Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo na mnaendelea na ibada tukufu ya swaum. Yafuatayo ni maswali yaliyoulizwa na baadhi ya ndugu zetu, majibu yake.
1) Mimi nilikuwa na swali la kuuliza kuhusu kufunga. Kuna usemi niliusikia watu wakisema kuwa kufunga kila mwezi siku ya tarehe 13, 14 na 15 kama kwa mtume Adam kuna fadhila kubwa sana katika zama zetu.
Je usemi huu ni kweli?
JIBU: Ni Sunnah kufunga kila mwezi tarehe zilizotajwa kwenye swali; wanazuoni wanasema huleta nuru usoni mwa mwenye kufunga siku hizo.
2) Ama baada ya salamu napenda kuuliza,kuna mtu aliishi na mwanamke miaka 8 akawa hafungi kwa sababu hakuwa na ndoa,mwaka huu mungu kamjalia keshafunga ndoa na ramadhani hii kafunga, je anatakiwa alipe za miaka iliyopita au anasamehewa zimepita.
JIBU: Huu ni mtihani kwa Waislamu. Kwanza kuishi na mtu wa jinsia tofauti kama mume na mke pasipo na ndoa ni haramu (ni zinaa). Hilo ni dhambi na dhambi, kama hakujua basi ni bora atubu kwa moyo mkunjufu hususan katika mwezi huu mtukufu. Hilo halina athari yoyote kwa swaum kwa kudai kuwa eti kwa kuwa hawana ndoa basi swaum haisihi!! La hasha!! Swaumu ni ibada tofauti. Kwa hali hii itabidi aliteacha swaumu analazimika kulipa swaum zake hara iwezekanavyo na itambidi aache swaum zote za Sunnah hadi amalizie kulipia faradhi.
3) Kwa kina mama wakati mwingine anapata uvivu au kuchoka ktokana na majukumu pengine kupika daku anashindwa kuswali taraweh kwa wakati,je akilala kisha akaamka usiku anaweza kuswali taraweh?na je kuna sura maalum za kusoma wakat wa swala na nilazima ziwe sura za kufuatana.
JIBU: Kwanza ieleweke kuwa muda wa sala ya Taraweh ni muda wa sala ya isha-i, ambayo huanza baada ya mwanga kupotea kabisa sehemu ya magharibi hadi alfajiri inapotanda. Kwa nyakati za mwezi huu muda wa isha-i unaisha takriban saa 11.15, hivyo mwenye kukamilisha ibada ya sala ya isha-i, taraweh pamoja na witri kabla ya muda huo, basi hana kosa ya kuacha sala.
4) Ikiwa Taraweh ni sunna,Allaah atauliza rakaa zilizopungua
JIBU: Ndio ni Sunnah lakini ni Sunnah iliyosisitizwa. Wanazuoni wametukataza kuziacha Sunnah zilizosisitizwa.
5) kama mtu kasahau kunuia je funga yake haikubaliwi,kuna utaratibu kuwa mtu anaweza kunuia mwanzoni mwa ramadhani badala ya kunuia kila siku?
JIBU: Kama amesahau kunuia basi hiyo itakubalika, ila kama amedharau kunuia basi hapo itambidi alipe swaum hiyo ila kutwa nzima atabaki katika hali ya swaum na wala sio kuanza kula!! Kunuia ni kila siku na mara moja kwa mwezi mzima.
Bado kama kuna mtu ana mushkil katika haya yaliyotajwa hapo juu, basi asisite kuuliza.
Maswali / maoni yanakaribishwa. Pia kama ukiona kimya kwa email kama moja baada ya kuuliza na hujajibiwa, basi nitashukuru sana kama ukiikumbushia.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...