Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo.
Tunaendelea na risala ya Sayyidina AbuBakr Siddiq RadwiyAllahu Anhu.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, aya hapo juu ya 40 kutoka Sura Tawba inayoelezea fadhila mmojawapo ya Khalifa wa 1 wa Kiislam, Sayyidina AbuBakr Siddiq na ndiye tutakaemzungumzia kwani tarehe 22 ya mfungo huu 9 aliiaga dunia.
TAFSIRI: Wakati wawili (Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam na Sy AbuBakr) walipokuwa ndani ya pango, mmoja alimuambia mwenzake usihuzunike, hakika Allah yuko pamoja nasi.
Sy AbuBakr alijitolea mali yake yote kwa ajili ya Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam na Uislam. Baada ya kusilimu tu, Sy AbuBakr alimletea Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam dinar 40,000 kwa matumizi atakavyo Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam mwenyewe. Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam alisema kuwa Uislamu umepata faida sana kupitia mali ya Sy AbuBakr kuliko mali ya Sahaba yeyote.
Sy Abubakr hakuabudu sanamu wala kunywa pombe, kabla ya kusilimu, na katika enzi ambazo ilikuwa haiajaharamishwa na kusema kuwa pombe inaua akili ya binadamu kwa hiyo sikuona sababu kuitumia ambapo inanipa hasara tu!
Sy Abubakr alikuwa karibu sana na Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam kila mara. Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam amesema kuwa kila aliyempa wito wa Uislamu, kwanza alikataa isipokuwa Sy Abubakr aliyekubali mara moja.
Sy Abubakr ndiye aliyemkomboa Bilal bin Rabah kwa pesa nyingi mno pale alipoteswa kwa sababu ya kusilimu.
Sy Abubakr alipofuatana na Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam kutoka Makkah kuhamia Madina, njiani alimbeba Mtume mgongoni na kutembea juu ya vidole vya mguu kwa kuhofia makafiri wasije kuyafuata vikanyago. Walipojipumzisha kwenye pango, Sy Abubakr aliingia kwanza kuisafisha na kuziba matundu yote, kisha ikabaki tundu moja tu, aliloziba kwa kidole cha mguu. Kumbe ndani alikuwa nyoka wa zama za Mtume Musa aliyetaka kumuona Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam. Aliposhindwa kupita kwenye matundu, ndipo alimng’ata Sy Abubakr. Kwa kuwa Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam aliweka kichwa chake kitukufu kwenye paja la Sy Abubakr na alilala, Sy Abubakr alivumilia sana maumivu makali ya kung’atwa na nyoka na wala hakutikisika. Ila machozi yalibubujika kwenye uso tukufu wa Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam na ndipo Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam aliamka na kufahamishwa hali halisi. Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam alimpaka mate yake matukufu Sy Abubakr sehemu alipong’atwa na maumivu yalitoweka.
Wakati wa ugonjwa wake, Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam alimsimamisha kwenye nafasi yake Sy Abubakr kuwa Imamu wa Masahaba.
Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam alipoaga dunia, Masahab walichangayikiwa kabisa na Sy Umar alitembea na panga akisema “yeyote atakaesema kuwa Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam ametuondoka, basi nitamuua”. Lakini Allah Alimjaalia ushupavu Sy Abubakr, alipoingia Msikitini na kuanza kuwatuliza Masahaba, kisha alisimama juu ya mimbar. Alisoma aya ya 144 ya Sura Aali Imran : na Muhammad hakuwa ila ni Mtume. Na wamekwishapita kabla yake Mitume, je akifariki na kuuawa basi mtageuka kurudi nyuma? Na atakaegeuka kurudi nyuma, huyo hatamdhuru kitu Allah. Na Allah Atawalipa wanaomshukuru. Baada ya kumaliza aya hiyo ndipo Masahaba walitulia.
Alichaguliwa Khalifa wa Kiislamu kwa kura zote za Masahaba wote akiwemo Sayyidina Ali RadwiyAllahu Anhu, aliyekiri kuwa yule aliyechaguliwa na Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam kuiongoza umma katika sala (imamu), basi bila shaka anapaswa kuwa Khalifa wetu. Ieleweke kuwa mwenye kupinga Usahaba wa AbuBakr, basi bila shaka anazikataa aya za Quran Tukufu na kwa hali hiyo atajiondoa katika Uislam.
Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...