Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo. Tunaendelea na risala kuhusu FIQ-HI
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, aya hapo juu ya Sura An Nisaa 4: 59 inayozungumzia uhakika wa fiq-hi au maarifa ya sheria za Kiislamu kwani wengi wa ndugu zetu hawana elimu nayo.
Enyi mlioamini mtiini Allah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allah na Mtume, ikiwa mnamuani Allah na siku ya mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.
Tuangalie ukisiaji wa mjinga na mjuzi: Bwana 1 alipanda juu ya mti lakini alishindwa kushuka huku watu wakimsubiri chini. Mara akapita mpita njia na alipoona hivo aliwashauri wamrushie kamba kisha yule bwana aiufunge kiunoni ndipo waliopo chini wamvute, kwa hali hiyo atashuka kirahisi tu. Walipomvuta, yule bwana akaanguka na kufa papo hapo.Ndugu zake walianza kumhoji yule mpita njia, ambae alijitetea kuwa eti ni juzi tu alimtoa mtu 1 kutoka kisimani kwa staili hiyo na alinusurika!! Hivi ndivyo wajinga wanavyokisia.
Tuangalie ukusiaji wa wajuzi: kwa Imam Abu Hanifa alikuja bwana 1 na kumuambia: nimetenda kosa 1, nimewajibika kuoga ila katika kugombana na mke wangu kuwa ikiwa nitaoga basi mke wangu awe na talaka 3!! Sasa wanaosema tufuate Qurani na Hadithi tu, walete aya au Hadithi inayotoa hukumu ya kesi kama hiyo!! HAKUNA. Imam Abu Hanifa kamwambia afuatane nae na walipofika kando ya mto, Imam alimsukuma hadi yule bwana katumbukia kwenye mto. Alitoka kwa shida, ila mke wake alisalimika na talaka kwani kwa kutumbikia kwenye maji ina maana alijiogea bila ya kutarajia.
Majambazi 4 walipora mali kisha wakwamwambia kuwa kama yeye atawashitaki kuwa fulani na fulani ni mwizi, basi mkewe atakuwa na talaka 3. Kwa hali hiyo aliyeporwa hakuwa na jinsi ila kunyamaza tu huku majambazi walitamba mitaani bila kushitakiwa. Baada ya masiku aliambiwa amwone Imam Abu Hanifa. Akamwelezea tatizo lake, Imam akamwambia awaalike majambazi wote, pia wakaandaliwa wababe kama 5. Wababe walisimama mlangoni baada ya karamu na kila jambazi akitoka yule aliyeibiwa aliulizwa: je huyu ndiye jambazi? Akitoka jambazi asiyehusika na tukio la kumpora, yule bwana alijibu : siye; ila kwa wale wane aliambiwa akae kimya na wale wababe wataelewa na kuwakamata. Kwa hali hiyo majambazi wote 4 walikamatwa, mali yake ikapatikana na mkewe kusalimika na talaka 3.
Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Kind Regards,
Muhammad KHATRI
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...