Ads 468x60px

Oct 1, 2013

MTUME IBRAHIM - PT 7‏ (Kiswahili)

Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo. Ijumaa Kareem
Tunaendelea na risala juu ya maisha ya Mtume Ibrahim Alaihissalaam.
AYA:  INNAS SWAFAA WAL MARWAATA MIN SHA-‘AAIRILLAH.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, hapo juu ni aya 158 ya Sura Al Baqarah, inayozungumzia mhangaiko aliyoupata mke wa Mtume Ibrahim, Mama Hajirah akimhangaikia mwanae Mtume Ismail.
Allah Anasema: Hakika Milima ya Swafaa na Marwa ni miongoni mwa alama za Allah. Alama huwa ya aina 2 – 1 ya kikabila na 2 ya madhehebu. Alama za kikabila hubadilika lakini za madhehebu hazibadiliki. Mfano kuvaa msalaba ni alama ya kimadhehebu ya kikristo na hivyo Muislamu akiivaa basi imani itamtoka.
Basi Swafaa na Marwa zimekuwa vipi alama za Allah? Ni kwa sababu miguu mitukufu ya mja mtakatifu wa Allah, Mama Hajirah, yalikanyaga milima hiyo.
Labda kwa kukumbusha tu, baada ya Mtume Ibrahim kutolewa kutoka kwenye moto, cha kujiuliza hapa: ni kwa nini Mtume Ibrahim alipata misukosuko yote hiyo? Allah Anasema : INNI JAA ILUKA LINNASI IMAMA; Nitakufanya uwe muongozi wa watu (Al Baqarah: ..124). Kisa hicho kilitokea nchini Iraq na baada ya hapo Mtume Ibrahim alihukumiwa kuihama nchi yake ya Iraq  na kuelekea nchi ya Shaam (Syria). Mtume Ibrahim aliridhia na hivyo kuhamia Shaam.
Mtume Ibrahim alikuwa na wake wawili – Mama Sarah (mwanae ni Mtume Is-haq) na Mama Hajirah (mwanae ni Mtume Ismail). Hapo nako alihukumiwa kawaache Mama Hajirah na mwanae Ismail kwenye jangwa palipo Makkah leo. Aliwaachia tende kidogo na maji. Mara tu Mtume Ibrahim alipoanza kuondoka baada ya kuwaacha kwenye jangwa, Mama Hajirah alimuuliza; hivi unatuacha hapa je hii ni amri ya Allah? Mtume Ibrahim alimjibu; ndiyo. Mama Hajirah akamuambia aende kwa amani kwani kamwe Allah hatowaacha katika shida.
Yale maji yalipoisha, basi Mtume Ismail, aliyekuwa mtoto mchanga wakati huo, alishikwa na kiuu na njaa na hivyo kuanza kulia. Mama Hajirah alimwonea huruma mwanae katika hali hiyo na hivyo alikimbilia kuupanda mlima Swafaa ili aweze kutupa macho kama kuna mtu yoyote akionekana kwa mbali ili aje amsaidie. Kisha anarudi kumwangalia mwanae na mara hupanda mlima Marwa. Alifanya hivyo mara 7 na ndiyo maana baada ya kutufu Al Kaaba ni wajibu kukimbia mara 7 baina ya milima hiyo. Mtume Ismail katika kupiga miguu yake ardhini ndipo yakatoka maji na Mama Hajirah aliimbia ZAMZAM (simama) na maji yale yakatulia. Wanazuoni wanasema wanasema lau kama Mama Hajirah asingetamka hivyo, basi maji yangeenea ulimwengu mzima.
Maji ya zamzam yana baraka sana, kama alivyoeleza Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam kuwa: (1) mtu akinywa maji ya zamzam tu bila ya kula chochote, basi yatamtosheleza na wala hatasikia njaa. (2) Kunyweni maji ya zamzam na yale yaliyosalia baada ya kutawadha kwa kusimama ili maji ya baraka ienee mwili mzima kwa kasi. (3) Dua inayoombwa wakati wa kunywa maji ya zamzam hukubalika.
Wasafiri walipopata taarifa za kuwepo kwa maji maeneo hayo, wakaanzisha makazi yao hapo. Mama Hajirah aliwaambia kuwa milki ya maji ya zam zam ni yake ila aliruhus makazi. Hapo ndipo Mtume Ismail akaanza kulelewa na hadi kuwa mkubwa huku Mtume Ibrahim akiwatembelea mara kwa mara.
Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views