Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo.
Mwezi wa nane katika Kalenda ya Kiislamu ni Sha'abaan. Utukufu wa mwezi huo juu ya miezi mingine ni kama ule wa Mtume ﷺ juu ya Mitume wengine.
BAADHI YA TAREHE MUHIMU:
Qiblah ilibadilishwa kutoka Baytul Maqdis na kuwa Al Kaaba.
Imam Abu Hanifa, mmoja kati ya Maimamu wanne, kuiaga dunia hii tarehe 2.
Imam Husein RadwiyAllahu kuzaliwa tarehe 6.
Usiku wa kuwa huru na moto wa Jahannam (au kasimatu rizki) tarehe 15.
KUBADILIKA KWA QIBLAH:
Baytul Maqdis (Msikiti wa Aqsa) ulikuwa ndiyo Qiblah ya mwanzo ya Waislamu. Karibu Mitume wote waluielekea katika sala zao. Mtume ﷺ alitamani sana kuelekea Al Kaaba tangu mwanzo tu.
Kila Mtume ﷺ aliposali akielekea Baytul Maqdis, Mayahudi hukasirika sana na hata husema "inakuaje Mtume wenu anawaamrisheni kutenda kinyume na Mayahudi na inapokuja swala ya ibada basi anauelekea mji wetu (Jerusalem)?" Mtume ﷺ hakujisikia kabisa vizuri kwa maneno hayo ya Mayahudi na alitamani sana kuelekea Al Kaabah.
Sub-Hanallah! Mara moja Allah Akatelemsha aya inayoelezea: "Tunashuhudia ukiinua uso wako mara kwa mara mbinguni. Basi tutakuelekeza upande wa Qiblah uiridhiayo wewe. Elekea Msikiti wa Haraam (Al Kaaba) sasa hivi, na enyi Waislamu! Elekeze nyuso zenu huko pia, popote mlipo .." (Quran Tukufu 2:144). Zingatieni watukufu Waislamu kuwa badiliko la Qiblah limetokea kwa sababu tu ya kumridhisha Mtume ﷺ. Kuanzia hapo qiblah yetu ni Al Kaaba huko Makkah.
IMAM ABU HANIFA:
Jina lake hasa ni Nooman bin Thabit bin Zuta bin Mah. Alizaliwa katika mji wa Kufa, Iraq, mwaka wa 80 Hijria. Alikuwa katika zama tukufu wa Tabi'in (wale waliowafuata Masahaba).
Amepokea Abu Huraira RadwiyAllahu Anhu kuwa Mtume ﷺ amesema kuwa : Katika ummah wangu atakuja mtu ataitwa Abu Hanifa. Siku ya Qiyama yeye (Abu Hanifa) ndiye atakuwa taa ya ummah wangu. Hadithi nyingine imeeleza kuwa "katika kila karne idadi Fulani ya ummah wangu utakuwa na daraja ya juu; Abu Hanifa atakuwa na daraja ya juu zaidi katika zama zake".
Miongoni mwa Masahaba aliokutana nao ni Sayyiduna Anas bin Maalik, Sayyiduna Sahl bin Saad na Sayyiduna Abul Tufail Amir bin Wathila RadwiyAllahu Anhum. Imam Abu Hanifa alipata elimu ya dini kupitia baadhi ya Masahaba na wanazuoni wapatao kama 4,000. Baadhi ya Masahaba ni Sayyiduna Hammad Basri, Sayyiduna Ata bin Abi Rabah, Sayyiduna Ikramah, Sayyiduna Imam Baaqir, Sayyiduna Imam Jafar Saadiq, Sayyiduna Abu Ali, Sayyiduna Abu Hurayrah, Sayyiduna Abdullah Ibn Umar, Sayyiduna Aqabah bin Umar, Sayyiduna Safwaan, Sayiduna Jabir na Sayyiduna Abu Qatadah RadwiyAllahu Anhum.
Imam Abu Hanifa alikuwa mfanya biashara na kila Ijumaa alikuwa akitoa sarafu 20 za dhahabu kwa wasiojiweza kama sadaka. Kwa muda wa miaka 40 Imam alisali sala ya Alfajiri kwa udhu ule ule wa sala ya Ishai (kwa maana usiku kucha alikuwa katika ibada bila ya kulala). Imam alihiji mara 55. Alihitimisha Quran Tukufu kila siku kimoja na usiku kimoja. Pia alikuwa akihitimisha Quran Tukufu katika rakaa moja ama mbili. Alikuwa mcha Mungu sana kiasi cha kufunga mwaka mzima (isipokuwa siku zile 5 zilizokatazwa) kwa muda wa miaka 30. Mahala alipofariki, alisoma Quran Tukufu 7,000.
WATUKUFU WAISLAMU TUPO JAMANI!!!
Mwezi Sha'abaan mwaka 150 Hijria, Imam aliiaga dunia hii huko Iraq akiwa katika hali ya sala, akiwa na umri wa miaka 70. Jeneza lake lilisaliwa mara 6 na kila mara waumini wapatao 50,000 walihudhuria na wengine walikuja kumuombea kwenye kaburi lake kwa siku karibu 20 hivi.
Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah.
0 comments:
Post a Comment
Enter your Comment here...