيخ محمد انعام الحسن رحمهم الله انظر كتابهم : القول البليغ في التحذير من جماعة التبليغ
Mawahabi wamejuzisha kuwaua Jamaa wa Tabligh, na kuwakufurisha Viongozi wao kama Shaykh Khalid al-Naqshabandi, Shaykh Muhammd Ilyaas, Shaykh Muhammad Zakariyya na Shaykh Muhammd In’aam al-Hsan رحمهم الله .
Angalia Kitabu chao : al-Qawl al-Baliigh fi al-Tahdhiir min Jama’at al-Tabligh (Tamko lilio wazi kabisa la kutahadharisha dhidi ya Kundi la Tabligh).
اتفق المسلون على أن الآية ( ليس كمثله شئ و هو السميع البصير ) الآية 11 سورة الشورى فيها تنزيه لله عن مشابهة المخلوقين أما الوهابية يقولون هذه الآية لا تخلو من تشبيه لله بخلقة كما في كتاب بغية المرتاد ص 178
Waislamu wameafikiana kwa kauli moja kuwa Aya isemayo: “Hapana kitu kama mfano Wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona” al-Shuura: 11, kwamba Aya hiyo inamtakasa Mwenyezi Mungu Allah na mshabawa wowote na Viumbe chochote.
Mawahabi, hata hivyo, wanasema kuwa “Aya hii haikani kutokuweko mshabaha wa Allah na viumbe Vyake”
Maneno hayo yamo katika Kitabu chao kiitwacho: Bughyat al-Murtaad, ukurasa 178.
الصحابي الجليل عبد الله بن عمرو كان يعلق على أعناق أطفاله الحروز التي من كتاب الله أو من ذكر الله روى ذلك الترمذي و البخاري في كتابه خلق أفعال العباد و غيرهما و أما الوهابية فيحرمون ذلك و يجعلون ذلك من و سائل الشرك كما في كتابهم فتاوى مهمة ص 111
Mmojawapo wa Maswahaba wakubwa, ‘Abdullah bin ‘Amr رضي الله عنه alikuwa akiwavisha watoto wake hirizi shingoni mwao, za Aya kutoka Kitabu cha Mwenyezi Mungu, au Majina ya Mwenyezi Mungu. Ameipokea Tirmidhi na Bukhari katika Kitabu chake Imam Bukhari kiitwacho: Kitaab Khalq Af’aal al-‘Ibaada, na katika vitvu vyake vengine.
Mawahabi, hata hivyo, wanaharamisha hivyo na wanasema kuvaa hirizi ni miongoni mwa njia za ushirikina, wanasema hayo katika Kitabu chao Fatawaa Muhimma, ukurasa 111.
الرسول صلى الله عليه و سلم أباح للنساء لبس الذهب كما روى ذلك ابن ماجه و غيره و الألباني الوهابي يحرم لبس الأساور و الحلق و الخاتم و نحوه من الذهب على النساء كما في كتابه آداب الزفاف ص 132
Mtume صلى الله عليه وسلم amewahalalishia Wanawake kuvaa dhahabu, kama ilivyopokewa katika Hadithi kutoka Sunan Ibn Majah.
Al-Bani,kinara wa, UWahabi, anaharamisha kuvaa bangili, vikuku, pete na mapambo mengine ya dhahabu, kwa wanawake!
Angalia kitabu chake: Aadaab al-Zafaaf (Maadili ya Harusi), ukurasa 132.
الصحابي الجليل أبو هريرة كان له خيط طويل فيه من العقد ألفان يسبح الله كل يوم اثنتي عشر ألف تسبيحه رواة ابن سعد في طبقاته و الوهابية يحرمون حمل السبحة لذكر الله كما في مجلة التمدن
Abu Hurayra, mmojawapo wa Maswahaba wakubwa wa Mtume صلى الله عليه وسلم alikuwa na Kamba ndefu, yenye mfundo 2000, ambayo alikuwa akiitumia, kila siku, -kama Tasbihi- kukmsabbih Allah, mara elfu 10. Ameipokea Ibn Sa’d katika kitabu chake al-Twabaqaat.
Mawahabi wanasema Haramu kutumia Tasbihi kumtaja Mwenyei Mungu. Wamesema maneno hayo kwenye Jarida la al-Tamaddun.
