Ads 468x60px

Apr 29, 2017

Ze Rehmat Yak Nazar Bar Haal e Zaram Ya Rasool Allah ﷺ



Ze rehmat yak nazar bar haal-e-zaram Ya Rasool Allah

Ghareebam, beynawayam, khaaksaram Ya Rasool Allah


Tui taskeen-e-dil, araam-e-jaan, sabr o qarar-e-man

Rukh-e-pur noor banuma, bey qararam Ya Rasool Allah


Dam e aakhir numai jalwah deedar Jaami
Ze lutfe tu hamee umeedwaaram Ya Rasool Allah

Ya Rasool Allah Sall'Allahu Alaihi Wasallam, Please cast one blessed glance on my state,
I am in distress, in need of aid and assistance Ya Rasool Allah!
( Sall'Allahu Alaihi Wasallam)

Only you are the solace to my heart,
Only You are the comfort for my soul,
Only You are the peace and contentment for my heart.
Bless me with the honour of your Blessed vision for I am restless and yearning Ya Rasool Allah.
( Sall'Allahu Alaihi Wasallam)

When it is the time of death bless Jaami with the honour of your vision,
I live with this hope from your Mercy Ya Rasool Allah.
(Sall'Allahu Alaihi Wasallam)


Huzoor Molana Abdul Rahman Jami Alayhirrahmah.

Translated by khaakpaaye Imam Ahmad Raza Radi Allahu Anhu
Faqeer Mohammed Shakeel Qadiri Ridawi.

Imam Azam Abu Hanifa by Hadrat Abdullah ibn Mubarak Radi Allahu Anhhum

Imam al Muslimeen,Imam al Aimma Sayyidunaa Imam Azam Abu Hanifah Numaan Ibn Thabit Radi Allahu Taala Anhu 

by Hadrat Abdullah ibn Mubarak Radi Allahu anhu 





لقد زان البلاد ومن عليها 
إمام المسلمين أبو حنيفه 

امام المسلمين امام ابو حنیفه رضى الله عنه نے شہروں اور شہریوں کو زینت بخشی

Imam al Muslimeen Abu Hanifah Radi Allahu Anhu blessed the towns and its people with beauty. 




باحكام واثار وفقه 
كأيات الزبور على صحيفه

احکام (قرآن) آثار (احادیث) اور فقہ سے جیسے صحیفہ میں زبور کی آیات نے

With the beauty of Ahkaam (Quran e Kareem ) and Athaar (Ahadith Shareefah ) and with the beauty of Fiqh ,as the pages were decorated by the verses of the Zabur

فما في المشرقين له نظير 
ولا في المغربين ولا بكوفه 

کوفہ بلکہ مشرق و مغرب میں ان کی نظیر نہیں ملتی (یعنی روئے زمین میں ان جیسا کوئی نہیں ہے)

He has no parallel in Kufa 
or indeed the East or the West 

بيت مشمرا سهرا لليالي 
وصام نهاره لله خيفه 

(آپ) عبادت کے لئے مستعد بیداری میں راتیں بسر کرتے اور خوف (خدا) کی وجہ سے دن کو روزے رکھتے

He spent his nights in worship 
And fasted throughout the days out of fear of The Almighty 


وصان لسانه عن كل إفك 
وما زالت جوارحه عفيفه 

انہوں نے اپنی زبان ہر بہتان طرازی سے محفوظ رکھی اور ان کے اعضاء (ہر گناہ سے) پاک رہے

He kept his tongue free from blame and accusations 
And his body free from all sins 


يعف عن المحارم والملاهي 
ومرضاتة الإله له وظيفه 

آپ لہو و لعب اور حرام کاموں سے بچے رہے رضائے الہی کا حصول آپ کا وظیفہ تھا

He stayed away from all Haram and futile activities 
Gaining the Almighty's pleasure was his wazifah 


