Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo.
Maarifa au ujuzi katika sharia za Kiislam inaitwa FIQ-HI, na ifuatayo ni risala fupi kuhusiana na fadhila zake.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, aya hapo juu ya Sura An Nisaa 4: 59 inayozungumzia uhakika wa fiq-hi au maarifa ya sheria za Kiislamu kwani wengi wa ndugu zetu hawana elimu nayo.
Uthibitisho wa fiq-hi ndani ya Quran; TAFSIRI: Enyi mlioamini mtiini Allah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allah na Mtume, ikiwa mnamuani Allah na siku ya mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.
Kwanza kabisa ieleweke kuwa kuna njia 4 za kufuatwa katika kutatua masuala ya dini, nazo ni : Quran, Hadithi, umoja wa Ummah na kukisia.
Nini maana ya FIQ-HI? Fiq-hi ni falsafa ya sharia za Kiislamu na inaelezea sharia za dini kupitia Quran na Sunnah (Hadithi). Mfano wake ni kama khalifa au mfalme atoe hukumu kwa kuzingatia sheria ya dini, na khalifa au mfalme huyo akitenda kinyume na sheria, basi huyo hatafuatwa. Mfano: Sy AbuBakr alipokuwa khalifa, aliwauliza Masahaba: enyi watu, mimi ninapofuata amri ya Allah na Mtume wake ni sawa, je ikiwa nikienda kinyuma mtafanyaje? Sahaba mmoja masikini alisema: tunaapa kwa Mola aliyetuumba, tutakunyoosha kama mkuki. Ndipo Sy AbuBakr aliwaambia : nyinyi ni waelewa.
Pia tuna maimamu wanne au madhehebu nne za kufuata sharia za Kiislamu nazo ni Imam Abu Hanifa, Imam Shafi’I, Imam Ahmad bin Hambal na Imam Malik Rahimahumullah.
Nini maana ya umoja wa ummah? Mfano Qadhi atatoa hukumu kutokana na kauli za Masahaba.
Nini maana ya kukisia? Ni kauli au hukumu za Masahaba, Tabii na Maimamu wanne. Yule asiyewakubali hao basi mfano wake ni kama mwenye kuumwa na tumbo kisha akadai kuwa akienda kwa daktari basi ataingia gharama maabara na mengineyo. Ni bora tu anunue dawa ya tumbo dukani na atapona!! Na ndiyo maana watu kama hao ni wapotovu.
Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...