Ads 468x60px

Mar 28, 2013

Fadhila Za Elimu - PT 1 (Kiswahili)



Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo. Je mnakumbuka dua inaponyesha mvua??

Mwezi/ Mfungo tulionao ni Jamadi-ul-Awwal au Mfungo 8. Kwa kuwa sikuona historia ya mwezi huo, nimeona ni bora nilete mada nyeti ambayo wengi wetu tuko mbali nayo kwa namna Fulani hivi. Nayo ni kuhusiana na elimu ya dini.

AYA: INNAMA YAKHSHALLAHA MIN IBAADIHIL ULAMAA.

Tafsiri ya aya:
Hakika wamchao au wenye kumuogopa Allah zaidi katika viumbe vyake ni wanazuoni tu.
Kwani mimi na nyinyi hatumuogopi Allah? Sasa imekuaje hapa wakatajwa wanazuoni tu ni wenye kumuogopa Allah?
Ieleweke kuwa mwenye kuwa na elimu zaidi, ndiye mwenye kumuogopa zaidi Allah. Mwenye kuwa na elimu zaidi, atakuwa na maarifa zaidi; mwenye kuwa na maarifa zaidi, atakuwa na hofu au ucha Mungu zaidi na mwenye kuwa na hofu zaidi ya Allah basi atajipatia ukaribu zaidi wa Allah.

HADITHI: Ameeleza Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam kuwa katika Ufalme wa Allah, mwenye kuwa na maarifa zaidi kuliko kiumbe chochote ni MIMI, mwenye kuwa na ucha Mungu zaidi ni MIMI na mwenye kujaaliwa zaidi ukaribu wa Allah pia ni MIMI. Kama inavyoelezea aya ya Sura An-Najmi kuhusiana na msafara wa miraji : “FAKANA QAABA QAUSAINI AU ADNAA, FA-AWHAA ILAIHI MAA AWHAA”. Allah na Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam walikaribiana sana kama vile upinde na kamba yake, kisha Mola Akamjaalia wahyi ya chochote alichomjaalia.

Ili kuelewa zaidi, tumia mfano huu: sote tunafahamu kuwa nyoka ni mnyama mmoja hatari sana. Ieleweke kuwa mwenye kuwa kwenye hali ya ihram, haruhusiwi kuua mdudu wa aina yoyote ndani ya Msikiti wa Haraam, Makkah; la sivyo atalipa kaffara. Lakini anaruhusiwa kumuua nyoka kama atajitokeza Msikitini hapo na hata kama yumo katika ihram na pia hatalipa kaffara.
Ikiwa kijana mwenye umri wa miaka 20 akiletewa nyoka, bila shaka atakimbia kwani anafahamu ukali wa nyoka na madhara yake. Nyoka huyo huyo akiletwa mbele ya mtoto wa miezi 5, si ajabu mtoto hataogopa, kwani hana maarifa ya nyoka wala madhara yake. Hivyo jinsi maarifa itakuwa zaidi ndivyo hofu itakuwa zaidi.

Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
 Kind Regards,

Muhammad KHATRI 

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views