الوهابية يحرمون على الإمام و المأموم رفع الأيدي للدعاء عقب الصلاة و تامين المأموم خلف الإمام كما في مجلتهم ذكرى العدد السابع 1991 ص 16
Mawahabi wanaharamisha kuinua mikono juu na kuomba dua kwa sauti na kuitikia amin, kwa Imamu na Maamuma, baada ya Swala za Faradhi.
Yamo maneno hayo kwenye Jarida lao, toleo la 7, Mwaka 1991, ukurasa wa 16.
الرسول صلى الله عليه و سلم علم رجلا أعمى أن يقول اللهم إني أسألك و أتوجه إليك بنبيك محمد نبي الرحمة يا محمد إني أتوجه بك إلى ربي في حاجتي لتقضى لي صححه الطبراني و غيره و الوهابية يكفرون المتوسلين و المستغيثين برسول الله صلى الله عليه و سلم كما في كتابهم مجموعة التوحيد ص 139
Mtume صلى الله عليه وسلم alimfundisha KIPOFU kuomba kwa kusema: اللهم إنى أسالك وأتوجه إليك بنبيك محمد نبي الرحمة يا محمد إنى أتوجه بك إلى ربى فى حاجتى لتقضى لى [Ewe Mola wangu! Nakuomba na naelekea Kwako kupitia kwa Mtume Wako, Muhammad, Mtume wa Rehema. Ewe Muhammd! Mimi naelekea, kupitia wewe, kwa Mola wangu, kwa haja yangu, anikidhie” Ameiswahihisha al-Tabarani na wengine.
Mawahabi wanawakufurisha wenye kutwasali na wenye kuomba kwa jina la Mjumbe wa Mwenyezi Mungu صلى الله عليه وسلم .
Wameyasema hayo kwenye kitabu chao Majmu’at al-Tawhid, ukurasa 139.
الرسول صلى الله عليه و سلم توضأ بمكوك رواه مسلم و المكوك ستة أمداد و المد يساوي ثلاثة أرباع كوب من الماء تقريبا و الألباني الوهابي يحرم الوضوء بأكثر من مد كما نشرت عنه مجلة التمدن
Mtume صلى الله عليه وسلم alitawadha kwa kutumia maji ya ujazo wa kibirika MUKUUK. Ameipokea Muslim. Na Kibirika cha Mukuku ni sawa navibaba sita, na kila kibaba ni sawa na robo tatu ya gilasi ya kawaida.
Albani Wahabi anaharamisha kutawadha kwa maji kupindukia kibaba kimoja. Amechapisha hayo kwenye jarida la al-Tamaddun.
الرسول صلى الله عليه و سلم اغتسل بخمسة مكاكيك رواه مسلم و الألباني الوهابي يحرم الاغتسال بأكثر من أربعة أمداد كما نشرت عنهم مجلة التمدن
Mtume صلى الله عليه وسلم alikuwa akioga kwa kutumia Vibirika vitano vya MUKUUK, kama alivyoipokea Muslim.
Albani Wahabi anasema ni haramu kukoga kwa kutumia maji zaidi ya wiangi wa vibaba vine. Amechapisha hayo kwenye jarida lao al-Tamddun.
الألباني الوهابي يحرم على المسلمين صلاة التراويح عشرين ركعة كما في كتابه صلاة التراويح
Albani Wahabi anasema ni haramu kwa Waislamu kuswali Tarawehe rakaa 20. Amesema hayo katika kitabu chake al-Tarwiih.
الوهابية يطعنون بسيدنا عمر بن عبد العزيز رضي الله عنه فيقولون الغبار الذي دخل انف فرس معاوية افضل من عمر بن عبد العزيز بألف مرة . انظر كتابهم إطلاق الأعنة ص16 و مجلتهم نداء الإسلام العدد الخامس جمادى الآخرة 1415
Mawahabi wanamdharau na kumnyanyasa Sayyidina Uar bin Abd al-Aziz (Khalifa, mchamungu, ambaye ahulu-Sunna wanamzigatia kuwa ni Khalifa Muadilifu wa Tano, baada ya Mkhalifa wane wa mwanzo), kwa kusema kuwa vumbi la ndani ya pua ya farasi wa Mu’awiya ni bora mara alfu moja, kuliko Umar bin Abd al-Aziz.
