Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo. Tunamalizia masimulizi ya Khalifa wa kwanza wa Kiislam, Sayyidina AbuBakr Siddiq RadwiyAllahu Anhu, ambaye aliiaga dunia hii mwezi 22 Mfungo 9, ambayo ni kesho Jumanne.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad ﷺ, aya hapo juu ya 40 kutoka Sura Tawba inayoelezea fadhila mmojawapo ya Khalifa wa 1 wa Kiislam, Sayyidina AbuBakr Siddiq na ndiye tutakaemzungumzia kwani tarehe 22 ya mfungo huu 9 aliiaga dunia.
TAFSIRI: Wakati wawili (Mtume ﷺ na Sy AbuBakr) walipokuwa ndani ya pango, mmoja alimuambia mwenzake usihuzunike, hakika Allah yuko pamoja nasi.
FADHILA: Ingawa Sayyidina Abu Bakr Siddiq Radwiyallahu Anhu alikuwa mtu mwenye fadhila nyingi, lakini pamoja na yote hayo, kubwa zaidi ni kuwa vizazi vyake vinne (4) walikuwa Masahaba. 1 – Yeye mwenyewe Radwiyallahu Anhu. 2 – Baba yake, Abu Quhafa Radwiyallahu Anhu. 3 – Mwanae, AbdulRahman Radwiyallahu Anhu 4 – Mjukue, Abu Atiq Muhammad Radwiyallahu Anhu.
Baadhi ya mambo muhimu ya Sayyidina Abu Bakr Siddiq Radwiyallahu Anhu alikuwa wa kwanza:
1 – Kusilimu.
2 – Kukiita Quran Tukufu "MSAHAFU" (Kitabu).
3 – Kuikusanya Quran Tukufu baada ya Mtume ﷺ.
4 – Kupigana na makafiri
5 – Kuwa Khalifa
6 – Khalifa aliyeanza ukhalifa katika uhai wa baba yake.
7 – Kumchagua Khalifa atakaemfuata.
8 – Kujenga hazina.
9 – Kuitwa Khalifa.
10 – Kujenga Msikiti miongoni mwa Waislamu.
11 – Miongoni mwa wafuasi wa Mtume ﷺ kuingia Peponi.
Kuhusu fadhila za Sayyidina Abu Bakr Siddiq Radwiyallahu Anhu, kuna aya nyingi za Quran Tukufu na Hadithi pia; kati ya hizo Hadithi 181 zimepokelewa katika fadhila zake tu, Hadithi 88 zimepokelewa na Sayyidina Abu Bakr & Sayyidina Umar bin Khattab Radwiyallahu Anhuma, 17 zimepokelewa na Abu Bakr, Umar & Uthman bin Affan Radwiyallahu Anhum, 14 zimepokelewa na Makhalifa wote wanne, 16 zimepokelewa na Makhalifa wote wane pamoja na Masahaba wengine. Hivyo, katika jumla ya Hadithi 316, Mtume ﷺ ametuthibitishia fadhila ya sahiba wake wa pango, Sayyidina Abu Bakr Siddiq Radwiyallahu Anhu.
Matukio matatu muhimu sana yalitokea wakati wa Ukahlifa wake:
1. Mtume ﷺ aliipeleka jeshi la Masahaba shupavu na wakati bado ilikuwa katika kitongoji cha mji wa Madina, Mtume ﷺ aliiaga dunia. Baadhi ya Masahaba walimshauri Sy AbuBakr kuirejesha jeshi hilo ili kama kukitokea mchafuko wowote, basi watasaidia. Sy AbuBakr alisema hawezi kuirudisha jeshi ambalo Mtume ﷺ alishaituma.
2. Alijitokeza Musailmah bin Kazzaab aliyedai utume, akawa na wafuasi laki moja. Sy AbuBakr aliituma jeshi ya Masahaba shupavu 10,000 kukabiliana nae huko Yamama. Waislamu hao wachache walishinda ila wale waliohifadhi Quran wapatao 700 waliuawa mashahidi. Baada ya hapo ndipo Sy AbuBakr alianza kazi ya kuikusanya Quran iwe msahafu.
3. Kundi la Masahaba walimjia Sy AbuBakr wakidai kuwa kwa kuwa Mtume ﷺ ameshaiaga dunia, basi na wao hawatatoa zaka. Sy AbuBakr alisimama kwa ujasiri na kutangaza jihad dhidi yao na kusema kuwa kila yule aliyetoa japo mbuzi, atahakikisha anafanya hivyo.
Imani ina matawi 360 na Sy AbuBakr alijaaliwa matawi yote. Siku ya Qiyama, kila atakaeingia Peponi, ataitwa kupitia mlango maalumu kutokana na alivyo kithirisha ibada fulani; mfano kama mtu alikithirisha sana saumu, basi ataitwa kupitia mlango wa wenye kufunga saum. Sy AbuBakr ataitwa kupitia milango yote, inamaanisha alikuwa mkamilifu wa kila ibada.
Maswali na maoni yanakaribishwa.
Jazak Allah.