Ads 468x60px

Jul 30, 2013

RAMADHAN KAREEM - PT 9 (LAYLATUL QADRI)‏ (KISWAHILI)


Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo na mnaendelea na ibada ya swaum pamoja na ibada zingine. Mwezi mtukufu ndyo inatukimbia kwa kasi sana kwani tunakamilisha theluthi 2 yake leo, hivyo bado theluthi tu!!
Baada ya Kumshukuru Allah na kumtakia Rehma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam, Sura Qadr inazungumzia fadhila za usiku wa Laylatul Qadri. 
Fadhila za Laylatul Qadr.
Aya: Hakika Tumeitelemsha (Quran) katika usiku uliotukuka (wa Laylatul Qadri). Ewe Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, je unafahamu Laylatul Qadr ni nini? Laylatul Qadr ni bora kuliko ibada ya miezi 1,000. (humo) Malaika hushuka pamoja na Jibrael, kwa idhini ya Mola wao na wanaomba usalama na amani hadi alfajiri inapotanda.
Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alikuwa akiwasimulia Masahaba ujasiri wa Mcha Mungu wa Bani Israel, ambae mchana hufunga saumu na kupigana jihad na usiku hukesha katika ibada ya Allah, ilikuwa hivyo kwa miaka 400; tukumbuke kuwa watu wa umati zilizopita, pamoja na umri zao kuwa mkubwa, hata miili yao ilikuwa kubwa na pana.
Masahaba wakahuzunika na kusema Ewe Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, bila shaka hao watatuzidi katika thawabu kwani sisi umri zetu ni fupi. Allah Akatelemsha sura nzima ya Qadri kuwapa habari njema umma wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam.
Baadhi ya alama zinazopatikana katika usiku wa Laylatul Qadri ni kuwa usiku huo mbwa hawabweki, maji ya bahari ambayo ni chungu lakini usiku huo huwa tamu kupita asali, nyota za mbinguni hazianguki, kunakuwa na utulivu usiku huo, kama upo ndani ya ibada na ukajihisi mwili kusisimka basi elewa kuwa Malaika mtukufu Jibrael amekupa mkono.
 Ni usiku wa kufanya ibada kadri tuwezavyo, tuombe dua kwa Allah kwani Allah Anafurahi sana kuona waja wake wakimuomba. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alitoa mfano wake kuwa mtu 1 alisafiri na ngamia wake akiwa na chakula cha kutosha. Alipofika porini, alishtukia ngamia wake ametoweka, hivyo hakuwa na la kufanya. Akalala huku akaweka kichwa juu ya jiwe anasubiri kifo. Alipozinduka, alimuona yule ngamia wake amesimama kichwani mwake. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam akawauliza Masahaba, niambieni huyu mtu atakuwa na furaha kiasi gain? Masahaba wakajibu kuwa furaha isiyo na mfano. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam akasema Allah zaidi kuliko huyo mtu wakati mja anapomuomba.
Pia ni bora kusoma Qasida Burdai kwani ni Qasida iliyokubalika kwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam na hivyo ina faida tele.
Kithirisha kusoma: ALLAHUMMA QINA ADHABANNAARI WA-ADKHILNAL JANNATA MA-AL ABRAARI YAA AZIZU YAA GHAFFAARI, katika siku 10 za mwisho.
Allah atukubalie ibada zetu, amin.

Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views