رايت العاتبين له سفاما  
خلاف الحق مع حجج ضعيفه

امام اعظم رضی اللہ عنہ کے نکتہ چین بے وقوف مخالف حق اور کمزور دلائل والے ہیں

The ones who pick faults, are foolish ,against the truth and with weak evidence 

وكيف يحل أن يو ذي فقيه
له في الأرض آثار شريفه

ایسے فقیہ کو کسی بھی وجہ سے تکلیف دینا کیونکر جائز  ہے جس کے علمی فیوض تمام دنیا میں پھیلے ہوئے ہے

How is it valid to cause pain to such a Faqeeh 
whose grace and favour of  knowledge has blessed the whole world


وقد قال ابن إدريس مقالا 
صحيح النقل في حكم لطيفه

حالانکہ صحيح روایت میں لطیف حکمتوں کے ضمن میں امام شافعی رضی اللہ عنہ نے فرمایا کہ

Imam Shafii has stated a saheehul naql in the hukm of lateef

بان الناس في فقه عيال 
على فقه الإمام أبي حنيفه

تمام لوگ فقہ میں امام ابو حنیفہ رضی اللہ عنہ کی فقہ کا محتاج ہیں

And that is, that everyone in fiqh is dependant on the fiqh of Imam Azam Abu Hanifah 

  فلعنة ربنا أعدد رمل 
على من زد قول أبي حنيفه

ریت کے ذروں کے برابر اس شخص پر اللہ تعالٰی کی لعنت ہو جو امام ابو حنیفہ رضی اللہ عنہ کے قول کو مردود قرار دے

May Allah's curse equal to the particles of sand 
be on those who disregard the qowl of Imam Azam Abu Hanifah. 

TAKEN FROM 
DURR AL MUKHTAR SHAREEF 

Translated by khaakpaaye Imam Ahmad Raza
Faqeer Mohammed Shakeel Qadiri Ridawi

Mar 20, 2017

SAYYIDINA ABUBAKR SIDDIQ - PT 3 [Kiswahili]

Assalaamu alaikum,

 

Natumai hamjambo. Tunamalizia masimulizi ya Khalifa wa kwanza wa Kiislam, Sayyidina AbuBakr Siddiq RadwiyAllahu Anhu, ambaye aliiaga dunia hii mwezi 22 Mfungo 9, ambayo ni kesho Jumanne.

 

 

Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad , aya hapo juu ya 40 kutoka Sura Tawba inayoelezea fadhila mmojawapo ya Khalifa wa 1 wa Kiislam, Sayyidina AbuBakr Siddiq na ndiye tutakaemzungumzia kwani tarehe 22 ya mfungo huu 9 aliiaga dunia.

TAFSIRI: Wakati wawili (Mtume na Sy AbuBakr) walipokuwa ndani ya pango, mmoja alimuambia mwenzake usihuzunike, hakika Allah yuko pamoja nasi.

 

FADHILA: Ingawa Sayyidina Abu Bakr Siddiq Radwiyallahu Anhu alikuwa mtu mwenye fadhila nyingi, lakini pamoja na yote hayo, kubwa zaidi ni kuwa vizazi vyake vinne (4) walikuwa Masahaba.  1 – Yeye mwenyewe Radwiyallahu Anhu.   2 – Baba yake, Abu Quhafa Radwiyallahu Anhu.    3 – Mwanae, AbdulRahman Radwiyallahu Anhu     4 – Mjukue, Abu Atiq Muhammad Radwiyallahu Anhu.

 

Baadhi ya mambo muhimu ya Sayyidina Abu Bakr Siddiq Radwiyallahu Anhu alikuwa wa kwanza:

1 – Kusilimu.

2 – Kukiita Quran Tukufu "MSAHAFU" (Kitabu).

3 – Kuikusanya Quran Tukufu baada ya Mtume .

4 – Kupigana na makafiri

5 – Kuwa Khalifa

6 – Khalifa aliyeanza ukhalifa katika uhai wa baba yake.

7 – Kumchagua Khalifa atakaemfuata.

8 – Kujenga hazina.

9 – Kuitwa Khalifa.

10 – Kujenga Msikiti miongoni mwa Waislamu.

11 – Miongoni mwa wafuasi wa Mtume kuingia Peponi.

