Natumai hamjambo.
Mwezi tulionao ni wa Rajab, ambayo ina fadhila tele. Ifuatayo ni sehemu ya kwanza risala ya Rajab.
AYA: INNA ADDATASH SHUHURI INDALLAHITHNA ASHARA SHAHRAN FI KITABILLAHI YAUMA KHALAQAS SAMAWAATI WAL ARDHI MINHA ARBA-ATUN HURUM, DHAALIKAD DINUL QAYYIMU FALAA THUDHLIMUNA FIHINNA ANFUSIKUM.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, aya hapo juu ni ya 36 ya Sura Tawbah, inayozungumzia utukufu wa miezi minne. Mwezi Rajab, ambao ni mmojawapo kati ya miezi hiyo mine, mwezi ambao una fadhila tele. Ni mwezi ambamo dua hukubalika.
TAFSIRI: Bila shaka idadi ya miezi kwa Allah ni miezi kumi na mbili katika kitabu cha Allah tangu Alipoumba mbingu na ardhi, miongoni mwao minne ni yenye huruma (tukufu). Hii ni dini iliyonyooka na hivyo msidhulumu nafsi zenu katika miezi hizo.
DUA YA RAJAB: ALLAHUMMA BAARIK LANA FI RAJAB WA SHA’ABAAN WA BALLIGHNA ILAA SHAHRI RAMADHAN.
Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam amesema kuwa Rajab ni mwezi wa Allah, Shaaban ni wa kwangu na Ramadhani ni ya ummah wangu.
Ni mwezi wa heshima na hata zama za ujahili Waarabu waliuheshimu sana mwezi huu kwa kuacha mapigano na mauaji.
Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Kind Regards,
Muhammad KHATRI
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...