Assalaamu
alaikum,
Natumai
hamjambo. Kuanzia leo nitakuwa natuma risala fupi kuhusu msafara wa isra na
Mi-‘iraj ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, ambao ulitokea mwezi 27 Rajab.
SUB-HANALLADHI
ASRA BI-ABDIHI LAYLAN MINAL MASJIDIL HARAAMI ILAL MASJIDIL AQSA, ALLADHI
BAARAKNA HAWLAHU LINURIYAHU MIN AYATINA, INNAHU HUWAS SAMIUL BASIR. (SURA BANI
ISRAIL, AYA 1)
Baada
ya Kumshukuru Allah na kumtakia Rehma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi
Wasallam, aya hapo juu ni ya kwanza ya Sura Bani Israil, ambayo inazungumzia
msafara wa miraji.
Ieleweke
kuwa kila Mtume aliyeletwa hapa duniani alipewa muujiza au miujiza.
Lakini
Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam aliletwa kama muujiza licha ya
kupewa miujiza mingi, mmojawapo ukiwa huu msafara wa miraji.
Tafsiri
ya aya:
Utukufu
ni Wake Yeye Aliyempeleka Mja Wake katika sehemu tu ya usiku kutoka Msikiti wa
Haraam (Makkah) hadi Msikiti wa Aqsa (Palestina), ambao umezungukwa na Baraka
Zetu, ili Tumuonyeshe baadhi ya alama zetu. Hakika Allah ndiye Mwenye Kusikia
Mwenye Kuona.
Tukiichunguza
aya peke yake tu ina nukta nyingi za kuzingatia.
- Kwanza kabisa, Allah Ametaja Utukufu Wake kwa kuanza aya. Hii ni kuukata kata kabisa utata uliotokea na utakaotokea kwani mwenye kuleta utata katika msafara huu, basi moja kwa moja analeta mashaka katika uwezo wa Sub-hana!
- Baadhi ya watu wanadai kuwa eti Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alioteshwa tu kwenda mbinguni na si kuwa alienda (yaani eti mwili wake haukuenda)!!! Sehemu ya pili ya aya inafafanua : “ALIYEMPELEKA MJA WAKE”. Sehemu ya aya haisemi kuwa “alimuotesha”! Hivyo mwenye kupinga msafara huo wa kiwiliwili na roho basi atatoka katika Uislamu.
- Msafara huu ulifanyika katika
sehemu fupi mno ya usiku. Riwaya moja inaelezea ufupi wa msafara kuwa maji
aliyotawadhia Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam yalikuwa bado yanasambaa
ardhini wakati Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam aliporejea. Riwaya nyingine inasema
kuwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alipofungua mlango kutoka chumbani
mwake, ile komeo (cheni) bado ilikuwa ikicheza aliporejea! Kwa ufupi hatuwezi
kupata picha ya ufupi wa msafara huo na ndiyo maana ikatajwa kuwa ni muujiza.
- Vile vile ni sababu ya msafara kuwa usiku tu? Sababu kuwa iliyotajwa kuwa ili watu wasipate kuona. Imani ni kuamini kisichoonekana, hivyo lau kama msafara ungetokea mchana basi wengi wangemuona Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam akienda na hivyo kupima imani ingekuwa ngumu.
Kwa
nini sehemu ya kwanza ya msafara ulikuwa kutoka Makkah hadi Palestina? Hii ni
kwa sababu Waarabu walikuwa na misafara ya mara kwa mara baina ya sehemu hizo.
Hivyo kuwafahamisha kuwa msafara huu wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam baina
ya sehemu hizo katika muda mfupi ili wawe na picha ya sehemu wanazoambiwa.
Maoni
/ maswali yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad
KHATRI
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...