Ads 468x60px

Mar 18, 2014

Fadhila ya FIQ-HI (Maarifa ya sheria za Kiislam) PT 2 (Kiswahili)


Assalaamu alaikum, 
Natumai hamjambo. Tunaendelea na risala kuhusu FIQ-HI
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, aya hapo juu ya Sura An Nisaa 4: 59 inayozungumzia uhakika wa fiq-hi au maarifa ya sheria za Kiislamu kwani wengi wa ndugu zetu hawana elimu nayo.
Enyi mlioamini mtiini Allah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allah na Mtume, ikiwa mnamuani Allah na siku ya mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.
Kuwaamini maimamu wote wanne (Imam Abu Hanifa, Imam Shafi, Imam Malik na Imam Ahmad bin Hambal) na kumfuata mmojawapo ni jambo la lazima. Pia siyo kuwa baadhi ya masuala amfuate imam mmoja na baadhi amfuate imam mwingine. Mfano wa mwenye kufanya hivyo ni kama mgonjwa wa tumbo akatafuta tiba kwa madaktari wanne tofauti, hivyo hali atakayokuwa nayo mgonjwa huyo ndivyo atakuwa mwenye kuwafuata maimamu tofauti.
Ila kama kuna dharura ndipo anaweza kumfuata Imamu mwingine. Mfano: kwa Imam Shafi mtu akimgusa mwanamke basi udhu wake hubatilika, hivyo wakati wa kutufu Al Ka-aba wanamfuata Imam Abu Hanifa.
Masahaba walipokuwa na tatizo lolote basi walimwendea Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, lakini je baada ya yeye kuiaga dunia?
Kwa Sy AbuBakr, ikamfikia kesi moja na suluhisho yake haikupatikana ndani ya Qurani wala Hadithi. Kisha aliwauliza Masahaba: je mnakumbuka kuwa kesi kama hiyo ilimfikia Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam na alijibu nini? Masahaba walijibu: ndiyo tunakumbuka na Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alijibu hivi. Sy AbuBakr akatoa hukumu juu ya suala hilo kisha alimtukuza Allah na kumshukuru kwa kusema kuwa wapo waja wako ambao hata na leo pia wanakumbuka kauli ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam.
Ukisiaji wa mjinga na wa mjuzi.
Swali linakuja, je Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam amezungumzia nini kuhusu hilo?
Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alimtuma Muaz bin Jabal kuwa Qadhi wa Yemen, ila kwanza alimuuliza kuwa atahukumu vipi kesi atakazoletewa? Muaz alijibu kuwa kwanza ataangalia ndani ya Quran, kisha Hadithi. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alimuuliza kuwa je kama hukufanikiwa kupata jibu ndani ya Quran na Hadithi, hapo utafanyaje? Muaz alijibu kuwa katika hali hiyo atakisia akizingatia mafundisho ya Quran na Hadithi. Ndipo Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alimshukuru Allah kuwa watu wa aina hiyo wapo katika umma wake.
Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views