Ads 468x60px

Mar 14, 2017

SAYYIDINA ABUBAKR SIDDIQ - PT 2 [Kiswahili]

Assalaamu alaikum,

 

Natumai hamjambo. Tunaendelea na masimulizi ya Khalifa wa kwanza wa Kiislam, Sayyidina AbuBakr Siddiq RadwiyAllahu Anhu, ambae siku yake ni Jumanne ya tarehe 21/3/2017..

 

 

Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad , aya hapo juu ya 40 kutoka Sura Tawba inayoelezea fadhila mmojawapo ya Khalifa wa 1 wa Kiislam, Sayyidina AbuBakr Siddiq na ndiye tutakaemzungumzia kwani tarehe 22 ya mfungo huu 9 aliiaga dunia.

TAFSIRI: Wakati wawili (Mtume na Sy AbuBakr) walipokuwa ndani ya pango, mmoja alimuambia mwenzake usihuzunike, hakika Allah yuko pamoja nasi.

 

Sy Abubakr alipofuatana na Mtume kutoka Makkah kuhamia Madina, njiani alimbeba Mtume mgongoni na kutembea juu ya vidole vya mguu kwa kuhofia makafiri wasije kuyafuata vikanyago. Walipojipumzisha kwenye pango, Sy Abubakr aliingia kwanza kuisafisha na kuziba matundu yote, kisha ikabaki tundu moja tu, aliloziba kwa kidole cha mguu. Kumbe ndani alikuwa nyoka wa zama za Mtume Musa aliyetaka kumuona Mtume . Aliposhindwa kupita kwenye matundu, ndipo alimng'ata Sy Abubakr. Kwa kuwa Mtume aliweka kichwa chake kitukufu kwenye paja la Sy Abubakr na alilala, Sy Abubakr alivumilia sana maumivu makali ya kung'atwa na nyoka na wala hakutikisika. Ila machozi yalibubujika kwenye uso tukufu wa Mtume na ndipo Mtume aliamka na kufahamishwa hali halisi. Mtume alimpaka mate yake matukufu Sy Abubakr sehemu alipong'atwa na maumivu yalitoweka.

 

 

Wakati wa ugonjwa wake, Mtume alimsimamisha kwenye nafasi yake Sy Abubakr kuwa Imamu wa Masahaba.

 

Mtume alipoaga dunia, Masahab walichangayikiwa kabisa na Sy Umar alitembea na panga akisema "yeyote atakaesema kuwa Mtume ametuondoka, basi nitamuua". Lakini Allah Alimjaalia ushupavu Sy Abubakr, alipoingia Msikitini na kuanza kuwatuliza Masahaba, kisha alisimama juu ya mimbar. Alisoma aya ya 144 ya Sura Aali Imran : na Muhammad hakuwa ila ni Mtume. Na wamekwishapita kabla yake Mitume, je akifariki na kuuawa basi mtageuka kurudi nyuma? Na atakaegeuka kurudi nyuma, huyo hatamdhuru kitu Allah. Na Allah Atawalipa wanaomshukuru. Baada ya kumaliza aya hiyo ndipo Masahaba walitulia.

 

Alichaguliwa Khalifa wa Kiislamu kwa kura zote za Masahaba wote akiwemo Sayyidina Ali RadwiyAllahu Anhu, aliyekiri kuwa yule aliyechaguliwa na Mtume kuiongoza umma katika sala (imamu), basi bila shaka anapaswa kuwa Khalifa wetu. Ieleweke kuwa mwenye kupinga Usahaba wa AbuBakr, basi bila shaka anazikataa aya za Quran Tukufu na kwa hali hiyo atajiondoa katika Uislam.

 

Sayyidina AbuBakr alikuwa mjasiri na shupavu sana kiasi cha kwamba wakati wa Mtume kuiaga dunia, baadhi ya mambo magumu yalijitokeza lakini aliyatatua kwa ujasiri mkubwa. Mmojawapo ikiwa: Mtume alituma jeshi la Masahaba shupavu na bado walikuwa ndani ya kitongoji cha mji wa Madina wakati Mtume alipoiaga dunia. Baadhi ya Masahaba walipomuomba Sayyidina AbuBakr kurejesha jeshi hilo ili kukabiliana na vurugu ikiwa zitatokea, alikataa kwa madai kuwa Mtume alishaituma jeshi hilo na hivyo yeye hawezi kuirejesha.

 

Pia baadhi ya Masahaba walikataa kutoa zaka baada ya Mtume kuiaga dunia, lakini Sayyidina AbuBakr kwa ujasiri wake alihakikisha kila mstahiki wa kutoa zaka anatekeleza amri hiyo hata kama ikibidi kukabiliana nao kwa jihad.

 

Bado hali ilikuwa haijatulia vizuri, mara akajitokeza Musailm bin Kazzaab aliyedai utume. Wafuasi wake walifikia 100,000 dhidi ya jeshi la Waislam kiasi cha 10,000; Waislam walishinda vita hivyo.

 

Maswali na maoni yanakaribishwa.

 

JazakAllah.

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views