Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo na mnaendelea na ibada ya swaum pamoja na ibada zingine.
Mwezi 17 ya Mfungo huu wa Ramadhani, vita vya kwanza vilitokea huko Badri. Kwa bahati, siku hiyo ilikuwa Ijumaa na mwaka huu pia siku imeangukia ya Ijumaa - LEO. Kumbukeni kuwa mwenye kuomba dua kwa baraka ya Mashahidi wa vita vya Badri, basi dua yake hukubalika. Namalizia risala fupi ya Badri, ila kwanza kuna swali imeulizwa.
SWALI: kuna mstikiti niliswali taraweh lakini nilishangaa tuliswali rakaa 8 na witri 3 jumla 11 tarawehe ikaisha. Nimezoea kuswali rakaa 20 je hii ni sawa? nilimuuliza mwenyeji wangu akanijibu ni sawa kwani tumeswali rakaa 11 kwa sababu tumesoma sura ndefundefu, ukisoma sura ndefu ndefu unasoma rakaa 11,
Nawale wanaosoma rakaa 20 wanasoma sura fupifupi. pia nikahisi ule msikiti ni wa aswali suna ,kwani hata ile kunuia swaumu hakuna na vitu vingi nikaona tofauti.
Je kunatofauti gani kati sisi na aswali suna? na msikiti kama huu unaweza endelea kuswali? nisaidie tafadhari.
JIBU: Kama mtakumbuka kupitia risala zangu zilizotangulia kuwa taraweh ni rakaa 20 wala sio 8 kama baadhi wanavyodai. Uhakika wa rakaa 8 katika Hadithi inakuja hivi; Katika Bukhari imeelezwa: Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alikuwa na desturi ya kusali SWALATUL LAYL (Sala ya Usiku) rakaa 8 + 3 witri, jumla 11.
Kumbukeni kuwa hiyo ilikuwa ni desturi ya kila siku. Mimi nauliza je kama ni taraweh ambayo imetajwa katika Hadithi za Ramadhan, kwa nini kwenye Hadithi hii itajwe SALA YA USIKU na si TARAWEH???
Hii inathibitisha kuwa sala ya usiku na Tahajjud. Taraweh ni rakaa 20 na wala haina pingamizi.
Ni bora kutosali katika misikiti ya Answar Sunnah kwani wana itikadi zinazotofautiana za Kiislamu.
Risala ya Badri ...
Katika vita vya Badri, Waislamu walikuwa 313 tu wakiwa na farasi 17 tu na mikuki kama 8 na pia hawakujianadaa kabisa kupigana. Makafiri walikuwa kati ya 900 na 1,000 na kila mmoja alikuwa na farasi au ngamia na vifaa vyote na walijiandaa kikamilifu. Makafiri walikuja na dhamira ya kuwadhalilisha Waislamu. Masahaba walimtayarishia Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam banda la kukaa na kutoa amri. Iliponadiwa nani atakaemlinda Mtume Swallallahu Alaihi wasallam, AbuBakr Siddiq ndiye aliyejitokeza.
Makafiri 70 waliuawa katika vita wakati Masahaba 14 tu wakawa mashahidi. Usiku wa kuamkia siku ya vita, Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alipotembelea uwanja wa vita, aliweka alama kuwa kafiri Fulani atakufa hapa na Fulani hapa, na ndivyo ikawa.
Wakati wa vita, walikuja watoto wawili kwa AbdulRahman bin Auf na kumwambia waonyeshwe aliko Abu Jahal ili wakamuue kwani anamtukana sana Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam. Walipoonyeshwa, mmoja alimpiga panga la nguvu hadi mguu kuvunjika. Jeuri lake likawa pale tu kwani kabla ya kufa alisikitika mno kupigwa na watoto wadogo badala ya jemedari kama yeye.
Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...