Ads 468x60px

Aug 26, 2013

VITA VYA UHUD (KISWAHILI)


Assalaamu alaikum,
 Natumai hamjambo. Kama nilivyoahidi, ifuatayo ni kisa cha vita kwa muhutasari kabisa.
 VITA VYA UHUD (VITA VYA PILI VYA KIISLAM)
 AYA: WALAA TAQULU LIMAN YUQTALU FI SABILILLAHI AMWAATUM BAL AHYAA-UN WALAA KIN LAA TASH-URUN. (SURA: AL BAQARAH – 154).
 AYA: WALAA TAHSABANNALLADHINA QUTILU FI SABILILLAHI AMWAATUM BAL AHYAA-UN INDA RABBIHIM YURZAQUN. (SURA: AALI IMRAN – 169).
 Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam, aya 2 hapo zinaelezea fadhila za kuuawa shahidi katika kupigania dini ya Allah.
 Tafsiri: Wala msiwaambie waliouawa katika njia ya Allah kuwa ni wafu, bali wako hai lakini nyinyi hamtambui. (2:154)
Tafsiri: Wala usiwadhanie kabisa waliouawa katika njia ya Allah kuwa ni wafu, bali wako hai, wanaruzukiwa kutoka kwa Mola wao Mlezo. (3:169)
 Baada ya makafiri wa Makkah kupigwa vibaya sana katika vita vya Badri na kudhalilika, walikuwa na chuki ya kulipiza kisasi kwa Waislam. Hivyo waliandaa jeshi lao kutaka kupigana na Waislam. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alipopata taarifa hizo, aliwatangazia Waislam na kuandaa jeshi.
 Vita hivyo vilitokea nje kidogo tu ya mji mtukufu wa Madina na kando kabisa na milima ya Uhud. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam aliiamrisha kundi la Masahaba kama 50 hivi kulinda sehemu moja ya uwanja ambapo palikuwa na njia ya kuingilia uwanjani hapo na akawasisitiza wasitoke hapo hata kama ndege wanatafuna miili ya waliouawa.
 Katika vita hivyo, Amii wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, Sayyidina Hamza RadwiyAllahu Anhu aliuawa kikatili na hadi mke wa Abu Sufyan, Hinda, alitafuna moyo wa Sayyidina Hamza! Waislam waliokuwa wapatao kama 700 hivi, walishinda na walipoanza kukusanya ngawira, miongoni mwa Masahab 50 wakasema kuwa kwa kuwa tumeshinda hivyo tuungane na wenzetu la sivyo tutakosa ngawira. Baadhi yao wakasema kwa kuwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam aliwakataza wasitoke hapo hadi waamrishwe tena, walikataa kuacha sehemu zao. Kwa kuwa wengi kati ya hao 50 kuondoka mahala hapo na kuungana na wenzao katika ukusanyaji wa ngawira, makafiri walipata taarifa hizo na hivyo kuwazunguka Waislam na kuingilia sehemu ambayo Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam aliwaagiza Masahaba 50 kubakia hapo. Tukio hilo limerekodiwa ndani ya Quran hivi:
 AYA: Na Allah Alikutimizieni miadi Yake, vile mlivyokuwa mnawaua kwa idhini yake, hadi mlipolegea na mkazozana juu ya amri, na mkaasi baada ya Yeye kukuonyesheni mliyoyapenda. Wapo miongoni mwenu wanaotaka dunia na wapo miongoni mwenu wanaotaka akhera. Kisha akakutengeni nao (maadui) ili akujaribuni. Nae sasa Ameshawasameheni. Na Allah ni Mwenye Fadhila juu ya waumini. (3:152)
 Vita ambavyo Waislamu walishashinda, wakajikuta wanavamiwa kwa mara ya pili na hivyo kupigwa. Hapo ndipo hata Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alipoteza meno zake 2 na alijeruhiwa pia. Makafiri walizua taarifa kuwa wamemuua Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam (astaghfirullah). Ndipo Masahaba shupavu kina Sayyidina Umar wasimama kuwahakikishia Waislam kuwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam yu hai na yuko salama. Katika vita hivyo, Waislam 70 waliuawa shahidi.

Maswali / maoni yanakaribishwa
JazakAllah,
Muhammad KHATRI 

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views