Assalaamu
alaikum,
Natumai
hamjambo. Ifuatayo ni risala fupi kuhusu hijrah – kuhama kutoka Makkah na
kwenda Madina.
Kalenda
yetu pia huanzia mwenzi wa hijrah na ndyo maana inaitwa HIJRIYYAH. Ingawa mwaka
wetu wa 1435h haumaanishi kuwa safari hiyo ya hijrah imetimiza miaka
hiyo, la, bali kalenda ilianziwa baada ya muda Fulani.
AYA: THANIYATH NAINI IDH HUMA FIL
GHAARI IDH YAQULU LISWAHIBIHI LAA TAHZAN INNALLAHA MA-‘ANA.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia
Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, sehemu ya aya hapo juu ya 40
kutoka Sura Tawbah (9), inazungumzia msafara wa hijrah.
TAFISIRI: … naye ni wa pili katika
wawili walipokuwa katika pango, naye akamwambia sahibu wake: usihuzunike,
hakika Allah yuko pamoja nasi …
Dhulma dhidi ya Waislamu ilipokithiri,
Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alihukumiwa kuihama mji wa Makkah na kwenda
Madina. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alimkabidhi amana za watu Sy Ali na
kumwambia awalipe, kisha alale kwenye kitanda cha Mtume Swallallahu Alaihi
Wasallam na kesho yake aje Madina. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alitoka na
Sy AbuBakr. Kwa kuwa makafiri walipata taarifa ya kuhama kwa Mtume, walikaa nje
ya nyumba wakimsubiri kumuua. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alitoka akisoma
aya ya Sura Yasin, akachukua mchanga na kuwamwagia kichwani na wale wote
wakalala usingizi na Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam akapita.
Sy AbuBakr alimbeba Mtume Swallallahu
Alaihi Wasallam mgongono mwake na mwenyewe akatembea juu ya viganja vya miguu
ili maadui wasitambue vikanyago. Walipofika kwenye pango THOUR, Sy AbuBakr
aliingia ndani kuisafisha na kisha kumuita Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam.
Sy AbuBakr alifunga matundu yote ila moja tu ikabaki. Nyoka aliyekuwepo hapo
tangu zama za Mtume Musa kutaka kumuona Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam,
alishindwa kutoka na hivyo alimng’ata Sy AbuBakr kwenye mguu. Sy AbuBakr
alivumilia maumivu na machozi yalipobubujika kwenye uso wa Mtume Swallallahu
Alaihi Wasallam ndipo Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alimwekea Mate matukufu
na alipona.
Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam
alipowasili Madina alipokewa kwa shangwe na Qasida. Pia alijenga Msikiti mjini
hapo.
Maswali
/ maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad
KHATRI
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...