 

Kuhusu fadhila za Sayyidina Abu Bakr Siddiq Radwiyallahu Anhu, kuna aya nyingi za Quran Tukufu na Hadithi pia; kati ya hizo Hadithi 181 zimepokelewa katika fadhila zake tu, Hadithi 88 zimepokelewa na Sayyidina Abu Bakr & Sayyidina Umar bin Khattab Radwiyallahu Anhuma, 17 zimepokelewa na Abu Bakr, Umar & Uthman bin Affan Radwiyallahu Anhum, 14 zimepokelewa na Makhalifa wote wanne, 16 zimepokelewa na Makhalifa wote wane pamoja na Masahaba wengine. Hivyo, katika jumla ya Hadithi 316, Mtume ametuthibitishia fadhila ya sahiba wake wa pango, Sayyidina Abu Bakr Siddiq Radwiyallahu Anhu.

 

 

Matukio matatu muhimu sana yalitokea wakati wa Ukahlifa wake:

1. Mtume aliipeleka jeshi la Masahaba shupavu na wakati bado ilikuwa katika kitongoji cha mji wa Madina, Mtume aliiaga dunia. Baadhi ya Masahaba walimshauri Sy AbuBakr kuirejesha jeshi hilo ili kama kukitokea mchafuko wowote, basi watasaidia. Sy AbuBakr alisema hawezi kuirudisha jeshi ambalo Mtume alishaituma.

 

2. Alijitokeza Musailmah bin Kazzaab aliyedai utume, akawa na wafuasi laki moja. Sy AbuBakr aliituma jeshi ya Masahaba shupavu 10,000 kukabiliana nae huko Yamama. Waislamu hao wachache walishinda ila wale waliohifadhi Quran wapatao 700 waliuawa mashahidi. Baada ya hapo ndipo Sy AbuBakr alianza kazi ya kuikusanya Quran iwe msahafu.

 

 

3. Kundi la Masahaba walimjia Sy AbuBakr wakidai kuwa kwa kuwa Mtume ameshaiaga dunia, basi na wao hawatatoa zaka. Sy AbuBakr alisimama kwa ujasiri na kutangaza jihad dhidi yao na kusema kuwa kila yule aliyetoa japo mbuzi, atahakikisha anafanya hivyo.


Imani ina matawi 360 na Sy AbuBakr alijaaliwa matawi yote. Siku ya Qiyama, kila atakaeingia Peponi, ataitwa kupitia mlango maalumu kutokana na alivyo kithirisha ibada fulani; mfano kama mtu alikithirisha sana saumu, basi ataitwa kupitia mlango wa wenye kufunga saum. Sy AbuBakr ataitwa kupitia milango yote, inamaanisha alikuwa mkamilifu wa kila ibada.

 

Maswali na maoni yanakaribishwa.


Jazak Allah.

Mar 14, 2017

SAYYIDINA ABUBAKR SIDDIQ - PT 2 [Kiswahili]

Assalaamu alaikum,

 

Natumai hamjambo. Tunaendelea na masimulizi ya Khalifa wa kwanza wa Kiislam, Sayyidina AbuBakr Siddiq RadwiyAllahu Anhu, ambae siku yake ni Jumanne ya tarehe 21/3/2017..

 

 

Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad , aya hapo juu ya 40 kutoka Sura Tawba inayoelezea fadhila mmojawapo ya Khalifa wa 1 wa Kiislam, Sayyidina AbuBakr Siddiq na ndiye tutakaemzungumzia kwani tarehe 22 ya mfungo huu 9 aliiaga dunia.

TAFSIRI: Wakati wawili (Mtume na Sy AbuBakr) walipokuwa ndani ya pango, mmoja alimuambia mwenzake usihuzunike, hakika Allah yuko pamoja nasi.

