Ads 468x60px

Aug 2, 2013

RAMADHAN KAREEM - PT 9 (JUMA'ATUL WADAH)‏ (KISWAHILI)


Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo na mnaendelea na ibada ya swaum pamoja na ibada zingine. Mwezi mtukufu ndyo inatukimbia kwa kasi sana kwani leo ni Ijumaa ya mwisho ya Mfungo kwa mwaka huu!!
Baada ya Kumshukuru Allah na kumtakia Rehma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam, imesomwa aya za Quran Sura Juma’a inayozungumzia fadhila ya Ijumaa.
Fadhila za ijumaa kwa kuwa leo ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani mwaka huu. Tafsiri ya aya:
Enyi mloamini, ikinadiwa (ikiadhiniwa) kwa ajili ya sala ya Ijumaa, nendeni kwa ajili ya dhikri ya Allah (sala ya Ijumaa), na acheni manunuzi (kazi/ biashara) zenu, hii ni bora kwenu ikiwa mnafahamu.
Ijumaa ilivyoanzishwa. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alipohama Makkah kwenda Madina, alipumzika kwenye kitongoji cha Quba kwa siku 4 na kuweka jiwe la msingi wa Masjid Quba. Mwenye kusali rakaa 2 sunnah humo hupata thawabu ya umra 1. Siku ya Ijumaa asubuhi Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alianza safari ya kuelekea Madina. Alipofika kitongoji cha Bani Saalim, ilikuwa wakati wa adhuhuri na hapo ndipo Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alisalisha Ijumaa ya mwanzo. Baada ya hapo ndipo alipokelewa kwa shangwe kubwa alipowasili Madina.
Hadithi: Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam amesema kuwa mwenye kuoga vizuri siku ya Ijumaa, akapiga mswaki, akavaa nguo nzuri kama si mpya, akapaka manukato, akaenda Msikitini na bora kwa kutembea kama si mbali, akawahi na kukaa nafasi ya mbele au pale anapopata nafasi ila tu asiwabughudhi watu (riwaya nyingine inasema mwenye kuwa wa mwanzo atapata thawabu ya kuchinja ngamia katika njia ya Allah, wa pili atapa thawabu ya kuchinja ngo’mbe, wa tatu thawabu ya kuchinja mbuzi, wa nne thawabu ya kuchinja kuku, wa tano thawabu ya kutoa yai, nk), kisha akasikiliza khutba kwa makini bila ya kujishughulisha na jambo lolote, basi mtu huyo kwa kila hatua 1 atapata thawabu ya sala za mwaka mzima na hatua ya 2 atapata thawabu ya kukesha mwaka mzima.
Riwaya nyingine inasema kuwa mtu huyo anafutiwa madhambi kutoka Ijumaa moja hadi nyingine.
Pia tulizungumza mwanzoni kuwa mwezi huu thawabu ya faradhi 1 ni sawa na 70, Ijumaa 1 ni sawa na Ijumaa 70 za miezi ya kawaida.
Fadhila nyingine ya Ijumaa ni kuwa siku hiyo Mtume Adam Alaihissalaam aliumbwa, siku ya Ijumaa aliingizwa Peponi na siku ya Ijumaa aliletwa duniani, kiyama nayo itakuwa siku ya Ijumaa. Ndiyo maana kila siku ya Ijumaa wanyama, ndege na Malaika wanatetemeka kwa hofu kuwa isije ikawa kiyama leo. Ijumaa ni siku ambamo dua hukubalika. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam amesema nisalieni kwa wingi sana siku ya Ijumaa. Ndiyo maana Misikiti ya Ahlil Sunnah wal jamaa duniani kote husimama qiyam ya kumsalia Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam.

Allah atukubalie ibada zetu, amin.
Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah, 
Muhammad KHATRI 

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views