Ads 468x60px

Nov 13, 2013

Ashura (Kiswahili)


Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo.
ASHURA
Ashura ni mwezi 10 Mfungo 4 (Muharram), na ni siku ambamo matukio mengi yalitokea na yatatokea. Baadhi yao ni hizi zifuatazo:-

1) Allah Aliziumba Arshi, Kursi, mbingu, ardhi, jua, mwezi, nyota na pepo.
2) Mtume Adam aliumbwa na kuingizwa Peponi. Dua yake pia alikubalika siku hiyo alipoletwa ardhini.
3) Mtume Ibrahim alizaliwa na tarehe hiyo moto ulikuwa baridi na salama juu yake
4) Mtume Musa na ummah wake uliokoka na shari za Firauni ambaye aliangamizwa na watu wake.
5) Mtume Isa alizaliwa na tarehe hiyo aliinuliwa mbinguni.
6) Mashua ya Mtume Nuh ilitia nanga kwenye mlima Judi, Uturuki.
7) Mtume Suleiman alijaaliwa ufalme mkubwa
8) Mtume Yunus alitolewa kutoka tumbo la samaki mkubwa (papa)
9) Mtume Yakub alirejeshewa nuru ya macho yake.
10) Mtume yusuf alitolewa kutoka kisima.
11) Mtume Ayub aliondokewa kabisa na maumivu
12) Mvua ya kwanza kutoka mbinguni ilianza kunyesha
13) Saum ya siku ya hiyo ilikuwa maarufu sana na hata faradhi kwa baadhi ya ummah.
14) Imam Husein, mjukuu wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, aliuliwa kikatili huko Karbala, Iraq.
15) Qiyama itasimama
Pia ni bora kusoma ya siku ya Ashura, nayo ni hii ifuatayo:

KISHA SOMA MARA 7:-

Masimulizi ya mauaji ya kikatiliya Imam Husein katika risala inayofuata in sha Allah.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI 

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views