Ads 468x60px

Apr 23, 2013

Fadhila za Elimu - PT 5 (Mwisho) (Kiswahili)


Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo. Mada hii ni ndefu ila nimeona bora nihitimishe kwani bado nina mada nyingine nyeti na muhimu za kutuma. Pia huu ni Mfungo wa 9 (Jamadi-ul-akhar) na mwezi 22 ya Mfungo huu, Khalifa wa kwanza wa Kiislamu, Sayyidina AbuBakr Siddiq RadwiyAllahu Anhu, aliiaga dunia hii. Insha Allah baada ya mada hii nitaanza kutuma historia yake kwa ufupi. Ila nitafurahi sana ikiwa mtaniandikia maoni yenu ya moyoni kabisa na hasa zenye kukosoa kuliko za kunisifu. Mimi sistahili sifa yoyote ndugu zanguni ila najitahidi kwa kipaji nilichojaaliwa.
AYA: INNAMA YAKHSHALLAHA MIN IBAADIHIL ULAMAA.
Tafsiri ya aya:
Hakika wamchao au wenye kumuogopa Allah zaidi katika viumbe vyake ni wanazuoni tu. 
Kuna hatari moja ya baadhi ya watu kututishia kwa daraja za Hadithi. Wanaposema Hadithi Fulani ni “DHAIFU” wanakuwa na maana ya kutoitilia maanani!!!
Kwanza kabisa naomba tu ieleweke kuwa Hadithi maana yake ni kauli ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, ambayo daima haiwezi kuwa na kasoro. Allah Anatuhakikishia jambo hilo ndani ya Quran Tukufu : WAMA YANTIQU ANIL HAWAA. IN HUWA ILLA WAHYUN YUHAA. (SURA AN-NAJM; AYA 3-4)
(Tafsiri):  (Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam) wala hatamki kwa matamanio. Hayakuwa haya ila ni ufunuo uliofunuliwa.
Pia zingatia kitendo cha mmoja wa wanazuoni wakubwa wa enzi hizo, Allaama Ibn-ul Haaj. Alisoma Hadithi hii : Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam amesema kuwa mwenye kukata kucha siku ya jumatano basi atapatwa na ugonjwa wa mtango au mba (kama nimepatia majina, ila ni ugonjwa wa mtu kutokwa na alama nyeupe mwilini). Mwishoni mwa Hadithi iliandikwa “hii ni Hadithi dhaifu”. Mwanazuoni huyo alikata kucha siku ya jumatano baada ya kusoma kuwa Hadithi ni dhaifu. Baada ya masiku akaanza kutokwa na alama nyeupe na kuenea mwili mzima. Ndipo aligundua kuwa bila shaka ni kutokana na kutenda kwake juu Hadithi hiyo. Usiku mmoja alimuota Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, aliyemuuliza “Ibn-ul Haaj imekuwaje?” Akajibu kwa unyonge mkubwa “nimetenda juu ya Hadithi hiyo kwa kufikiria ni dhaifu”. Ndipo Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alimuuliza “je kauli yangu haikukufikia?” Alijibu tena kwa unyonge “ilinifikia”. Kisha Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alipapasa mkono wake mtukufu kwenye mwili wa mwanazuoni huo na akapona.
Cha kuzingatia: Hadithi zina daraja; kuna SAHIHI, HASAN, DHAIFU, n.k. Wanazuoni waliokusanya kauli za Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam kama kina Imam Bukhari, walijitolea maisha yao yote katika kazi hiyo huku wakizingatia mwenendo pamoja na tabia za waliopokea riwaya za Hadithi. Ikiwa mmojawapo katika waliopokea riwaya hafahamiki vizuri kitabia au masuala mengine muhimu ya kuzingatia, ndipo Hadithi husika hupewa daraja ya DHAIFU. ILA kauli ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam itabaki pale pale.
 Vile vile wapo “waislamu” wenye kumkashifu Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, wanachapisha vitabu vya Hadithi huku wakiziondoa kabisa Hadithi zinazowaletea dosari katika misheni yao!!!
Jamani kweli watu kama hawa tutawaita Waislamu????
 Allah atuhifadhi na fitina na ufisadi katika dini, amin.
 Ndugu zanguni msisite kutoa maoni yenu, toa ulichonacho moyoni kumnufaisha Muislamu mwenzako!
 JazakAllah,

 Kind Regards,
Muhammad KHATRI 

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views