Ads 468x60px

Sep 20, 2016

Sayyidina Uthman bin Affaan (Kiswahili)

Assalaamu alaikum,

Natumai hamjambo. Leo ni mwezi 18 Dhul Hujjah (Mfungo 3), ambamo Khalifa wa 3 wa Kiislam, Sayyidina Uthman bin Affaan RadwiyAllahu Anhu, aliuawa kikatili. Siku hiyo mashia husherehekea kwa kumtesa mbuzi wakishabishia Sayyidina Uthman! Ifuatayo ni fadhila zake kwa kifupi.Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad , aya hapo juu ya 29 ya Sura ya 48 AL FATAH, inayozungumzia fadhila za Makhalifa.
TAFSIRI: Muhammad ni Mtume wa Allah, na wale walio pamoja nae ni wakali kwa makafiri ila ni wenye kuhurumiana wao kwa wao (aya inaendelea).

Baada ya kusilimu kwa Sy Abu Bakr, Mama Khadija, Sy Ali na Zaid bin Haritha, aliyefuata kusilimu ni Sy Uthman. Ami yake alichukia sana na hivyo alimfungia chumbani kwa siku kadhaa, ila baadae alikereka na kumwacha.

Miongoni mwa fadhila kubwa alizojaaliwa ni ya DHUNNUREIN (yaani mwenye Nuru 2). Maana yake kuwa aliwaoa mabinti wawili wa Mtume mmoja baada ya mwingine. Kwanza alimuoa Ruqaiyya, hiyo ilikuwa kabla ya Mtume kutangaza utume. Mwaka wa pili wa hijria, wakati wa vita vya Badri, Ruqaiyya alikuwa mgonjwa na hivyo Sy Uthman hakuweza kushiriki vita hivyo, ila anahesabika miongoni mwa Masahaba wa Badri. Wakati Waislamu wanarejea na ushindi kutoka vitani, Ruqaiyya alikuwa akizikwa. Baada ya hapo alimuoa Umme Kulthum. Mtume alisema lau kama ningekuwa na mabinti 40, basi mmoja baada ya mwingine ningewaozesha na uthman. Pia hakuna Mtume yeyote aliyewaozesha zaidi ya binti mmoja kwa mtu mmoja tu isipokuwa Mtume .

Sy Uthman alikuwa na moyo wa kujitolea kwa ajili ya Allah na Mtume. Kwa ajili ya vita fulani alijitolea ngamia 300 kwa ajili ya Uislamu. Pia huko Madina, siku za mwanzoni kulikuwa tatizo la maji. Myahudi alikuwa na kisima ila aliwatoza pesa Waislamu kuwapa maji, lakini Sy Uthman aliinunua kisima hicho na kutoa wakfu kwa Waislamu. Vilevile aliihama mji wake wa Makkah katika mbili tofauti kwa ajili ya Uislam; kwanza aliihamia Habash (kwa sasa Ethiopia) na baadae mji wa Madina. Pia Hadithi 146 zimepokewa riwaya na yeye.

Mmojawapo ya kazi kubwa aliyofanya ni kukusanya Quran katika lugha halisi ya Kikureish na kuiweka alama za fat-ha, kisrah n.k. Kisha aliisambaza sehemu tofauti na pia aliwatuma wasomaji wawili kuwafundisha Waislamu wa sehemu hizo.

Wakati wa ukhalifa wake, nchi kama Roma, Qabras, nchi nyingi za Afrika, Hispania na sehemu kubwa ya Iran zikawa mikononi mwa Waislam.

Hakika Mayahudi wamekuwa maadui wakubwa wa Waislam tangu enzi hiyo. Walianza propaganda zao za kutaka kuleta mchafuko miongoni mwa Waislam. Wakaanza kuzua fitna dhidi ya gavana (kwa lugha ya sasa tuseme raisi) wa sehemu mbalimbali.Mmojawapo akiwa gavana wa Misri ambae walitaka aondolewe na nafasi yake ichukuliwe na Muhammad bin AbuBakr. Katika hali hii, waliandika barua na kumkabidhi mjumbe wa Sy Uthman na kumdanganya kuwa asiisome hadi kumfikia Sy Uthman. Njiani wasafiri walimkamata na kumhoji anakoelekea na hatimaye kuchukua ile barua. Kumbe mliandikwa "popote utakaposoma barua utamuua Muhammad bin AbuBakr" na kupigwa muhuri wa Sy Uthman. Waislam waliposomewa barua hii walimjia juu sana Sy Uthman na hatimaye kumfungia chumbani kwake. Sy Ali alipomuuliza Sy Uthman kuhusu mjumbe kama ni wa kwake na muhuri kama ni wake pia, alijibu ndiyo ila aliapa kuwa yeye hana taarifa kuhusu kilichoandikwa kwenye barua hii. Mwishowe aliuawa shahidi kikatili sana. Kwa karibu siku 40 alikaa na kiuu, alifunga saumu kila siku. Siku moja kabla ya kuuawa, alimuota Mtume aliyemwambia kuwa yeye Mtume anafahamu kwa matatizo anayoyapata na kuwa anafunga kila siku. Ila alimbashiria kuwa kesho yake atafuturu pamoja na Mtume.

Sy Uthman alikuwa akisoma Qurani, wakati adui alipoingia nyumbani kwake kupitia paa na kumpiga panga kichwani na damu ya kwanza kumwagika kwenye aya aliyokuwa akisoma: FASAYAKFIKA HUMULLAHU, WAHUWAS SAMIUL ALIM; Allah ndiye mwenye kukutosheleza, bila shaka Allah ndiye Mwenye Kusikia Mwenye Kujua.

Hii ni mmojawapo ya karama ya Sy Uthman. Mkewe alipiga kelele sana kutaka watu waje kumsaidia lakini kwa kuwa vurugu za wenye kutaka kumuua zilikuwa kubwa mno, alishindwa kusikika.

Maswali / maoni yanakaribishwa.

JazakAllah,

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views

Follow by Email