Angalia kitabu chao kiitwacho: Itlaaq al-A’inna, ukurasa 16, na jarida lao Nida’ al-Islaam, toleo la tano, Mfungo Nane, 1415.
الوهابية يقولون عن عقيدة الأزهر انها عقيدة شركيه و الأزهر يخرج عاهات كما في مجلتهم الذكرى و شريط مسجل بصوتهم
Mawahabi wanasema: Itikadi inayofundishwa kwenye Chuo Kikuu cha Al-Azhar Misri ni itikadi ya Ushirikina, na kwamba Chuo hicho Kikuu kinazalisha Punguani tu.
Wamesema hayo katika Jarida lao liitwalo al-Dhikraa, na kanda za sauti za viongozi wao.
الوهابية يطالبون بالصلح الدائم مع اليهود بلا قيد و لا شرط انظر جريدة التلغراف العدد 2754 في 23/كانون الأول /1994
Mawahabi wametoa Wito wa kuwa na mkataba wa suluhu ya Amani ya kudumu na Mayahudi (Wazayoni) pasi na mashari yoyote, wala vizuwizi vyovyote.
Angalia Gazeti la Telegraph, Nambari 2754, la tarehe 23, Disemba, 1994.
الوهابية يحرمون على المسلمين البقاء في فلسطين و يأمروهم بالخروج منها و تركها لليهود كما في كتابهم فتاوى الألباني ص 18 و جريدة اللواء الأردنية في 7/8/1992 و شريط مسجل بصوت أحد زعمائهم
Mawahabi wanawakataza Waislamu kusalia Falastina na wanawataka wahame na kuondoka katika Ardhi hiyo na kuwaachia Mayahudi.
Yamesemwaa hayo katika Fatwa za al-Albani, ukurasa 18, na vile vile katika Jarida la al-Liwaa’ la Jordan, toleo 7/8/1992, na vile vile katika kanda za sauti za mmojawapo wa mashekhe wao.
الوهابية يقولون إن الشيخ حسن البنا رحمه الله مشرك من الدعاة إلى الشرك و الضلال كما في مجلتهم ( المجلة) العدد ى830 كانون الثاني 1996
Mawahabi wanasema: Sheikh Hasan al-Banna رحمه الله ni mshirikina, na ni mmojawapo wa viongozi wanaolingania ushirikina na upotofu.
Yamesemwa hayo kwenye Jarida lao al-Majallah, Nambari 830, Januari, 1996.
الوهابية يشجعون على الزنا فيفتون لمن طلق امرأته بالثلاثة دفعة وآحده أن يحسبها مره ( أي طلقة واحدة يعني الثلاثة بواحدة ) و يعاشر زوجته كما في مجلتهم الدعوة 909
Mawahabi wanahalalisha Zina, kwa kusema kwamba Mwenye kumtaliki mkewe kwa kumwambia “Nimekuacha talaqa tatu!”, kwa mpigo moja, basi bado mwanamke huyo ni mkewe (yaani ameachika talaka moja tu) na hivyo anendelea naye kama mkewe wa kawaida, na kufanya naye tendo la ndoa.
Yamesemwa hayo kwenye Jarida lao al-Al-Da’wa,Namb. 909.
الوهابية يقولون اذا قبل الصائم أو لمس أو باشر أو جامع دون الفرج فانزل المني أو المذي لا يفطر كما نقل صاحب كتاب الإنصاف عن زعيمهم ج 3 ص 301 و 315
Mawahabi wanasema: Mtu aliyefunga, akambusu mkewe, au akamgusa, au akamkumbatia, au akafanya naye tendo la ndoa pasi na kumuingilia kwenye utupu, na akatokwa na manii, au madhy, kwa kufanya hivyo, basi swaumu yake iko Swahihi.
Amenukuuu hayo Mtunzi wa Kitabu cha al-Inswaaf, akimnukuu kiongozi wa Mawahabi, angalia ukurasaa,301 na 315, juzuu ya 3.
الوهابية يقولون الاستمناء أي إخراج المني سواء كان سببه تقبيل الرجل لزوجته أو ضمها إليه أو كان باليد لا يفطر كما في كتابهم تمام المنه ص 418
Mawahabi wanasema: Kupiga ponyeto, yaani kujichua hadi kutokwa na manii, iwe kwa mkono wake, au kwa kumbusu mkewe au kumkumbatia, hakuharibu Swaumu. Yamo kwenye kitabu chao Tamaam al-Minna, ukurasa 418.
