Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo. Tunaendelea na risala yetu kuhusu msafara wa Isra na Mi-'iraj.
Baada ya Kumshukuru Allah na kumtakia Rehma Mtume Muhammad ﷺ, hapo juu ni aya ya kwanza ya Sura Bani Israil, ambayo inazungumzia msafara wa miraji.
Tafsiri ya aya:
Utukufu ni Wake Yeye Aliyempeleka Mja Wake katika sehemu tu ya usiku kutoka Msikiti wa Haraam (Makkah) hadi Msikiti wa Aqsa (Palestina), ambao umezungukwa na Baraka Zetu, ili Tumuonyeshe baadhi ya alama zetu. Hakika Allah ndiye Mwenye Kusikia Mwenye Kuona.
Mtume Muhammad ﷺ alipoanza safari ya Masjidul Aqsa, njiani alimuona Mtume Musa akisali ndani ya kaburi lake. Hapa tunapata kufahamu kuwa Mitume si tu wapo hai ndani ya makaburi yao, bali huwa wanasali na pia hupata rizki.
Mtume Muhammad ﷺ alipofika Masjidul Aqsa, Jibrail alitoboa sehemu moja iitwao Sakhra na kisha kumfunga mnyama wao. Kisha Jibrail alitoa adhana juu ya Msikiti wa Sakhra na kurudi Masjidul Aqsa. Hapa Mitume wote walikuwepo na kila mmoja akawa anafikiria je ni Mtume Adam ambae ni baba wa binadamu wote, ndiye atakaesalisha leo? Au Khalili wa Allah, Mtume Ibrahim? Au ni Mtume Nuh kwani baada ya tufani ya zama zake, masuala ya uzaaji ulianza kupitia yeye. Lakini Jibrail alimshika mkono Mtume Muhammad ﷺ na kumpeleka mbele na kumuambia awa imamu wa Mitume wote. Baada ya sala, kila Mtume alisoma khutba ya kumsifu Mtume Muhammad ﷺ.
Baada ya hapo Mtume Muhammad ﷺ alifuatana na Jibrail kuelekea mbinguni. Kuna riwaya 2; (1) walienda kumtumia mnyama yule yule Buraaq au (2) Miraji ni jina la ngazi mmoja na hivyo walitumia ngazi hiyo kuelekea juu. Walipofika mbingu ya 1, mlango ulikuwa umefungwa. Jibrail alipiga hodi na kuulizwa ni nani? Alijibu mimi Jibrail niko na Mtume Muhammad ﷺ. Baada ya kuulizwa kama Mtume Muhammad ﷺ ameitwa, Jibrail akajibu kuwa ndiyo.
Mtume Muhammad ﷺ alimuona mzee mmoja ambae kila akiangalia vivuli upande wake wa kulia basi hutabasamu lakini anapoangalia vivuli upande wa kushoto basi hulia. Mtume Muhammad ﷺ aliuliza ni nani huyo na kwa nini mara hutabasamu na mara hulia? Jibrail alijibu kuwa msalimie huyu ni mtume Adam, upande wake wa kulia ni watoto wake walioleta imani na ndyo maana hutabasamu akiwaona. Wale wa kushoto ni watoto wake waliokataa imani na ndyo maana hulia akiwaona.
Mtume Muhammad ﷺ alianza kuchupa mbingu moja baada ya nyingine huku akikutana na Mitume kila mbingu. Mbingu wa 2 alikutana na Mtume Yahya na isa, ya 3 Mtume Yusuf, ya 4 Mtume Idris, ya 5 Mtume Harun, ya 6 Mtume Musa nay a 7 alikutana na Mtume Ibrahim aliekaa kwa kuegemea Baitul Maamur. Baitul Maamur ni kibla ya Malaika mbingu ya 7, ambamo kila asubuhi na jioni Malaika 70,000 wapya huingia hapo. Mtume Muhammad ﷺ aliwasalisha Malaika.
Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah.
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...