Assalamu Alaikum
Natumai hamjambo na
mnaendelea na kumi za kati za Mfungo wa Ramadhan. Tunaendelea na risala yetu...
Baada
ya Kumshukuru Allah na kumtakia Rehma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi
Wasallam, leo Insha Allah tutazungumzia kuhusiana na mambo yanayo batilisha
saumu.
1) Mwenye kula, kunywa au kumuingilia mke katika
hali ya kuwa anafahamu kuwa yumo ndani ya saumu, vinginevyo saumu
haitabatilika.
2) Mwenye kuvuta sigara, kiko na vinavyo fanana
navyo vya kuvuta.
3) Mwenye kutafuna tambuu au tumbaku hata kama
atatema.
4) Mwenye kuweka sukari, pipi, n.k. mdomoni kisha
ikayeyuka na akameza mate yenye ladha ya vitu hivyo.
5) Kama kulikuwa na kitu kimenasa kwenye meno yenye
ukubwa mfano wa mbegu ya maharage, ukakimeza, au kilikuwa ndogo ya hapo ila
ukaitoa kisha ukaimeza itabatilisha saumu. Pia ukatokwa na damu kwenye meno
mfano wa mate na ukahisi ladha ya hiyo damu itabatilisha saumu.
6) Matumizi ya sindano au ukaweka dawa puani au
masikioni au ukatia mafuta masikioni itabatilisha saumu. Maji yakiingia
masikioni haitaleta madhara kwa saumu.
7) Ulikuwa ukisukutua na bahati mbaya maji yakavuka
koo au ulikuwa ukisafisha pua na maji yakavuka hadi kuelekea kwenye bongo basi
itabatilisha saumu. Hata hivyo kama ulikuwa hufahamu kuwa umo ndani ya saumu
basi haitabatilisha.
Maswali
/ maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad
KHATRI
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...