Ads 468x60px

Dec 28, 2013

Mzinduzi Wa Dini - Imam Ahmad Ridaa (Part 1)‏ (Kiswahili)

Assalaamu alaikum,

Natumai hamjambo. Ifuatayo ni sehemu ya kwanza ya risala fupi kuhusu mzinduzi wa Dini.

Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, aya hapo juu ya 8 kutoka Sura Al Bayyinah (98), inayozungumzia malipo ya wamchao Allah.
TAFISIRI: Malipo yao kwa Mola wao Mlezi ni Bustani za daima, zipitazo mito kati yake, watakaa humo milele. Allah yu radhi nao, na wao waradhi naye, hayo ni kwa anaemuogopa Mola wake Mlezi.
 Tuelewe kuwa mlango wa Utume umeshafungwa na Mtume wa mwisho kuja ni Mtume wetu Swallallahu Alaihi Wasallam. Hakuna Mtume atakaekuja tena, ila Mtume Isa atakuja kabla ya Qiyama, lakini atakuja kama umma wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam.
 HADITHI: Imepokewa riwaya na Abu Huraira RadwiyAllahu Anhu, amesema Mtume Swallallahu alaihi Wasallam kuwa Hakika Allah atamtuma mwanzoni mwa kila karne mtu kwa ajili ya umma huu atakaefufua na kurejesha dini yao. (Ameinukuu Abu Daud).
 Wafasiri na wanazuoni wanaelezea katika ufafanuzi wa Hadithi hapo juu kuwa inapofika kipindi/ muda/ nyakati ambapo uhaba/ upungufu wa maarifa/ ujuzi unaonekana au uzorotaji katika kufuata sunnah; kukithiri kwa uvumbuzi potofu na ujinga; ndipo Allah humleta mja wake aidha mwanzoni au mwishoni mwa kila karne atakaetofautisha Sunnah na uvumbuzi. Atazikanusha na kuziweka wazi uvumbuzi huo na hatamuogopa yeyote zaidi ya Allah katika hilo. Mtu huyo anajulikana kama mjadidi/ mzinduzi wa dini.

KWA NINI MJADIDI/ MZINDUZI HULETWA BAADA YA MIAKA 100?
Mjadidi/ mzinduzi huletwa baada ya miaka 100 kwa sababu baada ya kila karne (miaka 100) mazingira na namna ya ufikiriaji za binadamu huingia katika hatua ya mabidiliko makubwa. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam usiku mmoja alisimama na kuwauliza Masahaba: je nisiwafahamishe umuhimu wa usiku huu?  Kuanzia usiku huu hadi kufikia miaka 100, kila aliye hai (leo) ardhini basi hatakuwa hai tena (baada ya miaka 100).
Hivyo dhana kuu inayopatikana kwa mzinduzi ni kuwa ana sifa moja au zaidi ya kipekee inayoinufaisha umma wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam katika masuala ya dini, mfano: taaluma ya dini, mawaidha, mahubiri, kuwafahamisha na kuwakataza watu juu ya maovu na kuwasaidia walio sahihi.
 Baadhi ya wazinduzi wa dini wa karne zilizopita ni Umar ibn Abdul Aziz, Imam Abu Hanifa Nooman bin Thabit, Imam Muhammad bin Idris Shafi, Imam Hasan Basri, Imam Malik bin Anas, Imam Ahmad bin Hambal, Imam Bayhaqi, Sheikh AbdulQadir Jilani, Imam Ghazali, Sheikh Ahmad Kabir Rifaee, Ibn Hajar Al Asqalani, Imam Jalaluddin Suyuti, Abdallah Al Haddad na Imam Ahmad Ridaa Rahimahullahu.

Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI 

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views