الصحابي الجليل عبد الله بن عمر رضي الله عنهما قال يا محمد لما خدرت رجله - رواه البخاري في كتابه الأدب المفرد - و الوهابية تقول من قال يا محمد فهو كافر مهدور الدم كما في كتابهم الاصول الثلاثة
Mmojawapo wa Maswahaba wakubwa, Abdullah bin Umar رضي الله عنهما alisema:يا محمد alipokufa ganzi mguu wake (akashindwa kusimama), ameipokea Bukhari.
Mawahabi wanasema: Mwenye kuita “Ya Muhammad!”, amekufuru na anastahiki kuuawa. Wameyasea hayo kwenye Kitabu chao kiitwacho: al-Usuul al-Thalathah (Misingi mikuu mitatu!)
معناه كفروا الصحابي عبد الله بن عمر و كفروا البخاري و رواة هذا الأثر من السلف و الخلف أي كفروا أمة محمد صلى الله عليه و سلم
Kwa maana hiyo, basi wamemkufurisha Abdullah bin Umar رضي الله عنهما na Imam Bukhari رحمه الله, bali na wapokezi wa Hadithi hiyo, tokea watu waliotangulia na hadi waliowafuata baada yao; yaani Wameukufurisha Umma mzima wa Mtume Muhammad صلى الله عليه وسلم
الوهابية يحرمون على المسلمين أن يجتمعوا على قراءة القران أو تعليم درس ديني قبل صلاة الجمعة كما في مجلتهم ذكرى العدد السادس آب 1991 ص 25 و 26
Mawahabi wanaharamisha Waislamu kukusanyika pamoja kwa kusoma Qur’ani au kusoma darasa yoyote ya Dini kabla ya Swala ya Ijumaa.
Wamesema hayo kwwenye Jarida lao al-Dhikraa, toleo la 5, Augosti, mwaka 1991, uk wa 25 hadi 26.
5 الوهابية يحرمون قول صدق الله العظيم بعد قراءة القرءان كما في مجلتهم البحوث العلمية
Mwahabi wanaharamisha kusema صدق الله العظيم baada ya kusoma Qur’ani. Wamesema hayo kwenye jarida lao al-Buhuuth al-Islaamiya, toleo la 5.
****
فيا أحباب رسول الله يا من تخافون على دين الله اعملوا بحديث الرسول صلى الله عليه و سلم ( من رأى منكم منكرا فليغيره بيده فان لم يستطع فبلسانه فان لم يستطع فبقلبه )
Hivyo basi, enyo wapenzi wa Mtume صلى الله عليه وسلم! Enyi mnaye muogopa Alla katika mambo ya Dini! Tekelezeni mafunzo ya Hadithi ya Mtume صلى الله عليه وسلم isemayo: “Mwenye kukona munkari, miongoni mwenu, auondoe kwa mkono wake. Na kama hana uwezo, basi (angalau) kwa ulimi wake. Na kama hawezi basi (angalau) kwa moyo wake”
و الحديث الآخر حيث قال الرسول عليه السلام ( إلى متى ترعون عن ذكر الفاجر اذكروه بما فيه كي يحذره الناس )
Na Hadithi nyengine, ambapo Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: “Mpaka lini mtaona haya kumtaja kwa jina Mtu muvu! Mtajeni kwa sifa zake za uovu ili watu wameuepuke!”
و عملا بكلام الرسول عليه السلام حذروا من أهل الكفر الوهابية و من على شاكلتهم و لكم الثواب إن شاء الله
Na ili tuweze kutii maneno ya Mtume صلى الله عليه وسلم Watahadharisheni na waonyeni watu dhidi ya Mawahabi Wanao kufurusha watu, na dhidi ya yeyote yule mwenye kufuata nyayo zao, ili mjipatie Thawabu kutoka kwa Allah, in sha Allah.
Jipatie Thawabu: Isambaze kwa Waislamu wengine ili kuwatahadharisha na Uwahabi, Mawahabi na Vizazi vyao vya Salafiyya, Answaarus-Sunna, ISIS, DAISH, BOKO HARAMU, AL-SHABAAB, pamoja na Vibaraka wao wengine wanaoimba nyimbo zao potofu!