Assalaamu alaikum,
Naomba niwajuze kuwa MUFTI MENK, kutoka Zimbabwe anatarajiwa hapa Tanzania katika siku zinazokuja.
TAHADHARI NA TAFAKARI
Huyu bwana ni mwenye kumkashifu Mtume wetu Mpendwa ﷺ na ni mwenye itikadi potofu ya kiwahabi na salafi.
Ninazo clips ambamo amemfanyia mzaha Mtume ﷺ kwa kuuliza "eti Mtume alifahamu (lugha ya) kichina? Je alifahamu (nchi ya) Uchina ulipo?" kisha watu wakacheka. Astaghfirullah!
Kwenye clip nyingine, anadai kuwa eti "Mtume ﷺ alikuwa na husuda, chuki, nk na ndiyo maana moyo wake ulisafishwa na maji ya zam zam wakati wa safari ya isra na miraj", Astaghfirullah!!
Watu kama hawa ndugu zanguni ni msiba mkubwa kwa Waislam.
Nawaombeni sana make mbali na watu kama hawa na muwatahadharishe na Waislam walioko karibu nawe.
Allah Atuhifadhi na waovu kama hao, AMIN.
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...