 

Sy Abubakr alipofuatana na Mtume kutoka Makkah kuhamia Madina, njiani alimbeba Mtume mgongoni na kutembea juu ya vidole vya mguu kwa kuhofia makafiri wasije kuyafuata vikanyago. Walipojipumzisha kwenye pango, Sy Abubakr aliingia kwanza kuisafisha na kuziba matundu yote, kisha ikabaki tundu moja tu, aliloziba kwa kidole cha mguu. Kumbe ndani alikuwa nyoka wa zama za Mtume Musa aliyetaka kumuona Mtume . Aliposhindwa kupita kwenye matundu, ndipo alimng'ata Sy Abubakr. Kwa kuwa Mtume aliweka kichwa chake kitukufu kwenye paja la Sy Abubakr na alilala, Sy Abubakr alivumilia sana maumivu makali ya kung'atwa na nyoka na wala hakutikisika. Ila machozi yalibubujika kwenye uso tukufu wa Mtume na ndipo Mtume aliamka na kufahamishwa hali halisi. Mtume alimpaka mate yake matukufu Sy Abubakr sehemu alipong'atwa na maumivu yalitoweka.

 

 

Wakati wa ugonjwa wake, Mtume alimsimamisha kwenye nafasi yake Sy Abubakr kuwa Imamu wa Masahaba.

 

Mtume alipoaga dunia, Masahab walichangayikiwa kabisa na Sy Umar alitembea na panga akisema "yeyote atakaesema kuwa Mtume ametuondoka, basi nitamuua". Lakini Allah Alimjaalia ushupavu Sy Abubakr, alipoingia Msikitini na kuanza kuwatuliza Masahaba, kisha alisimama juu ya mimbar. Alisoma aya ya 144 ya Sura Aali Imran : na Muhammad hakuwa ila ni Mtume. Na wamekwishapita kabla yake Mitume, je akifariki na kuuawa basi mtageuka kurudi nyuma? Na atakaegeuka kurudi nyuma, huyo hatamdhuru kitu Allah. Na Allah Atawalipa wanaomshukuru. Baada ya kumaliza aya hiyo ndipo Masahaba walitulia.

 

Alichaguliwa Khalifa wa Kiislamu kwa kura zote za Masahaba wote akiwemo Sayyidina Ali RadwiyAllahu Anhu, aliyekiri kuwa yule aliyechaguliwa na Mtume kuiongoza umma katika sala (imamu), basi bila shaka anapaswa kuwa Khalifa wetu. Ieleweke kuwa mwenye kupinga Usahaba wa AbuBakr, basi bila shaka anazikataa aya za Quran Tukufu na kwa hali hiyo atajiondoa katika Uislam.

 

Sayyidina AbuBakr alikuwa mjasiri na shupavu sana kiasi cha kwamba wakati wa Mtume kuiaga dunia, baadhi ya mambo magumu yalijitokeza lakini aliyatatua kwa ujasiri mkubwa. Mmojawapo ikiwa: Mtume alituma jeshi la Masahaba shupavu na bado walikuwa ndani ya kitongoji cha mji wa Madina wakati Mtume alipoiaga dunia. Baadhi ya Masahaba walipomuomba Sayyidina AbuBakr kurejesha jeshi hilo ili kukabiliana na vurugu ikiwa zitatokea, alikataa kwa madai kuwa Mtume alishaituma jeshi hilo na hivyo yeye hawezi kuirejesha.

 

Pia baadhi ya Masahaba walikataa kutoa zaka baada ya Mtume kuiaga dunia, lakini Sayyidina AbuBakr kwa ujasiri wake alihakikisha kila mstahiki wa kutoa zaka anatekeleza amri hiyo hata kama ikibidi kukabiliana nao kwa jihad.

 

Bado hali ilikuwa haijatulia vizuri, mara akajitokeza Musailm bin Kazzaab aliyedai utume. Wafuasi wake walifikia 100,000 dhidi ya jeshi la Waislam kiasi cha 10,000; Waislam walishinda vita hivyo.

 

Maswali na maoni yanakaribishwa.

 

JazakAllah.

Mar 13, 2017

SAYYIDINA ABUBAKR SIDDIQ - PT 1 [Kiswahili]

Assalaamu alaikum,

 

Natumai hamjambo. Mfungo tulionao ni wa TISA (JAMADI-UL-AKHAR), ambamo katika tarehe 22, Khalifa wa kwanza wa Kiislam, Sayyidina AbuBakr Siddiq RadwiyAllahu Anhu aliiaga dunia hii. Ifuatayo ni risala fupi kuhusu baadhi ya fadhila zake.

