Ads 468x60px

Feb 18, 2013

Sheikh Sayyid Abdul Qadir Jilani - PT 1 (Kiswahili)


Assalaamu alaikum,
 
Natumai hamjambo.
 
Mwezi uliopita nilijitahidi kuweka wazi suala la Maulidi pamoja na dalili zake kutoka Quran Tukufu, Hadithi na baadhi ya kauli za watu tofauti; ingawa nilishangaa hakuna swali iliyojitokeza!!! Huo ulikuwa mwezi wa kiongozi wa Mitume wote!
 
Mwezi (Mfungo) tulionao wa Rabi ul Akhar au Rabi ut Thani au Mfungo 7, ni mwezi wa masimulizi ya kiongozi wa Mawalii wa Allah (Marafiki wa Allah) - Sheikh Sayyid AbdulQadir Jilani Qaddasallahu Sirrah, na ifuatayo ni sehemu ya kwanza ya risala fupi:-
 
AYA:  ALAA INNA AWLIYA ALLAHI LA KHAUFUN ALAIHI WALAHUM YAHZANUN. (YUNUS: 62)

Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, aya hapo juu ya Sura Yunus, inazungumzia mawalii wa Allah

AYA: Jihadharini, marafiki wa Allah hawana hofu wala huzuni.

                      

Baba yake, Abu Saleh, alikuwa Walii na Mcha Mungu sana. Hukaa kwa siku kadhaa ndani ya pango bila ya kula na kufanya ibada ya Allah. Siku moja alishikwa na njaa na hivyo kuanza kutembea kando ya mto kutafuta chakula. Aliona tunda ikielea na kuiila. Mara nafsi yake ikamuuliza lau kama mmiliki wa tunda hilo akimuuliza siku ya Kiyama kuhusu kulak wake bila ya kuomba, je atajibu nini? Hivyo akaanza kumtafuta mmiliki hadi kufika kwenye bustani la matunda na kumuomba msamaha mmiliki wa bustani, Abdullah Somai, ambae alikuwa Walii pia. Mmiliki alimpangia masharti mawili ili amsamehe; 1 – aihudumie bustani lake lote kwa miaka 10 na baada ya hapo ndipo aambiwe sharti la pili. Abu Saleh alikubali kuhofia shitaka siku ya kiyama. Baada ya miaka 10, Abu Saleh aliongezewa miaka miwili tena na baada ya miaka hizo miwili, aliambiwa kumuoa binti wa mmiliki aliye kilema wa macho, mdomo, masikio, mikono na hata miguu!! Sharti hili ilikuwa ngumu sana lakini Abu Saleh aliikubali pia. Siku ya kuonana na mke wake, alipoingia chumbani na kumsalimia, mkewe alimjibu. Abu Saleh mara moja alitoka nje ya chumba akidhani kuwa amekosea chumba! Baba mkwe alimwambia hajakosea chumba na aliyejibu salamu yake ndiye mkewe aitwae Ummul Kheir Fatima. Alimwambia kuwa binti wake kuwa kilema wa macho, mdomo, masikio, mikono na miguu alimaanisha hajawahi kutenda madhambi. Kutokana na wacha Mungu hao ndipo alizaliwa Sh AbdulQadir.
 
Maswali/ maoni yanakaribishwa.
 
JazakAllah,
 
Muhammad Khatri
 
 

2 comments:

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views