Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo na mmejitahidi kufanya ibada usiku wa Laylatul Qadri. Mwezi mtukufu ndyo huo unatuaga, ila kuna baadhi mambo muhimu sana ya kuzingatia.
MMojawapo ni zakatul Fitri. Faida na utekelezaji wake ni hivi:-
1) Hiyo ni wajib, isipotekelezwa basi swaum ya mja hunin’ginia baina ya mbingu na ardhi
2) Muda uliotajwa kuwa ni mbora katika kuitekeleza ni baada ya mwezi kuandama hadi kabla ya Sala ya Idi. Hata hivyo, inaweza ikatekelezwa siku yoyote hata leo au siku 1 au wiki au hata mwezi baada ya Ramadhan; ila si vizuri kuahirisha kiasi hicho.
3) Katika utekelezaji wake, kilo 2 na gram kama 100 ya aidha unga wa ngano au mchele au chakula kinacholika mwezi wa Ramadhani kwa mji ule.
4) Ni jukumu la kila Muislamu mwenyewe,mke wake, watoto na hata mfanyakazi wa nyumbani kama ni Musialmu.
5) Wanaostahili kupewa ni Waislamu wasiojiweza akiwemo mfanyakazi wa nyumbani kama ni Muislamu.
6) Zakatul Fitri anaweza kupewa mtu mmoja au watu tofauti.
Matayarisho kwa ajili ya Sala ya Idi:-
1) Ni Sunnah kula tende katika idadi ya witri, mfano 1 au 3, kabla ya kuenda kusali.
2) Ni Sunnah kusoma Takbir wakati wa kuelekea kusali.
3) Ni Sunnah kwenda kwa kutumia njia moja na kurudi kupitia njia nyingine
4) Ni Sunnah kuvaa nguo mpya au nzuri na safi.
Maoni / maswali yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...