 

 

Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad , aya hapo juu ya 40 kutoka Sura Tawba inayoelezea fadhila mmojawapo ya Khalifa wa 1 wa Kiislam, Sayyidina AbuBakr Siddiq na ndiye tutakaemzungumzia kwani tarehe 22 ya mfungo huu 9 aliiaga dunia.

TAFSIRI: Wakati wawili (Mtume na Sy AbuBakr) walipokuwa ndani ya pango, mmoja alimuambia mwenzake usihuzunike, hakika Allah yuko pamoja nasi.

 

Jina lake hasa ni Abdullah, ila AbuBakr likawa maarufu na Siddiq alipewa na Mtume kwa kusadikisha msafara wa Miiraj. AbuBakr kamwe hakuabudu masanamu hata kabla ya kusilimu wala hakuwahi kunywa pombe kipindi bado haijaharamishwa; na alisema hawezi kutumwa kinywaji kinachoua akili ya binadamu. Baada ya kuwa na uwezo kutembea, baba yake (Abu Quhafa) alimpeleka mbele ya sanamu na kumuambia kuwa huyu (sanamu) ndiye mungu wetu anaetulisha, visha na kutupa kila kitu. Sy AbuBakr akasimama mbele ya sanamu na kusema: mimi nina njaa nilishe, nina kiuu ninyweshe, sina nguo nivishe. Alipoona kimya, alichukua jiwe na kulipiga sanamu na ikaanguka. Baba yake alikasirika sana na kumpiga kibao kisha kumburuza hadi nyumbani na akamwambia mkewe : hebu mfundishe mwanao, leo kampiga mungu wetu, hana adabu huyo. Mkewe alimjibu: ewe Abu Quhafa, naomba usimwambie chochote huyu mwanetu, kwani nilipomzaa nilisikia sauti ikisema: umebarikiwa mtoto atakaekuwa rafiki wa karibu wa Muhammad , Mtume wa mwisho. Mimi simjui huyu Muhammad ni nani.

 

Kisa cha kusilimu kwake; Sy AbuBakr alikuwa katika safari zake za biashara nchini Shaam (Syria), ambapo padiri mmoja aliziona alama fulani zilizotajwa kwenye vitabu vya kikristo kuhusu Sy AbuBakr. Padiri alimuambia arudi Makkah haraka kwani rafiki yake wa karibu, Mtume , atakapotangaza Utume, yeye awe karibu nae. Sy AbuBakr alipofika kwa Mtume , alimwambia kuwa anamuamini sana ila anahitaji aonyeshwe muujiza mmoja tu ili roho yake itulie. Mtume alimuambia kuwa anahitaji muujiza gani zaidi ya kuambiwa na padiri huko nchi ya Shaam kuhusu kutangaza kwangu Utume. Papo kwa hapo Sy AbuBakr alisilimu. Hivyo alikuwa wa mwanzo kusilimu.

 

Sy AbuBakr alijitolea mali yake yote kwa ajili ya Mtume na Uislam. Baada ya kusilimu tu, Sy AbuBakr alimletea Mtume dinar 40,000 kwa matumizi atakavyo Mtume mwenyewe. Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam alisema kuwa Uislamu umepata faida sana kupitia mali ya Sy AbuBakr kuliko mali ya Sahaba yeyote.

 

Sy Abubakr hakuabudu sanamu wala kunywa pombe, kabla ya kusilimu, na katika enzi ambazo ilikuwa haiajaharamishwa na kusema kuwa pombe inaua akili ya binadamu kwa hiyo sikuona sababu kuitumia ambapo inanipa hasara tu!

 

Sy Abubakr alikuwa karibu sana na Mtume kila mara. Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam amesema kuwa kila aliyempa wito wa Uislamu, kwanza alikataa isipokuwa Sy Abubakr aliyekubali mara moja.

 

Sy Abubakr ndiye aliyemkomboa Bilal bin Rabah kwa pesa nyingi mno pale alipoteswa kwa sababu ya kusilimu.

 

Maswali na maoni yanakaribishwa.

 

JazakAllah.

 

Visitor's Traces

Total Page views