Ads 468x60px

Aug 13, 2013

SHAWWAAL-UL-MUKARRAM (MFUNGO MOSI)‏ (KISWAHILI)


Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo. Mwezi mtukufu wenye Baraka tele ndiyo imetutoka, Allah Atujaalie tuuone tena mwakani in sha Allah tukiwa na afya njema. Pia Allah Atukubalia ibada tulizojaribu kuzileta katika mwezi huo na Atusamehe dosari na mapungufu yaliyotokea, amin.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam, mwezi wa 10 katika kalenda ya Kiislam ni Shawwaal (au Mfungo Mosi). Huu ni mwezi ambamo mahujaji huanza matayarisho ya safari zao za hijja.
Baadhi ya tarehe muhimu katika mwezi huu:-
Tarehe 1 – Eid-ul-Fitr.
Tarehe 15 – Vita vya Uhud
Usiku wa kuamkia Eid-ul-Fitr, Allah huwauliza Malaika wake kuwa nini ujira ya mwenye kutenda kazi (kufunga swaum katika mwezi wa Ramadhani)? Malaika hujibu alipwe malipo yake kikamilifu, ndipo Allah huwaambia enyi Malaika kwa kuwa waja wangu wametekeleza amri yangu mwezi Ramadhani na wanaelekea kusali sala ya idi shuhudieni kuwa Nimewasamehe madhambi yao!! Sub-hanallah! Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam amesema kuwa mja hurudi nyumbani katika hali ya kuwa amesamehewa.
QASIDA BURDAH.
Nimeona ni vyema nianze kusimulia fadhila, faida na Baraka za Qasida hiyo ili sote tufaidike.
Mwanachuoni maarufu wa Misri, Imam Saalih Saharafuddin Busairi, aliuguliwa na ugonjwa wa mwili kupooza (paralysed). Madaktari maarufu walikata tamaa kuwa shekhe hawezi kupona tena! Ndipo alianza kutunga beti za kumsifia Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam. Baada ya kuimaliza, usiku mmoja alikaa chumbani kwake na kuisoma kwa unyenyekevu sana na mara usingizi ulimpata. Alimuota Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam na kumlilia kwa ugonjwa alioupata na kumsomea Qasida. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alifurahi mno na kupapasa mkono wake tukufu kwenye mwili wa shekhe na kisha akamfunika kilemba chake kitukufu. Shekhe alipoamka tu kwanza alijikuta kilemba kilekile kitukufu amejifunika na pia akajikuta amepona kabisa kana kwamba hakuuguliwa! Sub-hanallah!!
Wanazuoni wanasema, Qasida hiyo ikisomwa kwa nia njema na unyenyekevu basi Allah huleta kheri na baraka. 
In sha Allah Qasida yenyewe nitaianza kuanzia risala ijayo.

Maoni / maswali yanakaribishwa.
JazakAllah,
Kind Regards, 
Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views