Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo.
Mfungo tulionao ni wa tisa (mwezi Jamadi-ul-Akhar) ambamo katika tarehe 22 Khalifa wa kwanza wa Kiislam, Sayyidina AbuBakr Siddiq RadwiyAllahu Anhu aliiaga dunia. Hivyo ifuatayo ni sehemu ya kwanza ya risala.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad SwallAllahu Alaihi wasallam, aya hapo juu ya 40 kutoka Sura Tawba inayoelezea fadhila mmojawapo ya Khalifa wa 1 wa Kiislam, Sayyidina AbuBakr Siddiq na ndiye tutakaemzungumzia kwani tarehe 22 ya mfungo huu 9 aliiaga dunia.
TAFSIRI: Wakati wawili (Mtume SwallAllahu Alaihi Wasallam na Sy AbuBakr) walipokuwa ndani ya pango, mmoja alimuambia mwenzake usihuzunike, hakika Allah yuko pamoja nasi.
Jina lake hasa ni Abdullah, ila AbuBakr likawa maarufu na Siddiq alipewa na Mtume SwallAllahu Alaihi Wasallam kwa kusadikisha msafara wa Miiraj. AbuBakr kamwe hakuabudu masanamu hata kabla ya kusilimu wala hakuwahi kunywa pombe kipindi bado haijaharamishwa; na alisema hawezi kutumwa kinywaji kinachoua akili ya binadamu. Baada ya kuwa na uwezo kutembea, baba yake (Abu Quhafa) alimpeleka mbele ya sanamu na kumuambia kuwa huyu (sanamu) ndiye mungu wetu anaetulisha, visha na kutupa kila kitu. Sy AbuBakr akasimama mbele ya sanamu na kusema: mimi nina njaa nilishe, nina kiuu ninyweshe, sina nguo nivishe. Alipoona kimya, alichukua jiwe na kulipiga sanamu na ikaanguka. Baba yake alikasirika sana na kumpiga kibao kisha kumburuza hadi nyumbani na akamwambia mkewe : hebu mfundishe mwanao, leo kampiga mungu wetu, hana adabu huyo. Mkewe alimjibu: ewe Abu Quhafa, naomba usimwambie chochote huyu mwanetu, kwani nilipomzaa nilisikia sauti ikisema: umebarikiwa mtoto atakaekuwa rafiki wa karibu wa Muhammad SwallAllahu Alaihi Wasallam, Mtume wa mwisho. Mimi simjui huyu Muhammad SwallAllahu Alaihi Wasallam ni nani.
Kisa cha kusilimu kwake; Sy AbuBakr alikuwa katika safari zake za biashara nchini Shaam (Syria), ambapo padiri mmoja aliziona alama fulani zilizotajwa kwenye vitabu vya kikristo kuhusu Sy AbuBakr. Padiri alimuambia arudi Makkah haraka kwani rafiki yake wa karibu, Mtume SwallAllahu Alaihi Wasallam, atakapotangaza Utume, yeye awe karibu nae. Sy AbuBakr alipofika kwa Mtume SwallAllahu Alaihi Wasallam, alimwambia kuwa anamuamini sana ila anahitaji aonyeshwe muujiza mmoja tu ili roho yake itulie. Mtume SwallAllahu Alaihi Wasallam alimuambia kuwa anahitaji muujiza gani zaidi ya kuambiwa na padiri huko nchi ya Shaam kuhusu kutangaza kwangu Utume. Papo kwa hapo Sy AbuBakr alisilimu. Hivyo alikuwa wa mwanzo kusilimu.
Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...