Ads 468x60px

Apr 29, 2014

Sayyidina AbuBakr Siddiq - PT 4 (MWISHO)‏ (Kiswahili)

Assalaamu alaikum,

Natumai hamjambo.
Namilizia risala ya Sayyidina AbuBakr Siddiq RadwiyAllahu Anhu.



Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, aya hapo juu ya 40 kutoka Sura Tawba inayoelezea fadhila mmojawapo ya Khalifa wa 1 wa Kiislam, Sayyidina AbuBakr Siddiq.
TAFSIRI: Wakati wawili (Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam na Sy AbuBakr) walipokuwa ndani ya pango, mmoja alimuambia mwenzake usihuzunike, hakika Allah yuko pamoja nasi.
Kuhusu fadhila za Sayyidina Abu Bakr Siddiq Radwiyallahu Anhu, kuna aya nyingi za Quran Tukufu na Hadithi pia; kati ya hizo Hadithi 181 zimepokelewa katika fadhila zake tu, Hadithi 88 zimepokelewa na Sayyidina Abu Bakr & Sayyidina Umar bin Khattab Radwiyallahu Anhuma, 17 zimepokelewa na Abu Bakr, Umar & Uthman bin Affan Radwiyallahu Anhum, 14 zimepokelewa na Makhalifa wote wanne, 16 zimepokelewa na Makhalifa wote wane pamoja na Masahaba wengine. Hivyo, katika jumla ya Hadithi 316, Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam ametuthibitishia fadhila ya sahiba wake wa pango, Sayyidina Abu Bakr Siddiq Radwiyallahu Anhu.
Matukio matatu muhimu sana yalitokea wakati wa Ukahlifa wake:
1)    Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam aliipeleka jeshi la Masahaba shupavu na wakati bado ilikuwa katika kitongoji cha mji wa Madina, Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam aliiaga dunia. Baadhi ya Masahaba walimshauri Sy AbuBakr kuirejesha jeshi hilo ili kama kukitokea mchafuko wowote, basi watasaidia. Sy AbuBakr alisema hawezi kuirudisha jeshi ambalo Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam alishaituma.
2)    Alijitokeza Musailmah bin Kazzaab aliyedai utume, akawa na wafuasi laki moja. Sy AbuBakr aliituma jeshi ya Masahaba shupavu 10,000 kukabiliana nae huko Yamama. Waislamu hao wachache walishinda ila wale waliohifadhi Quran wapatao 700 waliuawa mashahidi. Baada ya hapo ndipo Sy AbuBakr alianza kazi ya kuikusanya Quran iwe msahafu.
3)    Kundi la Masahaba walimjia Sy AbuBakr wakidai kuwa kwa kuwa Mtume Swall-Allahu Alaihi Wasallam ameshaiaga dunia, basi na wao hawatatoa zaka. Sy AbuBakr alisimama kwa ujasiri na kutangaza jihad dhidi yao na kusema kuwa kila yule aliyetoa japo mbuzi, atahakikisha anafanya hivyo.
Imani ina matawi 360 na Sy AbuBakr alijaaliwa matawi yote. Siku ya Qiyama, kila atakaeingia Peponi, ataitwa kupitia mlango maalumu kutokana na alivyo kithirisha ibada fulani; mfano kama mtu alikithirisha sana saumu, basi ataitwa kupitia mlango wa wenye kufunga saum. Sy AbuBakr ataitwa kupitia milango yote, inamaanisha alikuwa mkamilifu wa kila ibada.
Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI 

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views