Ads 468x60px

Sep 3, 2013

Mtume Ibrahim - PT 1 (KISWAHILI)


Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo.
Siku tunazoenda nazo zinaitwa siku za hijja, kwa maana baada ya Ramadhani, matayarisho ya safari ya hijja kwa wenye kujaaliwa huanza.
Ibada ya hijja, ambayo ni nguzo ya tano ya Kiislam, ina mahusiano ya ukaribu sana na Mtume Ibrahim Alaihissalaam na familia yake, na ndyo maana nimeona ni vyema nikaanzisha risala yenye kuelezea baadhi ya fadhila zake kwa kifupi.
AYA:  ALAMTARA ILALLADHI HAAJJA IBRAHIMA FI RABBIHI AN AATAHULLAHUL MULK.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, imesomwa kipande cha aya 258 ya Sura Baqara, inayozungumzia Mtume Ibrahim Alaihissalaam. Siku tunazoenda nazo hivi sasa ni siku za matayarisho ya ibada ya Hija, ambayo ina mahusiano ya ukaribu sana na Mtume Ibrahim na maisha yake. Kwa hali hii tumeona ni bora kuzungumzia kwa muhtasari sehemu ya maisha ya Mtume Ibrahim.
Ikumbukwe kuwa ni kudra ya Allah na pia ni kawaida ukizingatia kidunia kuwa mwenye kukusudiwa kupewa cheo fulani basi kwanza anajaribiwa na mitihani. Baada ya mitihani ndipo hupewa cheo.
Licha ya Utume, ni cheo gani Mtume Ibrahim alikusudiwa kupewa?
AYA:  QAALA INNI JAA-ILUKA LINNAASI IMAMA. Ewe Ibrahim Sisi tutakujaalia uongozi (imam) wa watu wote. (2: 124)
TAFSIRI YA AYA: Ewe Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, je hukumuona yule aliyehojiana na Ibrahim juu ya Mola wake Mlezi ambae Tulimjaalia ufalme mkubwa?
Ikumbukwe kuwa duniani wamepita wafalme 4 tu ambao ufalme wao pekee ulienea ulimwengu mzima. Wawili walikuwa Waislamu na wawili makafiri.
Makafiri: Namrud na Buzdinaqs
Waislamu: Mitume Suleiman na Dhul Qarnain.
Ufalme wa Mtume Suleiman si tu ulikuwa ardhini bali pia hata mbinguni kwa ndege na upepo pia. Mtume Suleiman akiiamuru upepo kuwapeleka yeye na watu wake, basi upepo huwapeleka kutoka sehemu moja kwenda wanapotaka.

Maswali / maoni yanakaribishwa
JazakAllah,
Kind Regards,
Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views