Natumai hamjambo. Ijumaa Kareem.
Mwezi wa Dhul Hijjah (Mfungo 3) ndyo huo unakaribia, panapo majaaliwa in sha Allah, mwezi utaandama jumapili hii na jumatatu ndyo mwezi mosi
Kwa wale waliobahatika na safari ya hijja mwaka huu, wanapokuwa katika hali ya ihraam (vitambaa vyeupe viwili kwa mwanamme na vazi nyeupe la kawaida kwa mwanamke), hawaruhusiwi kukata kucha wala kunyoa (hata nywele za sehemu ya siri) hadi baada ya kuvua ihraam.
Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam amesema katika Hadithi aliyonukuu Imam Muslim kuwa : mnapoona mwezi (kuandama) wa Dhul Hijjah, basi mwenye kukusudia kuchinja ajizuie kukata kucha na kunyoa (nywele) hadi baada ya kuchinja. Mwenye kufanya hivyo atapata thawabu nyingi.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...