Ads 468x60px

Sep 18, 2013

MTUME IBRAHIM - PT 4‏ (KISWAHILI)


Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo.
Tunaendelea na risala juu ya maisha ya Mtume Ibrahim Alaihissalaam.
AYA:  QULNA YA NARUKUNI BARDAN WA SALAAMAN ALAA IBRAHIM.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, hapo juu ni aya ya 69 ya Sura Ambiya (21:69). Katika risala iliyopita tulisema kuwa Namrudi alishindwa katika mjadala na Mtume Ibrahim. Ni kawaida kuwa yule anaeshindwa kwenye mjadala, basi aidha hukubali haki au huanza matusi na vurugu kuashiria kutopendezewa kwake kushindwa. Namrud aliposhindwa, alisema kuwa Ibrahim amekaidi katika dini ya mababu zake na hivyo aadhibiwe. Hivyo iliamuliwa aingizwe kwenye moto.
Ikachimbwa shimo kubwa na kazi ya ukusanyaji wa kuni ulianza mara moja. Miguu na mikono ya Mtume Ibrahim ilifungwa na kisha moto ukawashwa. Moto ulikuwa mkubwa mno na inasemekana mfano wake haijawahi kupatikana. Walishindwa kuelewa jinsi ya kumtumbukiza motoni Mtume Ibrahim, lakini alitokea mtu mmoja na ushauri wa kumkalisha kwenye kiti mfano wa manati na kurushwa hadi Mtume Ibrahim kufika motoni.
Mtume Ibrahim alipokaribia kuingizwa motoni, Jibrail alimjia na kumuuliza kama ana haja yoyote? Mtume Ibrahim alimjibu kuwa haja yake ni kwa Mola wake tu. Pia Malaika wa kunyesha mvua alikaa tayari kusubiri hukumu ya Allah ya kunyesha mvua kubwa kuuzima moto.
Pindi Mtume Ibrahim alipoingizwa kwenye moto, Allah aliihukumu moto: “Tuliiambia moto, ewe moto kuwa baridi ya usalama kwa Ibrahim”.  Kamba alizofungwa nazo Mtume Ibrahim ziliungua zote lakini hata nywele 1 pia ya Mtume Ibrahim haikuungua.  Mtume Ibrahim alikaa kwenye moto huo kwa miaka 40 na muda wote huo Jibrail alimpungia upepo huku Mtume Ibrahim alitokwa na jasho tu.

Maswali / maoni yanakaribishwa
JazakAllah,
Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views