Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo. Mfungo tulionao ni wa TISA (JAMADI-UL-AKHAR), ambamo katika tarehe 22, Khalifa wa kwanza wa Kiislam, Sayyidina AbuBakr Siddiq RadwiyAllahu Anhu aliiaga dunia hii. Ifuatayo ni risala fupi kuhusu baadhi ya fadhila zake.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad ﷺ, aya hapo juu ya 40 kutoka Sura Tawba inayoelezea fadhila mmojawapo ya Khalifa wa 1 wa Kiislam, Sayyidina AbuBakr Siddiq na ndiye tutakaemzungumzia kwani tarehe 22 ya mfungo huu 9 aliiaga dunia.
TAFSIRI: Wakati wawili (Mtume ﷺ na Sy AbuBakr) walipokuwa ndani ya pango, mmoja alimuambia mwenzake usihuzunike, hakika Allah yuko pamoja nasi.
Jina lake hasa ni Abdullah, ila AbuBakr likawa maarufu na Siddiq alipewa na Mtume ﷺ kwa kusadikisha msafara wa Miiraj. AbuBakr kamwe hakuabudu masanamu hata kabla ya kusilimu wala hakuwahi kunywa pombe kipindi bado haijaharamishwa; na alisema hawezi kutumwa kinywaji kinachoua akili ya binadamu. Baada ya kuwa na uwezo kutembea, baba yake (Abu Quhafa) alimpeleka mbele ya sanamu na kumuambia kuwa huyu (sanamu) ndiye mungu wetu anaetulisha, visha na kutupa kila kitu. Sy AbuBakr akasimama mbele ya sanamu na kusema: mimi nina njaa nilishe, nina kiuu ninyweshe, sina nguo nivishe. Alipoona kimya, alichukua jiwe na kulipiga sanamu na ikaanguka. Baba yake alikasirika sana na kumpiga kibao kisha kumburuza hadi nyumbani na akamwambia mkewe : hebu mfundishe mwanao, leo kampiga mungu wetu, hana adabu huyo. Mkewe alimjibu: ewe Abu Quhafa, naomba usimwambie chochote huyu mwanetu, kwani nilipomzaa nilisikia sauti ikisema: umebarikiwa mtoto atakaekuwa rafiki wa karibu wa Muhammad ﷺ, Mtume wa mwisho. Mimi simjui huyu Muhammad ﷺ ni nani.
Kisa cha kusilimu kwake; Sy AbuBakr alikuwa katika safari zake za biashara nchini Shaam (Syria), ambapo padiri mmoja aliziona alama fulani zilizotajwa kwenye vitabu vya kikristo kuhusu Sy AbuBakr. Padiri alimuambia arudi Makkah haraka kwani rafiki yake wa karibu, Mtume ﷺ, atakapotangaza Utume, yeye awe karibu nae. Sy AbuBakr alipofika kwa Mtume ﷺ, alimwambia kuwa anamuamini sana ila anahitaji aonyeshwe muujiza mmoja tu ili roho yake itulie. Mtume ﷺ alimuambia kuwa anahitaji muujiza gani zaidi ya kuambiwa na padiri huko nchi ya Shaam kuhusu kutangaza kwangu Utume. Papo kwa hapo Sy AbuBakr alisilimu. Hivyo alikuwa wa mwanzo kusilimu.
Sy AbuBakr alijitolea mali yake yote kwa ajili ya Mtume ﷺ na Uislam. Baada ya kusilimu tu, Sy AbuBakr alimletea Mtume ﷺ dinar 40,000 kwa matumizi atakavyo Mtume ﷺ mwenyewe. Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam alisema kuwa Uislamu umepata faida sana kupitia mali ya Sy AbuBakr kuliko mali ya Sahaba yeyote.
Sy Abubakr hakuabudu sanamu wala kunywa pombe, kabla ya kusilimu, na katika enzi ambazo ilikuwa haiajaharamishwa na kusema kuwa pombe inaua akili ya binadamu kwa hiyo sikuona sababu kuitumia ambapo inanipa hasara tu!
Sy Abubakr alikuwa karibu sana na Mtume ﷺ kila mara. Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam amesema kuwa kila aliyempa wito wa Uislamu, kwanza alikataa isipokuwa Sy Abubakr aliyekubali mara moja.
Sy Abubakr ndiye aliyemkomboa Bilal bin Rabah kwa pesa nyingi mno pale alipoteswa kwa sababu ya kusilimu.
Maswali na maoni yanakaribishwa.
JazakAllah.
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...