Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo na mnaendelea na ibada ya swaum pamoja na ibada zingine.
Pengine email hii ilipaswa kuwa ya mwanzo lakini si haba ...
Baadhi ya matukio (tarehe) muhimu katika mwezi wa Ramadhani:
Tarehe 1: Kuzaliwa kwa Sheikh Sayyid AbdulQadir Jilani
Tarehe 3: Fatima binti Rasul RadwiyAllahu Anha kuiaga dunia
Tarehe 10: Mama Khadija RadwiyAllahu Anha kuiaga dunia.
Mama aliyekuwa tajiri na mfanyabiashara maarufu wa Makkah, aliolewa na Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam akiwa na umri wa miaka 40 wakati umri wa Mtume ulikuwa miaka 25. Na ilitokana na uaminifu wa Mtume katika safari zake za biashara ya Mama Khadija. Mtumwa wake alimsimulia kuwa kila Mtume alipotembea basi kuwa wingu nayo ilitembea nae ikimpa kivuli. Na pia katika safari yake ya kwanza tu, wakati wengine walipata hasara katika biashara zao, Mtume alimletea faida maradufu Mama Khadija. Hicho kilimvutia sana hadi kupeleka posa la kutaka kuolewa na Mtume.
Baada ya kuolewa, Mama Khadija alisalimisha mali yake yote kwa Mtume ili itumike katika kuinusuru Uislamu.
Tarehe 17: Vita vya Badri (kisa kitafuata katika risala ya baadae) na Mama Aisha RadwiyAllahu Anha kuiaga dunia.
Mama Aisha, ambae ni binti wa Sayyidina AbuBakr Siddiq RadwiyAllahu Anhu, alikuwa mjuzi sana katika mambo ya dini na anamfuatia Bwana Abu Huraira katika kupokea riwaya kwa wingi Hadithi kutoka kwa Mtume.
Tarehe 21: Kuuawa shahidi kwa Sayyidina Ali RadwiyAllahu Anhu.
Usiku wa 21, 23, 25, 27 na 29 ni Laylatul Qadr.
Katika 10 hizi za kati, tukithirishe sana kutamka ALLAHUMMA RABBANAGH FIRLANA DHUNUBANA YAA RABBAL AALAMIN.
Na katika 10 za mwisho: ALLAHUMMA QINA ADHABANNAARI WA-ADKHILNAL JANNATA MA-AL ABRAARI YAA AZIZU YAA GHAFFAAR.
Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...