Assalaamu
alaikum,
Natumai
hamjambo. Natumai mnakumbuka tulipoishia katika risala yetu ya Mi-‘iraj. Mtume
Swallallahu Alaihi Wasallam alianza safari yake kuelekea Msikiti wa Aqsa na
njiani alionyeshwa baadhi ya alama.
SUB-HANALLADHI
ASRA BI-ABDIHI LAYLAN MINAL MASJIDIL HARAAMI ILAL MASJIDIL AQSA, ALLADHI
BAARAKNA HAWLAHU LINURIYAHU MIN AYATINA, INNAHU HUWAS SAMIUL BASIR. (SURA BANI
ISRAIL, AYA 1)
Baada
ya Kumshukuru Allah na kumtakia Rehma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi
Wasallam, aya hapo juu ni ya kwanza ya Sura Bani Israil, ambayo inazungumzia
msafara wa miraji.
Tafsiri
ya aya:
Utukufu
ni Wake Yeye Aliyempeleka Mja Wake katika sehemu tu ya usiku kutoka Msikiti wa
Haraam (Makkah) hadi Msikiti wa Aqsa (Palestina), ambao umezungukwa na Baraka
Zetu, ili Tumuonyeshe baadhi ya alama zetu. Hakika Allah ndiye Mwenye Kusikia
Mwenye Kuona.
Mtume
Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam alipokuwa akielekea Masjidul Aqsa, njiani
alimuona Mtume Musa akisali ndani ya kaburi lake. Hapa tunapata kufahamu kuwa
Mitume si tu wapo hai ndani ya makaburi yao, huwa wanasali na pia hupata rizki.
Mtume
Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam alipofika Masjidul Aqsa, Jibrail alitoboa
sehemu moja iitwao Sakhra na kisha kumfunga mnyama wao. Kisha Jibrail alitoa
adhana juu ya Msikiti wa Sakhra na kurudi Masjidul Aqsa. Hapa Mitume wote
walikuwepo na kila mmoja akawa anafikiria je ni Mtume Adam ambae ni baba wa
binadamu wote, ndiye atakaesalisha leo? Au Khalili wa Allah, Mtume Ibrahim? Au
ni Mtume Nuh kwani baada ya tufani ya zama zake, masuala ya uzaaji ulianza
kupitia yeye. Lakini Jibrail alimshika mkono Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi
Wasallam na kumpeleka mbele na kumuambia awa imamu wa Mitume wote. Baada ya
sala, kila Mtume alisoma khutba ya kumsifu Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi
Wasallam.
Baada
ya hapo Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam alifuatana na Jibrail
kuelekea mbinguni. Kuna riwaya 2; (1) walienda kumtumia mnyama yule yule Buraaq
au (2) Miraji ni jina la ngazi mmoja na hivyo walitumia ngazi hiyo kuelekea
juu. Walipofika mbingu ya 1, mlango ulikuwa umefungwa. Jibrail alipiga hodi na
kuulizwa ni nani? Alijibu mimi Jibrail niko na Mtume Muhammad Swallallahu
Alaihi Wasallam. Baada ya kuulizwa kama Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi
Wasallam ameitwa, Jibrail akajibu kuwa ndiyo.
Mtume
Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam alimuona mzee mmoja ambae kila akiangalia
vivuli upande wake wa kulia basi hutabasamu lakini anapoangalia vivuli upande
wa kushoto basi hulia. Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam aliuliza ni
nani huyo na kwa nini mara hutabasamu na mara hulia? Jibrail alijibu kuwa
msalimie huyu ni mtume Adam, upande wake wa kulia ni watoto wake walioleta
imani na ndyo maana hutabasamu akiwaona. Wale wa kushoto ni watoto wake
waliokataa imani na ndyo maana hulia akiwaona.
Mtume
Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam alianza kuchupa mbingu moja baada ya
nyingine huku akikutana na Mitume kila mbingu. Mbingu wa 2 alikutana na Mtume
Yahya na isa, ya 3 Mtume Yusuf, ya 4 Mtume Idris, ya 5 Mtume Harun, ya 6 Mtume
Musa nay a 7 alikutana na Mtume Ibrahim aliekaa kwa kuegemea Baitul Maamur.
Baitul Maamur ni kibla ya Malaika mbingu ya 7, ambamo kila asubuhi na jioni
Malaika 70,000 wapya huingia hapo. Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam
aliwasalisha Malaika.
FAIDA
YA QURAN:-
1.
Surah Al Fatihah ina nguvu ya uponyaji wa magonjwa yote. Soma
Surah Al Fatihah kabla ya kuanza kazi yoyote muhimu maishani.
2.
Iwapo utasoma aya 4 za Surah Al Baqarah ikifuatiwa na Ayatul
Kursi na aya 3 za Surah hii, shetani atakaa mbali.
Maoni
/ maswali yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad
KHATRI
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...