Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo. Ifuatayo ni sehemu ya mwisho ya risala fupi kuhusu mzinduzi wa Dini.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, aya hapo juu ya 8 kutoka Sura Al Bayyinah (98), inayozungumzia malipo ya wamchao Allah.
TAFISIRI: Malipo yao kwa Mola wao Mlezi ni Bustani za daima, zipitazo mito kati yake, watakaa humo milele. Allah yu radhi nao, na wao waradhi naye, hayo ni kwa anaemuogopa Mola wake Mlezi.
Imam Ahmad Ridaa – mzinduzi wa karne ya 14 ya Kiislam.
Alizaliwa mwezi 10 Shawwaal (Mfungo Mosi) 1272h.
Alikamilisha kusoma Quran (Msahafu) akiwa na umri wa miaka 4 tu; kwa kawaida watoto wa miaka 4 au hata 5 ndiyo kwanza huanza kusoma herufi za Quran.
Alihitimisha taaluma katika fani zote za dini katika umri wa miaka 13 na miezi 10 tu na alianza kuandika fatwa ya kwanza. Baada ya hapo baba yake alimkabidhi kazi ya kuandika fatwa, ila baba yake ndiye alikuwa akizisadikisha na kuweka sahihi . Baada ya miaka kama 10 hivi, ndipo baba yake alimkabidhi rasmi mwanae kazi hiyo.
Katika umri wa miaka 22, alifunga safari ya kwanza ya hijja pamoja na baba yake na huko alikutana na wanazuoni maarufu kina Sayyid Ahmad Zayni Dahlan na Mufti Abdullah bin AbdulRahman Siraaj. Hata siku 1, Imam wa Msikiti wa Makkah alimuambia Imam ahmad Ridaa : Naapa kwa Jina la Mola, naona Nuru ya Allah usoni mwako.
Baada ya miaka 28, alifunga safari ya pili ya hijja, akifuatana na kaka yake na mwanae. Aliulizwa na Shariff wa Makkah kuhusu elimu ya uficho (ilm-ul-ghaib) ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, na hivyo alitunga kitabu katika lugha ya Kiarabu “Al Dawlah Al Makkiyah”, ambacho kilikubalika kwa kiasi kikubwa sana kiliposomwa mbele ya wanazuoni waliokuwepo kipindi hicho. Licha ya kitabu hicho, Imam Ahmad Ridaa alitunga vitabu kama “Hussamul Haramain” (panga la Misikiti miwili Takatifu juu ya koo la wasioamini na waongo). Kitabu hiki kinazungumzia imani na itikadi potovu ya “waislam” wanaomkashifu Allah na Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam. Pia ni mtunzi wa vitabu zaidi ya 1,000.
Alifariki mwezi 25 Safar (Mfungo 5), 1340h. Mcha Mungu mmoja nchini Syria aliota kikao cha Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam ambamo aliulizwa ni nani anaesubiriwa. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam akajibu kuwa ni kipenzi chake aitwae Ahmad Ridaa. Asubuhi yake baada ya kuuliza, Mcha Mungu huyo alifunga safari ya kwenda India kuonana na Ahmad Ridaa, na alipofika katika kitongoji cha Barelvi, aliambiwa kuwa amefariki siku chache tu zilizopita, na alipokumbuka ndoto yake, kumbe ni kweli ilikuwa siku ile ile.
Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...