Ads 468x60px

Jan 20, 2014

Maulidi - PT 2 (Kiswahili)Natumai hamjambo na mpo katika maandalizi ya shamra shamra za Maulidi (mazazi ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam.
Tunaendelea na risala kuhusiana na sifa za Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam kama ilivyo ndani ya Quran na Hadithi na pia masuala ya wapingao Maulidi.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, aya hapo juu ya 15 kutoka Sura Al Maidah (15), inayozungumzia kuletwa kwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam.
TAFISIRI: Enyi watu wa Kitabu! Amekujieni Mtume wetu anaekufichulieni mengi mliyokuwa mkiyaficha katika kitabu na anaesamehe mengi. Bila shaka imekujieni kutoka kwa Allah Nuru na Kitabu kinachobainisha.
Allah alipotaka kumtuma Mjumbe wake Ardhini, Aliumba udongo wa Adam Alaihissalaam. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam amesema: “Mimi nilikuwa Mtume tangu Mtume Adam Alaihissalaam alikuwa baina ya udongo na maji”.
Kutoka bapa la Uso mmoja hadi nyingine, Nuru hii iliwekwa kwenye bapa la bwana Abdullah RadwiyallahuAnhu, baba wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam. Nuru hiyo baadae ikakaa kwenye tumbo la Mama Amina RadwiyallahuAnha, mama wa Mtumu Swallallahu Alaihi Wasallam. Katika ujauzito wa miezi 9, hakuhisi tabu wala kuona alama yoyote iliyo ya kawaida kwa kila mjamzito. Pia kila mwezi alipata habari njema kutoka kwa Mitume wa Allah. Mama Amina RadwiyAllahu Anha anaelezea kuwa siku ya kuzaliwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam ilipofika, ilikuwa wakati wa Alfajiri ya Jumatatu alipoona kundi la watu ikitelemka kutoka mbinguni wakiwa na bendera 3. 1 waliiweka kwenye ua la jumba lake, 1 juu ya paa la Al-Kaaba na 1 juu ya Masjidul Aqsa. Baadae wanawake wachache walimjia na kujitambulisha. 1 alikuwa Mama Maryam, Mama wa Mtume Isa Alaihissalaam, wa 2 alikuwa Aasiya mke wa Firauni, naa 3 alikuwa Mama Hajra mke wa Mtume Ibrahim Alaihissalaam. Wanawake wengine walikuwa watukufu wa Peponi. Wote hao walikuja kumhudumia. Baada ya matukio hayo ndipo Nuru ya ulimwengu, Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam alizaliwa. Quran ikatangaza kuwa: “Hakika imekuja kwanu kutoka kwa Allah Nuru na Kitabu kilicho wazi”.
Wanazuoni mashuhuri wameeleza kuwa usiku wakuzaliwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam ni bora zaidi kuliko usiku wa LaylatulQadri, na kuwa mwezi wa Rabi-ul-Awwal ni tukufu zaidi kuliko mwezi wa Ramadhani. Sababu yake ni kuwa usiku waLaylatul Qadri, Quran imetelemka wakati usiku wa kuzaliwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, amezaliwa yule iliyomtelemkia Quran.
Ulimwengu mzima ulifurahi kakuzaliwa kwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, na Al-hamdulillah hata leo wapenzi wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam wanaadhimisha siku hiyo kwa furaha kubwa. Hata hivyo, kuna maadui wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam wasemao kuwa kusherehekea ni upotovu na ubadhirifu. Allah awajaalie akili na imani sahihi. Allah atujaalie sisi sote mapenzi ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam.
Amin              Amin              Amin
DALILI NA UTHIBITISHO WA KUSHEREHEKEA NA KUADHIMISHA MAULIDI KUPITIA QURAN TUKUFU NA HADITHI.
Allah Amesema ndani ya Quran Tukufu : “Sema (Ewe Mtume uwaambie) kwa Fadhila za Allah na Rahma Zake inatakiwa wafurahikie, hiyo ni bora kwao kuliko waliyoyakusanya”. (Sura Yunus: 58)
Katika aya hii Allah Anatuagizia tufurahikie pindi tunapopata Fadhila na Rahma zake. Bila shaka, Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam ni Fadhila na Rahma kubwa kutoka kwa Allah. Allah Anatuambi : “Hatukukutuma (Ewe Mtume) ila uwe Rahma kwa walimwengu”. (Sura Ambiya: 107)
Allah Amesema ndani ya Quran Tukufu : Ewe Mwenye Kusimulia habari za uficho (Ewe Mtume) Hakika sisi tumekutuma uwe Shahidi na Mbashiri na Mwonyaji. Na mwitaji kumwendea Allah kwa idhini Yake, na jua lenye kuangaza. Na wabashirie Waumini kwamba wana fadhila kubwa itokayo kwa Allah”. (Sura Ah-zaab: 45-47). Allah pia akasema : “….na uwakumbushe siku za Allah …” (Sura Ibrahim: 5)
Wafasiri wanasema kuwa “siku za Allah” inamaanisha siku ambamo Allah Amewazawadia binadamu; kama vile kuongoka kwa Bani Israil na utumwa wa Firauni. Hivyo zawadi kubwa kuliko zote kutoka kwa Allah ni kuletwa (au kuzaliwa) kwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam na hii inamaanisha kuwa Maulidi ya Mtume ni siku ya Allah; kwa hiyo ni lazima ikumbukwe/ itajwe. Pia Allah Anasema : “Hakika Allah Amewafanyia wema mkubwa Waumini kwa kuwaletea Mtume aliye miongoni mwao …” (Sura Aali Imran: 164).

Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam mwenyewe alipoulizwa kuhusu kufunga (swaum) kwake kila siku ya Jumatatu, alijibu : “ni siku nilimozaliwa” (Al Muslim). Hii inaonyesha kuwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alifunga siku ya Jumatatu kumshukuru Allah kuzaliwa kwake. Pia Abu Jahal alipokufa, mmoja katika ndugu zake (Sayyidina Abbas RadwiyAllahu Anhu – Amii yake Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam) alimuota na kumuuliza hali yake baada ya kufa kwake. Abu Jahal alimjibu: ninaadhibiwa sana ila kila siku ya Jumatatu ninapunguziwa adhabu, pia ninaposikia kiuu basi hunyonya kidole changu cha shahada na husikia nafuu kidogo. Baba wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam ni kaka yake Abu Jahal, hivyo siku alipozaliwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, Abu Jahal aliletewa taarifa na mtumwa wake (Thuwaibah) kuwa nyumbani kwa kaka yako amezaliwa mtoto wa kiume! Kwa furaha hiyo, Abu Jahal alimuashiria kwa kidole chake cha shahada kumuacha huru mtumwa wake huyo. Wanazuoni wanasema ikiwa kafiri mkubwa na adui mkubwa wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam anapata nafuu katika adhabu yake kwa kufurahia tu kuzaliwa kwa mtoto wa kiume, je Muislamu akisherehekea Maulidi ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam hatapata faida?? (Al Bukhari). Wanaelezea pia kuwa mwenye kusherehekea Maulidi kwa heshima na mapenzi ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, basi atazawadiwa na Allah. Wanaelezea pia kuwa mikusanyiko ya Maulidi huwa ya heshima na mapenzi kwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam tu. Pia ieleweke kuwa shetani alilia mno alipozaliwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam na hivyo wanazuoni wanasema kuwa mwenye kuhuzunika na Maulidi, basi anamfuata shetani na huu si mwenendo wa Waislam.
Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views

Follow by Email