Assalaamu
alaikum,
Natumai
hamjambo.
Tunaendelea
na risala juu ya maisha ya Mtume Ibrahim Alaihissalaam.
AYA: ALAMTARA ILALLADHI HAAJJA
IBRAHIMA FI RABBIHI AN AATAHULLAHUL MULK.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia
Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, imesomwa kipande cha aya 258
ya Sura Baqara, inayozungumzia Mtume Ibrahim Alaihissalaam.
Mtume Ibrahim alikabiliana na ufalme wa
Namrud. Ikumbukwe kuwa Azar aliyetajwa ndani Quran na aliyekuwa mshirikina
akiabudu masanamu, si mzazi wa Ibrahim bali ni ami wake. Mzazi wa Mtume Ibrahim
anaitwa Tarikh bin Naakhur, aliyekuwa Muislam. Pia wazazi wa Mtume Swallallahu
Alaihi Wasallam walikuwa Waislamu.
HADITHI: Mtume Swallallahu ALaihi
Wasallam amesema kuwa: mimi ni Mtume na Mpendwa wa Allah, mimi ni mbora kwenu
kwa kila hali; Allah Kaigawa dunia hii sehemu 2 – Uarabu na uajemi, Uarabu
ukapewa ubora na mimi ni Mwarabu. Katika Uarabu kuna kabila nyingi na bora ni
Quraish na hivyo mimi ni Mquraish. Katika Maquraish, kuna ukoo nyingi, bora ni
Bani Hashim na mimi nimetokana na Bani Hashim. Bani Hashim ina familia nyingi
na mimi katika familia Abdullah. Na eleweni kuwa mimi nimetoka kwenye mgongo
ilitwahirika kutoka Mtume Adam hadi wazazi wangu Abdullah na Amina.
Mtume Ibrahim alizaliwa huku mzazi wake
alishaiaga dunia hii na hivyo alilelewa na Azar. Azar na wakazi wote walikuwa
wakiabudu masanamu na Namrud wakiamuamini kama mungu wao. Ieleweke kuwa Mtume
anazaliwa tu tayari akiwa Mtume na hivyo anakuwa na maarifa ya Allah. Tangu
utotoni, alipowaona Azar na wenzake wakiabudu masanamu, Mtume Ibrahim huchukia
sana moyoni na alitafuta jinsi ya kuvunja masanamu.
Maswali
/ maoni yanakaribishwa
JazakAllah,
Muhammad
KHATRI
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...