Natumai hamjambo.
Tunaendelea na risala juu ya maisha ya Mtume Ibrahim Alaihissalaam.
AYA: WA-IDH YARFA-U IBRAHIMUL QAWAA-IDA MINAL BAYTI WA ISMAIL, RABBANA TAQABBAL MINNA INNAKA ANTAS SAMI-UL ALIM.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, hapo juu ni aya ya 127 ya Sura Al Baqarah, inayozungumzia ukarabati wa Al Kaaba.
TAFSIRI: Wakati Ibrahim alipokuwa akipandisha kuta za Al Kaaba pamoja na Ismail, (wakati huo waliomba) Ewe Mola ikubali kazi yetu hii, bila shaka wewe ndiye Mwenye kusikia na Mwenye ujuzi.
Mtume Adam alipoletwa aridhini; kwanza ieleweke kuwa kutamka kuwa eti Mtume Adam alikosea na kuwa alitolewa Peponi, ni kinyume na adabu. Quran inasema INNI JAA-ILUN FIL ARDHI KHALIFA (Mimi nitamuumba khalifa kwa ajili ya ardhi). Hata kama Mtume Adam asingekula tunda alokatazwa, angeletwa tu ardhini. Mtume Adam alipoletwa ardhini, sauti ya Malaika ya dhikri ya Allah ilikosekana na kwa hali hiyo alikosa raha moyoni. Ndipo Allah alimuamrisha kujenga Nyumba Yake Tukufu. Hivyo Mtume Adam ndiye wakwanza kujenga Al Kaaba.
Tufani na mafuriko yaliyotokea zama za Mtume Nuh, yalileta maafa makubwa duniani, na walionusurika na Mtume Nuh na wafuasi wake wachache tu. Al Kaaba nayo iliathirika na kuna riwaya inasema iliinuliwa mbinguni. Mahala pa Al Kaaba ilibaki muinuko mdogo kuashiria kuwepo kwa jengo siku za nyuma.
Maswali / maoni yanakaribishwa
JazakAllah,
Muhammad KHATRI
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...