Ads 468x60px

Apr 22, 2014

Sayyidina AbuBakr Siddiq - PT 3‏ (KISWAHILI)


Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo.
Tunaendelea na risala ya Sayyidina AbuBakr Siddiq RadwiyAllahu Anhu, na siku ya yeye alipoiaga dunia ni kesho, Jumatano mwezi 22 Jamadi-ul-Akhar (Mfungo Tisa).

Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, aya hapo juu ya 40 kutoka Sura Tawba inayoelezea fadhila mmojawapo ya Khalifa wa 1 wa Kiislam, Sayyidina AbuBakr Siddiq na ndiye tutakaemzungumzia kwani tarehe 22 ya mfungo huu 9 aliiaga dunia.
TAFSIRI: Wakati wawili (Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam na Sy AbuBakr) walipokuwa ndani ya pango, mmoja alimuambia mwenzake usihuzunike, hakika Allah yuko pamoja nasi.
Sayyidina AbuBakr alikuwa mjasiri na shupavu sana kiasi cha kwamba wakati wa Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam kuiaga dunia, baadhi ya mambo magumu yalijitokeza lakini aliyatatua kwa ujasiri mkubwa. Mmojawapo ikiwa: Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam alituma jeshi la Masahaba shupavu na bado walikuwa ndani ya kitongoji cha mji wa Madina wakati Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam alipoiaga dunia. Baadhi ya Masahaba walipomuomba Sayyidina AbuBakr kurejesha jeshi hilo ili kukabiliana na vurugu ikiwa zitatokea, alikataa kwa madai kuwa Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam alishaituma jeshi hilo na hivyo yeye hawezi kuirejesha.
Pia baadhi ya Masahaba walikataa kutoa zaka baada ya Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam kuiaga dunia, lakini Sayyidina AbuBakr kwa ujasiri wake alihakikisha kila mstahiki wa kutoa zaka anatekeleza amri hiyo hata kama ikibidi kukabiliana nao kwa jihad.
Bado hali ilikuwa haijatulia vizuri, mara akajitokeza Musailm bin Kazzaab aliyedai utume. Wafuasi wake walifikia 100,000 dhidi ya jeshi la Waislam kiasi cha 10,000; Waislam walishinda vita hivyo.
FADHILA: Ingawa Sayyidina Abu Bakr Siddiq Radwiyallahu Anhu alikuwa mtu mwenye fadhila nyingi, lakini pamoja na yote hayo, kubwa zaidi ni kuwa vizazi vyake vinne (4) walikuwa Masahaba.  1 – Yeye mwenyewe Radwiyallahu Anhu.   2 – Baba yake, Abu Quhafa Radwiyallahu Anhu.    3 – Mwanae, AbdulRahman Radwiyallahu Anhu     4 – Mjukue, Abu Atiq Muhammad Radwiyallahu Anhu.
Baadhi ya mambo muhimu ya Sayyidina Abu Bakr Siddiq Radwiyallahu Anhu alikuwa wa kwanza:
1 – Kusilimu.
2 – Kukiita Quran Tukufu “MSAHAFU” (Kitabu).
3 – Kuikusanya Quran Tukufu baada ya Mtume Sall-Allahu Alaihi Wa Sallam.
4 – Kupigana na makafiri
5 – Kuwa Khalifa
6 – Khalifa aliyeanza ukhalifa katika uhai wa baba yake.
7 – Kumchagua Khalifa atakaemfuata.
8 – Kujenga hazina.
9 – Kuitwa Khalifa.
10 – Kujenga Msikitimiongoni mwa Waislamu
11 – Miongoni mwa wafuasi wa Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam kuingia Peponi.
Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views

Follow by Email