Ads 468x60px

Feb 3, 2013

Maulidi - Part 4 Q&A

Assalaamu alaikum,

Natumai hamjambo.

Kuna wenzetu watatu wameuliza maswali, haya hapa chini pamoja na majibu:-

1) SWALI: Je naweza kufunga siku niliyozaliwa?

JIBU: Kufunga inawezekana siku yoyote isipokuwa siku za Idi na Ijumaa. Kwa hali hii kama siku yako ya kuzaliwa ni Ijumaa basi itakubidi uongeze siku moja; yaani ufunge Alhamisi na Ijumaa na si Ijumaa peke yake.

2) SWALI: Je tunaweza kufunga tarehe 12 Mfungo 6 au Rabi ul Awwal (yaani tarehe alimozaliwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam) kwani siku hiyo inahesabika siku ya Idi?

JIBU: Baadhi ya wanazuoni wanasema haina dosari katika kufunga siku hiyo na baadhi wanakataza kwa kuwa ni siku ya Idi kwa Waislam. Kifikra (yangu mimi binafsi) ni bora kutofunga kwa sababu ya kuwa siku ya Idi; heri kufunga siku za Jumatatu kwani ndiyo siku aliyozaliwa Mtukufu wa Daraja Swallallahu Alaihi Wasallam.

3) Swali: Napenda kujua kuhusu riba.

JIBU: Swali haifafanui ni kitu gani katika riba. Hata hivyo, labda tu nielezee kwa jinsi nilivyoielewa. Riba ni haramu katika Uislamu; iwe kupokea au kutoa au hata kushuhudia wanapopeana riba. Hata hivyo ieleweke kuwa kuwa hukumu hiyo ni pale ambapo ufalme/serikali/ benki/ taasisi ya fedha ni ya Kiislamu asilimia 100%. Mfano, kwa hapa Tanzania, kwanza Serikali yetu si ya Kiislamu na pia benki zetu zote si za Kiislamu isipokuwa Amana na ZPB. Hivyo riba wanayotoa benki zetu za kawaida haitahesabika kuwa ni riba; ila sisi kuwapa riba itakuwa si sahihi. Kwa kuwa swali haikuwa wazi, nimejaribu kuelezea kwa muhutasari tu. Ila kama kuna la ziada, basi naomba msisite kuuliza.

JazakAllah,

Kind Regards,

Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views