Ads 468x60px

May 2, 2013

Sayyidina Abu Bakr Siddiq - PT 2‏ (Kiswahili)

Assalaamu alaikum,
 Natumai hamjambo. Kwa kuwakumbusha tu, kesho Ijumaa ni mwezi 22 ya Mfungo 9 (Jamadi ul Akhar) na ndiyo tarehe ambamo Sayyidina Abubakr Siddiq RadwiyAllahu Anhu aliiaga dunia hii. Itakuwa bora kama kila mmoja wetu akaleta Ikhlas 3 kisha akaomba dua kumtawassul Abubakr Siddiq kwani ana hisani nyingi juu Uislamu na Waislamu.
 Kisa cha kusilimu kwake; Sy AbuBakr alikuwa katika safari zake za biashara nchini Shaam (Syria), ambapo padiri mmoja aliziona alama fulani zilizotajwa kwenye vitabu vya kikristo kuhusu Sy AbuBakr. Padiri alimuambia arudi Makkah haraka kwani rafiki yake wa karibu, Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, atakapotangaza Utume, yeye awe karibu nae. Sy AbuBakr alipofika kwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, alimwambia kuwa anamuamini sana ila anahitaji aonyeshwe muujiza mmoja tu ili roho yake itulie. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alimuambia kuwa anahitaji muujiza gani zaidi ya kuambiwa na padiri huko nchi ya Shaam kuhusu kutangaza kwangu Utume. Papo kwa hapo Sy AbuBakr alisilimu. Hivyo alikuwa wa mwanzo kusilimu.
Baada ya kusilimu kwake. Sy AbuBakr alijitolea mali yake yote kwa ajili ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam na Uislam. Baada ya kusilimu tu, Sy AbuBakr alimletea Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam dinar 40,000 kwa matumizi atakavyo Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam mwenyewe. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alisema kuwa Uislamu umepata faida sana kupitia mali ya Sy AbuBakr kuliko mali ya Sahaba yeyote. 
Maswali / maoni yanakaribishwa.

JazakAllah,
Kind Regards,
 Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views