Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo. Ijumaa Kareem
Tunaendelea na risala juu ya maisha ya Mtume Ibrahim Alaihissalaam.
AYA: WA-IDH YARFA-U IBRAHIMUL QAWAA-IDA MINAL BAYTI WA ISMAIL, RABBANA TAQABBAL MINNA INNAKA ANTAS SAMI-UL ALIM.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, hapo juu ni aya ya 127 ya Sura Al Baqarah, inayozungumzia ukarabati wa Al Kaaba.
TAFSIRI: Wakati Ibrahim alipokuwa akipandisha kuta za Al Kaaba pamoja na Ismail, (wakati huo waliomba) Ewe Mola ikubali kazi yetu hii, bila shaka wewe ndiye Mwenye kusikia na Mwenye ujuzi.
Baada ya tufani ya zama za Mtume Nuh Alaihissalaam, wa kwanza kuukarabati Al Kaaba na kutufu alikuwa Mtume Ibrahim. Mwanae Mtume Ismail alikuwa na kazi ya kuleta mawe kutoka mlima Abu Qubais ulio pembeni mwa Msikiti Mtukufu, na Mtume Ibrahim alizifyatulia matofali na kujenga. Ukuta ulipoinuka urefu wa kifua, bila shaka kunatakiwa meza au ngazi ya kusimamia ili upambane na urefu.
Mtume Ibrahim alisimama juu ya jiwe moja kukabiliana na urefu. Kadri ukuta ulivyoinuka vivyo hivyo kwa muujiza wa Allah, jiwe nalo hurefuka. Ukarabati ilipokamilika, alama za miguu mitikufu ya Mtume Ibrahim yakabaki kwenye jiwe hilo, na Qurani imesimulia habari zake kuwa ni Maqamu Ibrahim.
Ni muujiza wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam kuwa kila alipokanyaga mawe basi ilitokea alama ya Mguu wake Mtukufu, lakini alipokanyaga kwenye mchanga hapakutokea alama.
Mtume Ibrahim akafikiria kuwa ukarabati wa Al Kaaba imekamilika ila mtu akitaka kutufu aanze wapi?? Alimwambia Mtume Ismail akalete jiwe moja kutoka mlima Abu Qubais ambao uwe wa aina pekee kuliko matofali ya Al Kaaba, ili aiweke pembeni na iashirie kutufu ianze hapo. Mtume Ismail alipofika mlimani hapo, alisikia sauti : Ewe Ismail chukua jiwe hii iliyoletwa na Mtume Adam kutoka Peponi; inaitwa Hajra-il Aswad. Kuna fadhila nyingi kuhusu jiwe hilo, lakini kubwa zaidi ni kuwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam ameibusu.
Ujenzi wa Al Kaaba ulipokamilika, Mtume Ibrahim alinadi: enyi mloamini, njooni kutufu Al Kaaba. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam amesema kuwa kila aliyejuwa kwenye tumbo la mama au kwenye mgongo wa mama, alitikia “LABBAYK”, na kila aliyetikia LABBAYK lazima atahiji na kwa idadi aliyotikia basi atahiji kwa idadi hiyo.
Allah Atujaalie sote tuitwe katika Jumba Lake Tukufu walau mara moja katika maisha, amin.
Maswali / maoni yanakaribishwa – ingawa kimya kimezidi mno ndugu zanguni!!!
JazakAllah,
Muhammad KHATRI
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...