Ads 468x60px

Feb 26, 2013

Sheikh Sayyid AbdulQadir Jilani - PT 2‏ (Kiswahili)



Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo.
Kwanza kabisa kuna maswali yameulizwa na mwenzetu, niyajibu kwa ufupi na kisha niendelee na risala.

1.     1) Baba yake Abu Sale alikuwa anaitwa nani? Anaitwa Abdullah.
2.     2) Je ni Baba yake Abu Saleh au ni Saleh mwenyewe aliekula tunda hilo? Abu Saleh ndiye aliyekula tunda
3.     3) Huyo mke aloozeshwa alikuwa ndo mke wake wa kwanza au alikuwa na mke mwingine kabla yake? Alikuwa mke wa kwanza
4.     4) Nini yalikuwa mahari ya mke huyo? Katika ufuatiliaji wangu, sijafanikiwa kupata mahari!

Sh AbdulQadir alizaliwa Ramadhani mosi na siku hiyo walizaliwa watoto wa kiume 1,100 na wote wakawa Mawalii wa Allah. Karama yake ilidhihirika papo hapo kwani yeye hakunyonya muda wa kufunga saumu hadi muda wa futari. Habari hizi zikawa maarufu kiasi cha kwamba mwaka uliofuata kulitokea hitilafu katika mwezi. Hivyo ilishauriwa kwenda nyumbani kwa Sh AbdulQadir ili wamuulize mama yake kama mwanae amenyonya leo au la? Jibu ilikuwa hapana na hivyo ikaamuliwa kuwa mwezi uliandama.

Akiwa mtoto mdogo, Sh AbdulQadir alijitenga na mambo ya kucheza ambayo watoto wengine huwa ni kawaida kucheza. Sh AbdulQadir alikuwa akifanya ibada ya Allah na alipowaona watoto wakicheza na hujisikia kuungana nao, basi husikia sauti ikisema : “njoo kwangu ewe uliyetukuka”. Siku za mwanzo baada ya kusikia sauti hukimbia kwa mama lakini kadri siku zilipoenda alizoea na hujishughulisha katika ibada. Alipofika umri wa miaka 5, mama yake alimuandikisha katika Madrassa moja ya Jilan. Pindi Sheikh alipofika Madrassa, basi Malaika husema “mpisheni Walii wa Allah”. Alipofika umri wa miaka 18, alimuombab idhini mama yake kwenda kusoma mjini Baghdad. Zama hizo watu walikuwa wakisafiri kwa mguu ama ngamia na njia nyingi hukatiza porini ambapo wanyang’anyi hujificha. Mama alimuombea na kumpatia dinari 40 (thamani ya pesa nyingi mno zama hizo), alizomshonea kwenye koti lake, kisha akamuusia daima aseme ukweli tu. Sheikh akamuahidi mama daima atasema kweli na baada ya kuombewa akaanza safari pamoja na msafara (kama ilivyo kawaida ya zama hizo).

Baada ya kupita vijiji kama viwili, msafara ulivamiwa na majambazi. Kila alichonacho (chenye thamani) walinyan’ganywa. Majambazi walipomfikia Sheikh, wakamuuliza alichonacho, alijibu ana dinari 40. Majambazi wakampuuza kwa kufikiria kuwa kijana anawatania tu. Majambazi walipokutana kwa kiongozi wao wakiwasilisha walichonyan’ganya, wakasema kuna kijana anadai eti ana dinari 40. Kiongozi akaamuru aletwe huyo kijana na kuanza kumhoji kuhusu hizo pesa. Sheikh akawaambia alikoficha.

-

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views