Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo. Mwezi 6 Rajab mmoja katika kiongozi wa masharifu kwa tarika ya Chishti aliiaga dunia na ifuatayo ni risala fupi.
SULTAN MUINUDDIN CHISHTI RAHIMAHULLAH.
Sultan Muinuddin Chishti Rahimahullah alizaliwa Khorasan, Afghanistan. Alikuwa mwaka sambamba na Sayyid AbdulQadir Jilani Qaddasallahu Sirrah. Kwa kuwa Sayyid AbdulQadir Jilani Qaddasallahu Sirrah alishachaguliwa kuiongoza bara la Uarabuni kuhuisha dini, Mtume ﷺ alimchagua Sultan Muinuddin Chishti Rahimahullah kuiongoza bara Hindi katika kuinusuru dini. Hakuwahi kupita maeneo ya bara Hindi wala hakufahamu kabisa lugha ya kihindi. Mtume ﷺ alimjia kwenye ndoto na kumuonyesha njia ya kwenda bara Hindi na kisha alimtemea mate matukufu na hivyo akafahamu lugha ya kihindi kwa fasaha.
Kutokana na karama zake, wachawi wa kibaniani wakajua huo ni uchawi, hivyo mfalme wa huko aliwakusanya wachawi wakubwa kukabiliana nae lakini wote walishindwa na hatimaye kusilimu. Zaidi ya mabaniani milioni 9 walisilimu kutokana na karama zake tofauti. Hatimaye aliiaga dunia mwezi 6 Rajab.
Maswali / maoni yanakaribishwa
JazakAllah.
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...