Ads 468x60px

Feb 3, 2013

Maulidi - Part 3

Assalaamu alaikum,

Natumai hamjambo na mlishiriki kikamilifu katika kusherehekea na kuadhimisha siku Tukufu ya kuzaliwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, mwezi 12 Mfungo 6 (Rabi-ul-Awwal).

Ni uthibitisho wa Hadith-ul-Qudsi, Allah Amesema: “Lau kama nisingemuumba Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam, basi nisingeumba Pepo, moto, Mwezi, Jua, mbinhu na ardhi, usiku na mchana na Mitume na Malaika”. Si hivyo tu bali Allah amesema kuwa “E Mpendwa! Lau kama nisingekuumba wewe basi Nisingejidhihirisha”. Nuru ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam iliumbwa kabla ya chochote, kama alivyosema: “Kitu cha kwanza Allah alichokiumba ni NuruYangu”. Nuru hii ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam ilikuwa juu zaidi karibu na Muumba wake kwa miaka 4,000. Allah alipokusudia kuumba, Aligawanya Nuru hii katika sehemu 4. 1) AliumbaKalamu 2) Meza Tukufu 3) Arshi 4) Viumbe vilivyosalia Allah alipotaka kumtuma Mjumbe wake Ardhini, Aliumba udongo wa Adam Alaihissalaam. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam amesema: “Mimi nilikuwa Mtume tangu Mtume Adam Alaihissalaam alikuwa baina ya udongo na maji”.

Kutoka bapa la Uso mmoja hadi nyingine, Nuru hii iliwekwa kwenye bapa la bwana Abdullah RadwiyallahuAnhu, baba wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam. Nuru hiyo baadae ikakaa kwenye tumbo la Mama Amina RadwiyallahuAnha, mama wa Mtumu Swallallahu Alaihi Wasallam. Katika ujauzito wa miezi 9, hakuhisi tabu wala kuona alama yoyote iliyo ya kawaida kwa kila mjamzito. Pia kila mwezi alipata habari njema kutoka kwa Mitume wa Allah. Mama Amina RadwiyAllahu Anha anaelezea kuwa siku ya kuzaliwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam ilipofika, ilikuwa wakati wa Alfajiri ya Jumatatu alipoona kundi la watu ikitelemka kutoka mbinguni wakiwa na bendera 3. 1 waliiweka kwenye ua la jumba lake, 1 juu ya paa la Al-Kaaba na 1 juu ya Masjidul Aqsa. Baadae wanawake wachache walimjia na kujitambulisha. 1 alikuwa Mama Maryam, Mama wa Mtume Isa Alaihissalaam, wa 2 alikuwa Aasiya mke wa Firauni, naa 3 alikuwa Mama Hajra mke wa Mtume Ibrahim Alaihissalaam. Wanawake wengine walikuwa watukufu wa Peponi. Wote hao walikuja kumhudumia. Baada ya matukio hayo ndipo Nuru ya ulimwengu, Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam alizaliwa. Quran ikatangaza kuwa: “Hakika imekuja kwanu kutoka kwa Allah Nuru na Kitabu kilicho wazi”. Wanazuoni mashuhuri wameeleza kuwa usiku wakuzaliwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam ni bora zaidi kuliko usiku wa LaylatulQadri, na kuwa mwezi wa Rabi-ul-Awwal ni tukufu zaidi kuliko mwezi wa Ramadhani. Sababu yake ni kuwa usiku waLaylatul Qadri, Quran imetelemka wakati usiku wa kuzaliwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, amezaliwa yule iliyomtelemkia Quran. Ulimwengu mzima ulifurahi kakuzaliwa kwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, na Al-hamdulillah hata leo wapenzi wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam wanaadhimisha siku hiyo kwa furaha kubwa. Hata hivyo, kuna maadui wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam wasemao kuwa kusherehekea ni upotovu na ubadhirifu. Allah awajaalie akili na imani sahihi. Allah atujaalie sisi sote mapenzi ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam. Amin Amin Amin

Maswali/ maoni yanakaribishwa.

JazakAllah,

Kind Regards,

Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views